Timu ya Taifa ya Shelisheli imewasili leo mchana jijini Arusha ikitokea Nairobi, Kenya kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (U23).

Mechi hizo zitachezwa Julai 27 na 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta, jijini Arusha. Timu hiyo imefikia kwenye hoteli ya ya Markelly’s.

Shelisheli imewasili na wachezaji 24 na viongozi sita akiwemo mchezaji wa kulipwa Kevin Betsy. U23 inaendelea na mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam chini ya Kocha Jamhuri Kihwelo na inatarajia kuondoka Julai 25 mwaka huu kwenda Arusha tayari kwa mchezo huo.

Pia Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewajumuisha kwenye kikosi cha U23 wachezaji Juma Seif Kijiko wa Yanga, Haruna Moshi wa Simba na Gaudence Mwaikimba ambaye msimu huu ameombwa usajili Moro United.

Lengo la Poulsen ni kuangalia kiwango cha wachezaji hao ili kuona kama anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho Agosti 10 mwaka huu kitacheza na Palestina katika mechi ya kirafiki itakayofanyika jijini Ramallah. Poulsen atataja kikosi hicho Julai 31 mwaka huu jijini Arusha baada ya mechi hizo mbili.

Boniface Wambura
Ofisa Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...