Na Joseph Ishengoma
MAELEZO, DAR ES SALAAM
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Chrisant Mzindakaya (pichani) kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa- NDC.
Taaifa iliyotolewa leo kwa Idara ya Habari na Wizara ya Viwanda na Biashara na kusainiwa na Katibu wake Mkuu Bi Joyce Mapunjo, imesema kuwa uteuzi huo umeanza tangu Julai 8,2011.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami kwa upande wake amewateua wajumbe wengine tia wa Bodi hiyo.
 
Wajumbe walioteuliwa ni Prof Idris Kikula ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Makenya Maboko (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Prof. Ntengua Mdoe (Mhadhiri Mwandamizi, chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine).

Wajumbe wengine walioteuliwa katika bodi hiyo ni Dkt Marcelina Chijoriga, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana Gabriel Masenga (Mkemia wa kampuni ya Far Chemical and Traveling Agency), Prof Abdulkarim Mruma (Giorogical Survey of Tanzania) na Bi Sondo (Wakili wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania).
Wengine ni Bi Eline Sikazwe (Mkurugenzi wa MAendeleo ya Viwanda, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Bwana Gideo Nassari ambaye ni Mkurugenzi wa NDC.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utendi huo utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2011

    ccm watachaguana tu hata kama wenye kuchaguliwa ni vikongwe. nyie mnaopiga makelele kila siku eti kazi zipewe vijana mkome. hawa watu ni from old school ambao elimu ya enzi zao ilikuwa chuma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...