Na Mwandishi Wetu.
KUNDI la Muziki wa Taarab la Five Star Modern Taarab limetoa wito kwa wasanii wenye uwezo wa kupiga gitaa la besi na Solo kujitokeza katika kufanyiwa usaili wa kujiunga na kundi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kiongozi wa kundi hilo Ally Jay alisema kwa sasa kundi hilo limefanikiwa kupata baadhi ya wasanii wa kuimba katika nafasi kadhaa.
Alisema kuwa wasanii wapya wameanza mazoezi lakini hata hivyo kuna baadhi ya vifaa vya muziki ambavyo vinahitaji watalaamu wa kuvitumia.
Alisema kuwa wasanii waliopatikana wa kuimba ni Mariam Mohamed, Musa Ally, Mafaloo Mzumbye, Juma Hamis,Shaban Hamis, Shaban Almas na Isha Junior.
Alisema kuwa kwa sasa wanaendelea kupokea wasanii pamoja na wanaoweza kupiga vyombo vya muziki ili kukamilisha bendi nzima.
“ Ni kwamba kwa sasa mimi natakiwa kuhakikisha kuwa ile hadhi ya kundi la Five Star inarudi kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Ally Jay.
Kundi hilo lilipoteza wasanii wake 15 katika ajali ya basi walilokuwa wakisafiria wakiwa wanatokea Mbeya kwenye moja ya shoo zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...