Usiku wa Kuamkia Jana Tumempoteza Ndugu yetu Boniface Kasyanju aliekuwa akijulikana kwa wengi kwa jina la Uncle Bonny.
Uncle Bonny Ni Mdogo wa Mzee Martin Kasyanju ambae ni mmiliki wa Bendi ya FM Academia. Kwa Wapenzi wote wa FM Mtamkubuka Uncle Bonny alikuwa hakosi Getini kwenye show zote za FM. Alikuwa ni mmoja wa Viongozi na Msimamizi wa Shughuli zote za Bendi.
Uncle bonny wa Kwanza Kushoto( Mwenye kofia nyekundu) Enzi za Uhai wake.
Hapa bendi ya FM ikiwa Mjini Arusha.
MAZISHI YAKE YATAKUWA LEO SAA 10 JIONI KATIKA MAKABURI YA KINONDONI
Binafsi Alikuwa Mtu wangu wa Karibu sana, Mcheshi na Mshauri Mzuri.
Tulimpenda lakini Mungu Kampenda Zaidi.
RIP Boniface.
Jose Mara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...