Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad akionesha  na baadhi ya viatu walivyokabidhiwa na Meneja wa Grand Malt Bi Consolata Adam. Waziri wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad (kushoto) akipokea jezi kutoka kwa Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar itakayopambana na timu ya Klabu ya Wazee ya Arusha Septemba 8, mwaka huu. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Baraza, Mbarouk Mussa. Grand Malt ambayo imetoa vifaa hivyo vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10, ni wadhamini wa bonanza litaloshirikisha pia vilabu vingine vya veterani. Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad akitangaza rasmi kuwa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kimeruhusiwa kudhamini michezo na shughuli mbalimbali kisiwani Zanzibar. Alitangaza jana mjini Zanzibar wakati Grand Malt ilipotoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 kwa ajili ya bonanza la veterani litakalofanyika Arusha Septemba 8, mwaka huu. Kulia ni Meneja wa kinywaji hicho, Consolata Adam na Makamu Mwenyekiti wa timu ya baraza, Mbarouk Mussa. (PICHA NA MARTIN KABEMBA) Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam (kulia) akihutubia katika hafla hiyo. Baadhi wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...