TAHADHARI KWA JAMII NA GIZA
 
Ankal pole na majukumu.
Leo naomba tukumbushane madhara yanayozidi kutukabili kipindi hiki cha GIZA KALI.
Katika kipindi hiki cha mgao mkali wa umeme kuna wachahe waliokumbwa na madhara makubwa pale umeme unapokatika au umeme unaporudi.
Wazazi,walezi jamii tumekuwa busy sana katika kutafuta kutokana na ugumu wa haya maisha ya sasa, huku tukihangaika tunakutana na tatizo la GIZA.

Wengi wetu tunarudi nyumbani usiku sana na kukuta hakuna umeme na watoto wetu wametumia mishumaa kwa shughuli zote hata kufanya homeworks zao.
Sio wote wanaoweza kuwa na generators, baadhi wanatumia waliobakia wanatumia taa za kuchaji, taa kuweka batteries ambazo kwa sasa zipo kwa wingi sana kila mahali.
Ninachotaka tukumbushane leo kwanza ni kuwa makini sana nan kuwakumbusha mara kwa mara wanaobaki majumbani kuzima vifaa vyetu ambavyo vinatumia umeme mara unapokatika ili unaporudi visipate madhara na hata kupelekea kuteketea kwa nyumba zetu.
Pili wazazi walezi na jamii kwa ujumla tuwe makini sana na matumizi ya mishumaa na ikibidi tununue zaidi tochi za kuweka batteries ikipatikana hela unaongeza taa za kuchaji ikizidi hela weka generator na ikizidi zaidi basi tuweke umeme wa solar kila kitu kina madhara lakini umakini pia uwepo likitoke la kutokea basi mungu atasaidia.
Tatu Jamii, dawa ya mbu (mfano doom, rungu hit, x-pel nk)  na moto ( moto wa mshumaa au moto wa kuwasha nje majalalani au hata mkaa) wanaobaki majumbani ni wajibu wetu walezi kuwapa mafundisho ya vitu hivi hatari sana. Usiingie chumba chenye mshumaa na kuanza kupiga dawa ya mbu ovyo, dawa ya mbu ikikutana na huo moto wa mshumaa matokea yake ni kuungua vibaya sana EPUKA. 

Pia tuwe makini sana na makopo ya dawa ya mbu yaliyokwishakutumika yanapotupwa majalalani yakishika moto yanalipuka vibaya na atakayekuwa karibu ataungua vibaya.
Jamii kwa haya machache tukiyazingatia na kuwapa darasa wanaobaki majumbani basi huenda kipindi hiki cha GIZA KALI madhara ya mishumaa kuunguza nyumba zetu au umeme kurudi mwingi na baadhi ya vifaa vya umeme kuharibika yatapungua sana.
 
Kila lakheri
Mdau Emmy/Liloemis Pub
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Maoni mazuri sana haya, natumai muheshimiwa sana TAA WA NESCORI atayasikia na huenda akatuonea huruma, kwa ujumla inakera, inatesa, na inafadhahisha...wenyewe mlishuhudia jana wakati wapinzani wa jadi wanapambana...hako ni ka mfano kadogo tu...fikiria ndio unafika nyumbani, unakanyaga kizingiti cha mlango, maana wengi tunawasili usiku kutokana na rafiki mkubwa wa huyu mheshimiwa anaitwa `Foleni'...
    'Baba huyo..baba huyo...' unaanza kuwasalimia watoto na kuwauliza mumefundishwa nini, mtoto analeta daftari kukuonyesha, anafungua ukurasa wa kawanza, mara taaa...haaa giza, mheshimiwa sana kafanya akzi yake...
    'Baba hakuna mshumaa, ..' unapapasa mfukoni, unajikuta huna kitu hela yote uliyokuwa nayo jamaa mmoja anayefanya kazi mlangoni mwa daladala keshaziwahi...masikini!
    Sina nia kuchekesha hapa, ila juhudi za ziada zinahitajika...mkumbuke wengine tunatumia LUKU...inamaana tumeshalipia hela kabla ya matumizi...hela hiyo ishalipia mishahara yenu nk...sasa huduma ipo wapi, hilo ni deni...haya UJUMBE MURUA MKUU, Naomba tutembeleane, siku moja moja sio mbaya, ...au unaogopa vibanda vya udongo..lol!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2011

    Mdau Emmy asante sana.tena sana..Dawa ya mbu na mshumaa sikuwa naiwazia kama "HAZARD"!!...Michuzi mimi nime-copy hii article na kui-print bila ruhusa yako mzee wa kazi.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2011

    Dada Emmy, asante sana kwa kutukumbusha na kutupa mambo mengine mapya ambayo wengine tumeyapata kutoka kwako.

    Hakika tukiyazingatia haya, tutapunguza sana madhara kwani nyumba nyingi zimeungua na kuleta madhara makubwa na kufika hata uhai wa Watanzania wenzetu kupotea kwa ajili ya huu mgao. Management ya mgao bado ni tatizo kwa watu tulio wengi. Tuzingatie aliyotuambia Dada yetu jamani.

    Hakika pia umefika wakati sasa kwa Serikali kuwa na msimamo thabiti wa kuondoa tatizo hili la mgao kabisa. Watanzania wa leo miaka 50 baada ya Uhuru hatustahili kabisa kuwa katika hali hii. Huku ni kurudi nyuma na kamwe si kwenda mbele.

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2011

    UBAKAJI< WIZI, MIGUU KUDUMBUKIA KWENYE MITARO, MAMBO MENGI TU HAWA TANESCO LAZIMA HUU MWAKA MZIMA WAWAPE WANANCHI UMEME BILA KULIPA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2011

    TATIZO LA WATANZANIA WAKATI WA DOWANS MLIPIGA KELELE MSILOLIJUWA MLIVYOJUWA NI MWARABU NDIO KABISA MKAJA JUU NA WAPINZANI WA CHADEMA WAKAJA JUU ZAIDI MKAZIMWA NA SOO LA BABU KIKOMBE SASA IMECHUKULIWA NA MMAREKANI SIJASIKIA HATA MPINZANI NAYE KUPIGA KELELE TUTAENDELEA HIVIHIVI GIZANI KWA TABIA YETU. BORA DOWANS LINGEWASHWA TUKAJUWA MOJA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 11, 2011

    nimefurahi na haya maelezo, kwakweli mie kopo la dawa ya mbu limeshawahi kunilipukia na kuniunguza vidole, paliuma sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...