Uncle Michuzi, 

hongera sana kwa jitihada zako za kuufahamisha umma juu ya mambo mbali mbali yanayo husu jamii yetu watanzania, Uncle kwakupitia Blog yetu hii ya jamii naomba niulize swali hili kwa wadau waliopewa dhamana ya mipango miji kwa Jiji la Dar limewakosea nini? 

Ukweli nikwamba Dar es salaam inapotea na kuja jiji lenye majumba marefu ya vioo. Ningependa tuziige nchi za wenzetu ambapo huwa tunaiga mambo mengi sana kutoka kwao, wenzetu hawabomoi majengo ya zamani nandio maana miji yao inavutia na wanapata watalii wengi japo hawana mbuga za wanyama kama wengi wetu wanavyo waza kuwa utalii utaimarishwa na mbuga za wanyama. 

 Naiomba serikali isaidie kuyalinda magengo machache ya zamani yaliyo bakia kwenye miji yetu Tanzania kwa manufaa ya Historia ya Nchi yetu, na kuepusha msongamano katika miji yetu.
  Mdau Sixmund Begashe akiwa katikati ya jiji la Helisinki –Finland na anakwambia mpangilio huu Foleni hapa itakuwa historia.
 Sehemu ya jiji la Stockholm – Sweden.
 Jiji la Helsinki – Finland, likionekana toka bandarini.
Watalii wakipita karibu na moja ya majengo ya kale yaliyopo katikati ya jiji la STOCKHOLMSWEDEN. Katika jengo hilo na mengine kama hilo,kuna makazi ya watu wenye kujiweza kiuchumi, kwa mujibu wa wakazi wa Stockholm. Foleni hapa haita tokea kamwe.

Mdau  SIXMUND J. BEGASHE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2011

    Mdau, Majengo ya kale yenye historia yapo na yanatunzwa vizuri tu. Nenda Zanzibar na Bagamoyo utayakuta tele. Sidhani kama kuwa na nyumba za nyasi kariakoo kutatuongezea watalii. Sikubaliani na wewe pia kwamba miji mikubwa Ulaya na marekani haina foleni, ingawa tunahitaji kutafutia ufumbuzi suala hilomfano kupitia ujenzi wa satellite cities kama ambavyo tayari mipango mbalimbali inatekelezwa. Kuna mambo mengi yanayokwamisha shughuli za utalii hususan Dar es salaam. Kubwa ni usalama mdogo wa mali na afya pamoja na ukosefu wa huduma muhimu za umeme, maji nk.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2011

    Anon wa kwanza nakubaliana na wewe asilimia 100. Foleni mimi nipo hapa kajimji kadogo tu cha mama basi saa 2-4 asubuhi na saa 10-12 jioni ni foleni tupu. Hawa jamaa wana kila mabarabara na mareli na mametro. Hii inatokana na watumiaji wa njia za usafiri kuongezeka. Hayo unayotuonyesha ni majengo yenye usanifu wa kizamani lakini yamefanyiwa matengenezo kuendana na wakati wa sasa. Niliwahi kupiga box la ujenzi London niliona wanavyoyafanyia ukarabati hayo majengo. Hayo majengo yamekarabatiwa kwa kutumia teknolojia ya leo na ni madhubuti sana. Huwesi kupewa kibali cha kujenga huku mpaka uonyeshe plan ambayo imepitishwa na mji husika ambao wanalinda usanifu wao.
    Dar es Salaam ikipanuliwa na mawizara yakienda Dodoma basi foleni itakwisha. Kwa sasa kila kitu ni Samora avenue. Wataalamu wa mipango miji wanatakiwa kupanga upya miji yetu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2011

    Hahahaah..huyu jamaa sijui katokea kijiji gani!! Anafikiri tatizo la dar ni foleni? Kaenda kuosha macho Ulaya akaona achukue hako kaphoto ili kuonyesha nae katembea..

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2011

    Anon wakwanza na watatu, kunahaja ya kutulia na kuelewa kinacho zungumziwa hapo, yaelekea ninyi mnamitazamo finyu sana. Tanzania inamaeneo makubwa sana ya wazi, kuweka majengo makubwa na kubomoa yazamani siyo sura ya maendeleo hata kido. Mimi nimesoma nje nimekaa nje na sasa naishi Dar, Ujenzi Dar ni kerooo, mvua kidogo tu ikinyesha kwa sasa utaona tatizo la foleni, maji machafu kila sehemu, niheri anae ishi kijijini kuliko anae ishi Dar kwa sasa. Hapa linazungumziwa jiji la Dar na inayo fanana na hiyo Zanzibar inapokea watalii wengi kwakuwa wametunza historia ya miji mikongwe, Bagamoyo yaelekea hujawahi kufika, kwa sasa watu wamesha anza kujenga majengo mapya katikati ya mji na kubomoa ya zamani, huu ni utumwa wakifikra tena nisinge penda kusikia mfano wa Marekani mwenye mfano huo anamtazamu mufu. Nikweli Dar inapoteza sura yake. Mdau alie tuma habari hii yupo sahii sana, namfahamu kasafiri sana, na likizo zake zote anazitumia kwa utalii njee kitu ambacho niadimu, yaelekea Anon wa tatu umeingia Dar leo hujui dhamani ya Majengo ya Kihistoria. Kwa sasa janaga la tetemeko sunami na mengine yakitokea kwa Dar watu wengi sana watapoteza maisha. Juzi tumesikia hata nyumba ya sanaa imevunjwa, haya ndio maendeleo? Dar ya sasa si ya miaka kumi iliyo pita. Tafakarini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2011

    Mdau ulieweka hii mada mimi nakuunga mkono. Tatizo letu tumetoka kwenye nyumba za udongo basi sisi magorofa ya vioo ndio tunaona maendeleo. Kuna majengo mazuri sana hapa Dar yamevunjwa kupisha ujenzi wa magorofa mapya wakati magorofa hayo yangeweza kujengwa katika mji mpya uliopangika kama unaotaka kujengwa Kigamboni. Majengo kama la Salamander au lile lililokuwa ofisi za Rita yangeweza kufanyiwa ukarabati kama lilivyofanyiwa jengo la TRA Samora au mgahawa wa Java wa zamani. Majengo memngi yaliokuwa ya kihistoria yamevunjwa na kupisha vikwangua anga ambavyo baada ya muda mfupi vitakua havina wapangaji maana kampuni zote kubwa zinahamia nje ya mji na na jiji linarudi kuwa makazi ya watanzania wenye asili ya kiasia tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...