JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali imehuzunishwa sana na tukio la jana wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame kati ya vilabu vya Simba na Yanga ambapo umeme ulikatika ghafla kwenye Uwanja wa Taifa. Wizara inawaomba radhi wapenzi wa soka wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa usumbufu uliojitokeza.
Tukio hilo ambalo siyo la kawaida halikutazamiwa na wananchi, hususani wapenda michezo, kwamba tukio la aina hiyo halitatokea Aidha, Serikali inawashukuru wananchi wote waliojitokeza uwanjani hapo kushuhudia mchezo wa jana kwa kuwa watulivu wakati wote wa tukio hilo hadi umeme Kwa kutambua uzito wa suala hili, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeunda Kamati ya watu wanne (4) kuchunguza sababu zilizosababisha umeme kukatika na kukosekana uwanjani hapo.
Kamati hiyo itaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Bi. Sihaba Nkinga. Wajumbe wengine ni Bw. Charles Bagenda,Mkuu wa Kitengo cha Umeme cha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw.Mohamed Kiganja, Kaimu Katibu Mkuu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Bi. Anna Chungu, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizarani.
Kamati itakamilisha kazi yake ndani ya siku saba (7) kuanzia kesho tarehe 12 Julai, 2011 na itakabidhi taarifa yake kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel J. Nchimbi (Mb).
Wizara inapenda kutumia fursa hii kuzipongeza timu za Simba, Yanga na Ocean View zilizoshiriki kwenye mashindano ya mwaka huu kwa kuonyesha kiwango kizuri cha mchezo na nidhamu ya hali ya juu.
Aidha,Wizara inaipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa kombe la Kagame, na Simba kwa kuwa washindi wa pili
Imetolewa na:-
KATIBU MKUU,
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Tarehe: 11 Julai, 2011
tukio la kukatika umeme siyo la kawaida kasema nani hiyo? na kuna haja gani ya kuunda tume ya kuchunguza ambao ulikatika kwenye mpira, huu ni kutafuta ulaji kwa kuunda tume ambazo at the end of the day are fruitless.
ReplyDeleteEe, sasa hiyo kamati ya watu 4 duh, hapo pesa tena! Mkishakamilisha uchunguzi huo, mtoe habari kama mlivyoa leo pamoja na hatua zitakazochukuliwa kwa wahusika. Wananchi tunataka nchi yetu ikimbie kimaendeleo lakini wahusika wakuu wanatembea, hapo tutafika kweli?! kalagabaho! Yaani nina hasira hadi zinamwagika!
ReplyDeleteha ha ha ha dah sasa unaunda tume ya nini?si kuna mgao?au basi iundwe tume kuchunguza kwanini kuna mgao!!yaani nchi inakoelekea inapotea kwa kweli kama maamuzi ya viongozi ni kama haya!!.hv kwel kwa akili ya kawaida mtu mmoja anaweza kuamua kweli kukata umeme kwa maksudi uwanja wa taifa?.hv waziri anashindwa kumuuliza direct Mkurugenzi mkuu wa Tanesco hadi aamue kuunda tume kwenye ishu ndogo kama hii?.tume itakula posho then ije na ripoti kuwa tatizo lilikuwa mgao au matatizo ya kiufundi..haha dah bora nibaki ughaibuni mpaka nizeeke!!
ReplyDeleteNi njama za simba baada ya kufungwa. Aliyezima ni mshabiki wa simba. Kwa ni hamjui hilo? Chunguzeni vizuri mtaujua ukweli.
ReplyDeleteMungu tusaidie na hawa viongozi wetu, Tume tena!tafadhali mtumie pesa zenu za mifukoni msichezee pesa zetu, tumechoka na tume sisizo na faida.
ReplyDeletejamani, katika akili y kawaida kabisa, kuna haja ya kuunda tume?
kwa nini kama alivyoshauri mtoa maoni hapo juu waziri wa wizara husika asitumie taratibu za kuwauliza wahusika hata pengine kupitia wizara husika?
Ni suala rahisi tu la kuwauliza TFF kwanza kwa kuwa ilifahamu kabisa kuna mgao, je, ilichukua tahadhari yoyote ya ama kuwasiliana na Tanesco kuwaomba waepushe ratiba ya mgao eneo hilo hadi kwisha kwa mechi na watu kuondoka au kuwa na standby generator?
kama ilifanya hivyo, tunarudi kwa Tanesco kuwataka watoe maelezo kwa nini walikata umeme wakati waliombwa kutofanya hivyo.
Simple and clear, kama ni TFF utaratibu uleule uliotumika kumfukuza Kaijage kwa kosa la kutopigwa wimbo wa Taifa utumike, mhusika aondolewe, kama ni Tanesco mhusika pia awajibishwe.
Narudia tena, tumieni pesa za mifukoni mwenu, tutaangalia kwenye ripoti ijayo ya Mkaguzi wa hesabu za serikali, tukiona mmetumia pesa zetu kwa hiyo tume yenu, safari hii tutawashtaki mahakamani kwa matumizi mabaya ya pesa zetu.
Jamani umeme unakatika kila siku tume ya nini??!! Huku ndio kutumia pesa za walipata kodi vibaya. Tayari TANESCO imelitolea tamko kuwa kulikuwa na hitilafu ya umeme, tume ya nini?
ReplyDelete"SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema hitilafu za kiufundi zilisababisha kutokea kwa hitilafu ya umeme juzi katika sehemu kubwa nchini na kusababisha mikoa kadhaa kuwa gizani kwa takriban saa tano. "
Wakiambiwa hawawezi kufanya maamuzi magumu wanalalamika..hili ni suala la Kumtask Meneja wa Mkoa wa Dar wa Tanesco pamoja na Mkiti wa TFF then ukweli utajulikana na hatua kuchukuliwa...hapo kuunda tume ni kukimbia majukumu ili mtu akiwajibishwa TUME isemekana ni mapendekezo ya TUME...
ReplyDelete