Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Henry Salewi akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wake wa mkutano. Kawaeleza waandishi waandike habari za kuielimisha jamii iachane na tabia ya kujichukulia sheria mikononi ya kuwasurubu wale wote wanaotuhumiwa kwa kujihusisha na makosa mbalimbali, tabia ambayo Kamanda amesema imekithiri mkoani Kagera na kuna haja ya kuirekebisha. picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Kagera
Home
Unlabelled
kamanda wa polisi kagera akerwa na tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hahaha slow news day...ebu nitafutie kamanda wa polisi asiyekerwa na watu kujichukulia sheria mkononi...nothing new here!
ReplyDeleteMi napenda sana wananchi wanavyojichukulia sheria maana polisi, mahakama hawana haki unampeleka mtuhumiwa anakurudia kesho kukuua. Sasa faida iko wapi? Tanzania kesi za uongo ni nyingi kuliko hata waliotenda kweli so what is the point? To kill them is real solution because we gonna reduce the population in magereza
ReplyDeleteyaani wee wewe anony wa tar 20 July saa 09:46 PM hujui usemalo. hao jamaa wanajichukulia sheria mkononi hawajui haki. mimi nawaita wapumbavu. samahani kwa kutumia neno kali lakini ndo wanachostahili. mfano juzi tu kuna mtu kaibiwa ba kakatwa mapaga mida ya usiku wa saa sita kwa maelezo yake. akasema aliyemkata mapanga na kumwibia ni fulani. kwamba aliweza kumtambua kwa jaketi alilovaa. wananchi kwa huo upumbavu wao wakakurupuka na kutaka kumuua mtajwa. hawakujiridhisha kwa namna yoyote kuhusika kwa mtu huyo. walishinwa kuangaia kama angalau kuna matone ya damu kwenye jaketi au limefuliwa,lakini waliamua kuua.
ReplyDeletenaomba hali kama hiyo imkute nduguyo au wewe ndo ujue maana ya kujichukulia sheriamkononi. kwani unaweza kuwa na visa na mtu, akipatwa na tatizo anakutaja wewe. kwa vile hakuna shera wala haki unauawa au nduguo anauawa ndo ujue usemalo.
bila kuwaadhibu hawataacha hiyo tabia. kamata wahisika wawe mfano. utaona kamaitatokea tena. maneno tu.
ReplyDelete