Ankal, 

Wawekee wadau hii ili waone! Angalia bajaj ilivyopigwa na starlet barabara ya Ali Hassan Mwinyi road mapande ya saa nane na ushei mchana huu, mtu kazaa wameumia na kuwahishwa gereji ya matibabu wakati vipando vyote viwili vimetelekezwa kunako tukio vikisubiri askari kanzu. Kuweni waangalifu barabarani,kama mna haraka mngepita hapa jana. 

Ni mimi Jumaa Kanyama

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    Siyo kwamba namtetea mwenye gari lakini hao madereva wa bajaj wengi hawana leseni na hawazingatii sheria za barabara. Mfano, wanatanua na kujipenyeza bila ya kuangalia kama kuna usalama wa kufanya hivyo kwanza.

    Wala hata hawaoneshi indicator kuwa wanakwenda kushoto au kulia wao kwa vile wanajua kuendesha basi ndiyo imekuwa leseni hiyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2011

    Inaonesha umelifurahiya hili tukio!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2011

    Wote wanaoendesha Bajaj na pikipiki hawana lessini alfu wengi wao ni wajanja wanjanja tu hata sheria za barabara hawazijui.Hayo ndo matokeo yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...