Ankal,
Wawekee wadau hii ili waone! Angalia bajaj ilivyopigwa na starlet barabara ya Ali Hassan Mwinyi road mapande ya saa nane na ushei mchana huu, mtu kazaa wameumia na kuwahishwa gereji ya matibabu wakati vipando vyote viwili vimetelekezwa kunako tukio vikisubiri askari kanzu. Kuweni waangalifu barabarani,kama mna haraka mngepita hapa jana.
Ni mimi Jumaa Kanyama
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
Siyo kwamba namtetea mwenye gari lakini hao madereva wa bajaj wengi hawana leseni na hawazingatii sheria za barabara. Mfano, wanatanua na kujipenyeza bila ya kuangalia kama kuna usalama wa kufanya hivyo kwanza.
ReplyDeleteWala hata hawaoneshi indicator kuwa wanakwenda kushoto au kulia wao kwa vile wanajua kuendesha basi ndiyo imekuwa leseni hiyo.
Inaonesha umelifurahiya hili tukio!!
ReplyDeleteWote wanaoendesha Bajaj na pikipiki hawana lessini alfu wengi wao ni wajanja wanjanja tu hata sheria za barabara hawazijui.Hayo ndo matokeo yake.
ReplyDelete