Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la mto Rufiji (RUBADA), Aloyce Masanja akifafanua jambo Dar es Salaam leo kuhusu mradi wa kuzalisha wanga kwa kutumia zao la muhogo. Kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya FJS,Frederic Scheer.

Na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

KAMPUNI inayojishughulisha na uzalishaji wa nafaka nchini, African Starch Development, kwa kushirikiana na kampuni ya FjS wanatarajia kujenga kiwanda cha zao za muhogo kata ya Bungu wilayani Rufiji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kampuni ya FjS, Frediric Scheer alisema lengo la ujenzi huo ni kuinua kipato cha wakulima na zao kwa ujumla.

Alisema kata hiyo inazalisha mhogo kwa kiasi kikubwa lakini hauna tija kwa wakulima na serikali, hivyo lengo ni kulifanya liwe na tija.

“Huu utakuwa ni mradi wenye kuleta ukombozi kwa wakulima wa kata ya Bungu na maeneo ya jirani ambapo kiwanda hicho kitawaoa ajira wananchi 2 00”alisema.

Aliongeza, kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kukusanya tani milioni nane za mhogo kwa mwaka, hivyo kitawapa fursa wakulima kuuza na kulima kwa wingi.

Mbali na ujenzi wa kiwanda hicho pia wakulima watapata mbegu bora zenye kuleta mazao haraka na kuhakikishiwa uhakika wa soko.

Alibainisha, mpango huo umeshakamilika na kiwanja kimeshapatikana ambapo mashine zitawasili hivi karibuni.

Alisema taasisi pia itakuwa na shamba mfano ili kutoa fursa kuendelea na uzalishaji pale inapotokea dharula ya zao kukosekana kwa wakulima.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA),Aloyce Masanja alisema mradi pia utaenda sambamba na ujenzi wa kambi ya vijana.

“Mradi huu una manufaa makubwa, pia tutajenga kambi ya vijana kwa lengo la kuwapa mafunzo vijana juu ya utunzaji na uzalishaji bora wa muhogo, kambi hiyo itakuwa endelevu” alisema

Masanja alifafanua, baada ya kuonyesha mafanikio, mradi huo utasogea kwenye kata nyingine za wilaya.

Alitaja kata hizo kuwa ni; Mlanzi, Mjawa, Mwambao, Kibiti na Mchukwi pamoja na Dimani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...