Paul Lamboni Ngilangwa
(1940-2003)
Baba yetu mpendwa leo hii tarehe 15/7/2011 umetimiza miaka 8 tangu ulipotutoka na kuzikwa kijijini kwako Makoga-Njombe. Baba japokuwa haupo nasi kimwili utaendelea kuwepo mioyoni mwetu kila siku.
Tunakukumbuka sana kwa ukarimu wako,busara zako, ucheshi, maonyo uliokuwa ukitupa na mshikamano ulioujenga katika familia na ukoo wako wa Ngilangwa kwa ujumla.
Baba unakumbukwa sana na wake zako, watoto wako na wenzi wao, wajukuu, wanaukoo wa Ngilangwa, marafiki na majirani.
Kauli yako ya ‘…wanangu elimu ndio itakuwa urithi wenu toka kwangu…’ imeendelea kutujenga katika kutafuta elimu katika pande mbalimbali za nchi na dunia.
Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi, tunaamini iko siku tutaonana tena!
Wakorintho 15:52-57
May Almighty good God Rest his Soul in Eternal Peace. Amen
ReplyDelete