Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad |
Na Mwandishi wa Maelezo,Zanzibar.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amewataka masheha na madiwani kushirikiana katika kuwafichuwa watu wanaojihusisha na magendo ya karafuu iil kuzuwia usafirishaji wa zao hilokwa nja ya magendo.
Akizungumza na viongozi hao pamoja na Makamanda wa vikosi ya ulinzi huko chuo cha Benjamin Mkapa Wete Pemba ikiwa ni mfululizo wa ziara yake ya siku tano kisiwani Pemba,Maalim Seif amesema suala la magendo kuanzia sasa ni mwisho.
Amesema iwapo viongozi hao wanaojishughulisha na vitendo vya magendo katika maeneo yao ni dhahiri vitendo hivyo vita punguwa.
Hivyo amewataka viongozi hao kusimamia na kuwajibika kulingana na nafasi zao juu ya udhibiti wa magendo ya karafuu na yoyote atakae bainika kufaya hivyo serikali itamchukulia hatuwa za kisheria ikiwa ni pamoja na kumvua uongozi wake.
Makamo huyo wa kwanza wa rais Zanzibar MaalmiSeif Sharif Hamad amelitakaShirika la Biashara la Zanzibar ZSTC kuhakikisha wafanyakazi i wake kuwa waadlilifu wakati wa ununuzi wakarafuu ili kupunguza malalamiko ya wakulima wanaopeleleka kuuza karafuu zao.
duh si alisema karafuu zitakua rukhsa kuuzwa binafsi? na kmkm italinda wananchi sio karafuu kusafirishwa?
ReplyDelete