Na Pardon Mbwate, wa Jeshila Polisi Kigoma
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa majambazi hayo yalikamatwa jana kwa nyakati tofauti mkoani humo yakijipanga kuteka magari na kupora mali za abiria.
Kamanda Kashai amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Leonard Ntaoyima(47), na Omari Ngoloye(30), wote wafanyabiashara wa Kijiji cha Katumbi katika Tarafa ya Buhimbi wakiwa na silaha moja aina ya SMG yenye nambari 3315435 pamoja na risasi tatu katika magazine wote walikamatiwa katika kijiji hicho katika Wilaya ya Kigoma mjini.
Watuhumiwa wengine ambao ni Raia wa Burundi ni Sylivanus Zehimana(27) na mwenzake Ndiwayo Safari(19), wote kutoka katika Kijiji cha Kinyinya nchini humno wakiwa na risasi 82 za SMG ambao walikamatiwa katika Kijiji cha Nyankwi kilichopokatika Tarafa ya Kifura Wilayani Kibondo.
Amesema kuwa kukamatwa kwa majambazi hayo kunatokana na taarifa za siri za Raia wema walizozitoa Polisi za kuwepo kwa watu hao kabla ya kuwekewa mtego na Polisi na kutiwa mbaroni kabla ya kufanya uporaji.
Kamanda Kashai amesema kuwa silaha hiyo ambayo ilikuwa imetumbukizwa kwenye mfuko wa rambo ilikuwa ikitumika katika utekaji wa mabasi na uporaji wa mali za abiria katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kamanda huyo amewashukuru wale wote waliosaidia kufanikiwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao na amezidi kutoa wito kwa wannchi kuendelea kutoa taariufa Polisi wanapobaini nyendo za watu wabaya ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.
Amesema kuwa mara nyingi watu kama hao wakiwemo wa kutoka nchi jirani wamekuwa wakishirikiana na Watanzania wachache kwa kufanya vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha ukiwemo wa utekaji wa magari na kupora mali za abiria.
Haya sasa mnaona mambo hayo,wananchi wa jirani wanakuja kutuzidishia umasikini.Ujambazi huu tena kwa silaha na sijui wameshatoa roho ngapi mpaka sasa.Hawa ndio wenye kuingia mabenki na mabomu maana watanzania hatuna sifa hiyo ya mabomu japokuwa tunao majambazi.
ReplyDeletehao waburundi ndio wanaoongoza ujambazi hapo nchini kwetu tunaomba jeshi la polisi liwafanyie kazi kisawasawa maana wameacha kazi zao za kupigana vita wameona bora waje kutuulia ndugu zetu na mibunduki yao
ReplyDeletewamezoea kuuwana kama kuku wanakuja kutuletea ujambazi wao na kuuwa ndugu zetu pambafff tunaomba wizara husika wafatilie kwa karibu sana uhamiaji wa hao warundi maana hatutaki balaa nchini kwetu tumezoea amani.
MIMI SIJAKUBALIANA NA WATOA MAONI WAWILI WALIONITANGULIA HAPO.
ReplyDelete1. MAJAMBAZI WAHUSIKA NI WANNE. WAWILI KUTOKA TZ NA WAWILI KUTOKA BURUNDI.
2. KIGOMA NI MKOA WA MPAKANI, HIVYO NI KAWAIDA MIKOA YA AINA HIYO KUWA NA WATU KUTOKA SEHEMU ZOTE MBILI ZA MPAKA.
3. SASA KUWASEMA WARUNDI NA KUWATUSI/KUWADHIHAKI PIA SIO UTARATIBU NA UTAMADUNI WA WATANZANIA; KWANI MISINGI YETU INAHITAJI TUWE NAKINI, TUTHAMINI UTU WA BINADAMU WENGINE NA PIA HATUNA MISINGI YA UBAGUZI.
LA MSINGI NI KWAMBA UJAMBAZI SIO JAMBO JEMA NA TULIEPUKE KWA NGUVU ZOTE; wala sio kunyoosha kidole dhidi ya jamii fulani ya watu ilhali vilivyosalia vinatuelekea
WARUNDI WENGI NI MAJAMBAZI MSIWATETEE. ISIPOKUWA WATANZANIA NAO WANAHUSISHWA KATIKA UJAMBAZI HUO KWA VILE UNAINGIZA PESA ZA MKATO PASIPOKUTOKA JASHO. HATA WATANI ZETU WAMESHIRIKI SANA UJAMBAZI HAPA NCHINI WAKISHIRIKIANA NA JAMAA ZETU. JAMBO LA MSINGI NI KWA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI PALE WANAPOONA KUNA WATU WASIOELEWEKA.
ReplyDelete