Wazo Ngosingosi ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu kulia) mara baada ya kuwa mtu wapili kumaliza shindano la kula chakula kilo moja ya wali,wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, za kimkoa zilizofanyika Julai saba mwaka huu eno la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga.
Washiriki wa Mashindano ya kula Wali kilo moja kwa muda wakipata maelezo kabla ya mashindano kuanza.
Maongezi ya hapa na pale.
Kipunga kikiwa tayari tayari kwa ajili ya washiriki wa mashindano.
kazi imeanza hapa.
Mchezo wa mashindano ya kula , ulibuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ' Tanganyika' ambapo aliweza kununua mchele wa kutosha na kwa upende wa kitoweo cha nyama ya kuku , kuku walinunuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu.
Washiriki 14 walijitokeza kati ya hao wanawake walikuwa ni wanne , na ulifanyika siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya kimkoa Julai saba, mwaka huu eneo la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga na kuhudhiriwa na mamia ya wakati wa eneo hilo pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa .
Mshindi wa kwanza, Sudi Kilamilo alipatiwa sh: 35,000 na ngao , mshindi wa pili Wazo Ngosingosi , alizawadiwa sh: 25,000 na mshindi wa tatu , Omary Manjawa .Picha na John Nditi.


Rais aliomba viongozi wawe wabunifu naona hawa wa Morogoro wameanza kuonyesha njia kwa ubunifu wa kubuni shindano la kula sana wakati nchi ina shida ya njaa sehemu mbalimbali hadi serikali inapiga marufuku chakula kusafirishwa nje sikuelewa kuwa serikali inapiga marufuku ili wananchi washindane kula sana nchini badala ya kuuza nje.
ReplyDeleteduh njaa itatuumiza watanganyika
ReplyDeleteKWAKWELI HII MICHEZO MINGINE HAINA KICHWA WALA MGUU.LAKINI NAUHAKIKA WADAU ANGALAU WAMEWEZA KUSEVU MLO MMOJA.
ReplyDeletehivi hii ni akili kweli hivi hawakuona michezo mingine isipokuwa hii kudhalilisha kweli kosa mali pata akili
ReplyDeletehaya mashindano yameandaliwa na serikali au? hebu iwekeni hii habari kwa kiengereza tuirushe
ReplyDeleteSiamini kwamba viongozi wa serikali wameshindwa kuwa wabunifu kiasi hicho; inaonyesha ni jinsi gani tulivyo na viongozi wasio na akili ya kufikiria. Badala wabuni hata mchezo wa kuweka bahati nasibu ya kujishindia vitu vidogo vidogo; na hela inayopatikana kwa kuuza ticketi hata kwa shilingi mia wakaiweka kwenye maendelezo ya shule kama kununua madawati au kuboresha mazingira ya zahanati; wanabuni mchezo wa kula. APPALLING! Hatutaendelea kamwe; kama viongozi wanaotuongoza ndio hawa.
ReplyDeleteFrom top to bottom; tumekwisha Tanzania. Labda miujiza ya Mola itokee
Mashindano kama hayo yapo mengi tu dunia. Hiyo hapo ni shindano anayemaliza kula mwanzo. Wenzetu Ughaibuni wanashindana nani atakula "sosage" nyingi, wengine wanashindana kuifukuza "cheese" mshindi atayeipata na kuna zawadi ya pesa inatolewa. Michezo kama hiyo inawafanya watu wapoteze wakati vizuri badala ya kufanya ngono na kupata maambukizi ya ukimwi. Kula kwetu Zanzibar huwa tunafanya mashindano ya nani atayekula dodo nyingi.
ReplyDeleteDuh! Hilo bwabwa lanitia njaa. Ni chele la mbeya au sumbawanga? Tuambiane basi ubunifu wa aina la chele,Chele chelewa oyeee!!!!!
ReplyDeletewewe Anonymous wa Fri jul 08.09;03;00pm2011 unasema mashindano kama haya yapo mengi duniani lakini sio tz ambayo inashida lukuki wangebuni yenye akili zaidi na inayojenga akili kuliko hii
ReplyDeleteMimi sielewi kosa la mashindano hayo ni nini? Watu wameshindanishwa kunywa bia itakuwa kula? au ndio lazima watu wafanye critism? Hio habari ya chakula kuzuiliwa kaulize Wizara ya Kilimo; Waziri Mkuu alishaagiza na Rais pia kwamba watu wakiamua kuuza mazao nje ya nchi RUKSA!
ReplyDeletesafi sana..good entertainment
ReplyDeleteBadala ya kufanya mashindano ambayo yataimarisha afya za Watanzania kwa muda mrefu, unafanya mashindano ya kuwa-motivate watu wale sana. Kazi kweli kweli.
ReplyDelete