![]() |
| Mh. Sugu |
Jana tarehe 8 Julai 2011 Polisi walinikamata kwa kile walichokiita kuwa ni kufanya mkutano bila kibali.Hata hivyo, mtiririko wa matukio unaonyesha kwamba polisi walisukumwa na sababu nyingine kwa kuwa suala la taarifa kupelekwa polisi kama sheria zinavyohitaji lilishashughulikiwa na viongozi wa CHADEMA mkoa na wilaya ya Mbeya Mjini.
Leo tarehe 9 Julai 2011 pamoja na kutolewa kwa dhamana polisi wameonyesha nia ya kutaka kuzuia tamasha la wazi la bure ( ‘Burudani Nyumbani’) ambalo wasanii mbalimbali walikuwa walifanye kwa mwito wangu kwa ajili ya kutoa burudani na kuhamasisha maendeleo. Polisi wameonyesha vitendo vya kutaka leo kufanyike tamasha la fiesta pekee wakati ambapo matamasha haya yote mawili yameandaliwa na wadau tofauti katika maeneo tofauti.
Mpaka wakati huu ninapotoa taarifa hii wananchi wengi wamejikusanya katika uwanja wa Ruanda Nzovwe ambao ni maarufu kama Uwanjawa Dr Slaa wakisubiri tamasha hilo lakini polisi wameonyesha dhamira ya kutaka kuwatawanya.
Leo tarehe 9 Julai 2011 pamoja na kutolewa kwa dhamana polisi wameonyesha nia ya kutaka kuzuia tamasha la wazi la bure ( ‘Burudani Nyumbani’) ambalo wasanii mbalimbali walikuwa walifanye kwa mwito wangu kwa ajili ya kutoa burudani na kuhamasisha maendeleo. Polisi wameonyesha vitendo vya kutaka leo kufanyike tamasha la fiesta pekee wakati ambapo matamasha haya yote mawili yameandaliwa na wadau tofauti katika maeneo tofauti.
Mpaka wakati huu ninapotoa taarifa hii wananchi wengi wamejikusanya katika uwanja wa Ruanda Nzovwe ambao ni maarufu kama Uwanja
Maneno na vitendo vya Jeshi la Polisi vinaelekea kuwa na uhusiano na kauli ambayo niliitoa hivi karibuni kupitia mtandao wa Facebook ya kutohitaji tamasha la Fiesta kufanyika Mbeya.Katika mazingira haya ni muhimu nikaeleza tu kuwa kauli yangu kuhusu Fiesta ilikuwa na madhumuni ya kuanzisha mjadala kuhusiana na suala zima la wizi na unyonyaji uliopo kwenye Sanaa, ambao sio tu unawanyima haki Wasanii, bali pia kukosesha mapato kwa Serikali ambayo yangetokana na kodi kupitia Sanaa ikiwemo muziki.
Nilifanya hivyo baada ya tamashahilo kutangazwa kufanyika katika eneo ambalo wananchi wamenipa wajibu wa uongozi wa kuwatumikia na kuwawakilisha.
Nilifanya hivyo baada ya tamasha
Hivyo kwa niaba ya wananchi wa Mbeya Mjini wanaokosa mapato katika sanaa na wasanii wa Mbeya wanaokosa fursa kutokana na vikwazo nilichukua uamuzi wa kuwakilisha kupaza sauti kama ambavyo nimekuwa nikipaza sauti katika masuala mengine yanayogusa umma kama viwanda, kilimo, barabara za Mbeya Mjini na Haki za wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na makundi mengine katika jamii.
Niliamua kupaza sauti katika hili kupitia Fiesta, kwa kuwa waandaji wake kimsingi ni sehemu ya vyanzo vya maovu kwenye maendeleo ya muziki hapa nchini. Fiesta ikiwa kitovu cha uonezi kwani hata Wasanii wanaoshiriki halipwi ipasavyo au hawalipwi kabisa. Na hii ni kutokana na wao kutumia njia haramu kuhodhi (monopolise)biashara ya muziki hapa nchini, huku wakiwanyima nafasi watanzania wengi kutumia vipaji na ubunifu wao kwenye biashara ya muziki.Waandaji wa Fiesta ndio wenye redio ya Clouds, Kampuni ya promotion ya Primetime, na pia wanahusika na N.G.O ya THT, waandaji wa matamasha ya injili, ikiwemo kuwa na ushirika katika Tamasha la Pasaka.Huku wakiwa na ushawishi wa hila kwenye Kili Music Awards (One Call Promotion) na mambo mengine yote muhimu yanayohusu Sanaa. Ikiwemo ujumbe wa bodi kwenye Tamasha la majahazi,Zanzibar . Lisingekuwa jambo baya kama wangetumia nafasi hizo kwa haki na maendeleo ya sanaa.
Kutokana na haya, kwa miaka mingi himaya (“empire”) hii imetumia nafasi yake dhalimu kukandamiza watu wengine hasa Wasanii. Kwa mfano kama Msanii hayupo kwenye hiyo “himaya”yao basi hana nafasi ya kutimiza ndoto yake. Na iwapo Msanii hakubaliani na taratibu zao au malipo finyu wanayowalipa Wasanii, basi watahakikisha wanampiga vita na hatimaye kuhujumu usanii wake ili atoweke, kwa kuwa tu hakubaliani nao. Msanii hana haki ya kufanya majadiliano ya kibiashara mbele yao . “Empire” hii imehodhi mpaka makampuni ya udhamini hapa nchini, ambapo makampuni haya yamekuwa magumu kutoa udhamini kwa wadau wengine kwa kuwa tu wao ni washirika wa “Empire” hii.
Walifikia hatua ya kuhodhi mpaka biashara ya usambazaji kwa “Wadosi” ambapo bila ya wao kuruhusu basi Msanii yeyote kazi yake haipewi nafasi ya kusambazwa wala kusikika. Hata kama nyimbo au album yake ni nzuri kwa kiasi gani.Kibaya zaidi wamehodhi mpaka nia njema ya Rais Kikwete katika kusaidia Sanaa na Wasanii. Mfano ni Studio ambayo Rais kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii waTanzania , lakini baadaye tukashangaa kusikia ipo mkononi! Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini yao na ndio makao ya THT! Wamefanikiwa kumhadaa Rais kuwa wao ndio “Care takers” wa Sanaa ya Tanzania akawaamini na wao wanaitumia vibaya imani njema ya Rais kwao kufanya dhuluma.
Yote niliyoyataja juu, japokuwa hayo ni kwa uchache tu! Yanalalamikiwasana na wasanii wengi na wadau hapa nchini, japokuwa wengi wameshindwa kujitokeza waziwazi kutoka na vitisho vya watu hawa. Vitendo hivyo wanavyofanya vimeleta madhara katika tasnia ya sanaa na matokeo yake ni kudumaa kwa maendeleo ya muziki hapa nchini. Vijana wengi wanaojihusisha na sanaa wamepoteza matumaini. Wengi walipata tegemeo la ajira kupitia muziki, lakini hali haipo hivyo tena. Vijana wengi wasanii wamekata tamaa kwa ajili ya ukandamizaji wa “empire” hii.
Na sio tu wasanii na wadau wengine wanawapoteza katika hili. Kwa watu hawa kuhodhi na kuvuruga kabisa biashara ya muziki, hata Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kodi. Kwa mujibu wa utafitiwa Dr. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa UDSM, hata katika hali hii mbaya ya biashara ya muziki, Serikali imepoteza Tsh. Milioni 18, kwa kutokusanya kodi kupitia muziki tu, ukiachilia mbali filamu na sanaa nyingine. Na iwapo hali itaboreshwa basi kodi hiyo itapanda mpaka wastani wa Tshs. Bilioni 50 kwa mwaka! Hizi sio pesa kidogo kwaserikali, hasa ukizingatia bajeti ya Wizara inayohusika na Utamadnuni ni Tsh bilioni 14, kwa mwaka, fedha ambazo mara nyingi hawapewi zote kutokana na Serikali kutokuwa na fedha ya kutosha! Lakini hapa utaona kukwa kodi ya mwaka peke yake ingetosha kwa bajeti ya Wizara na ziada kubwa ingebaki kwa miradi ya maendeleo kama kujenga Art Theatres n.k
Napenda ieleweke wazi kwamba mimi binafsi ni “Mhanga” au “victim” wa uharamia wa “himaya” hii kwa miaka mingi, tukupitia migogoro kadhaa ya kibiashara lakini kilichonisikuma kuchukua hatua hii; sio nafsi yangu pekee bali wajibu nilionao hivi sasa kama mwakilishi umma.Izingatiwe kuwa baada ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge na wananchi wa Mbeya tena kwa kishindo, Serikali kupitia Wizara inayohusika na utamaduni na pia Baraza la Sanaa (BASATA), walinipongeza kwa barua huku wakinitaka niendelee na harakati za kupigania sanaa na wasanii kwa kutumia nafsi au jukwaa langu jipya Bungeni na nje ya Bunge. Jukumu ambalo nililikubali kwa mikono miwili kwani harakati za muziki huu si kitu kipya kwangu, ulianza kabla ya Ubunge na ndio ninachokifanya na hasa ukizingatia mimi pia sasa ni Waziri Kivuli (Shadow Minister) wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Kwa lugha nyingine ujumbe nilioutoa wa kukataa Fiesta ni ishara ya mgomo wenye nia ya kutuma ujumbe wa madai ya msingi. Na historia inaonyesha kuwa, Wasanii wa Nigeria walianza kulipwa vizuri kama wanavyolipwa sasa baada ya kuanzisha migomo dhidi ya mapromota wanyonyaji wa nchini kwao.Na kama ni suala la kukuza uchumi na ajira, Ni nini mchango wa Fiesta na matamasha mengine kwa halmashauri za mji na majiji wanayopita na kuvuna mamilioni ya fedha kila siku?
Wenu katika kutaka haki,
Joseph Mbilinyi (Mb)
9/7/2011-Mbeya Mjini
Niliamua kupaza sauti katika hili kupitia Fiesta, kwa kuwa waandaji wake kimsingi ni sehemu ya vyanzo vya maovu kwenye maendeleo ya muziki hapa nchini. Fiesta ikiwa kitovu cha uonezi kwani hata Wasanii wanaoshiriki halipwi ipasavyo au hawalipwi kabisa. Na hii ni kutokana na wao kutumia njia haramu kuhodhi (monopolise)biashara ya muziki hapa nchini, huku wakiwanyima nafasi watanzania wengi kutumia vipaji na ubunifu wao kwenye biashara ya muziki.Waandaji wa Fiesta ndio wenye redio ya Clouds, Kampuni ya promotion ya Primetime, na pia wanahusika na N.G.O ya THT, waandaji wa matamasha ya injili, ikiwemo kuwa na ushirika katika Tamasha la Pasaka.Huku wakiwa na ushawishi wa hila kwenye Kili Music Awards (One Call Promotion) na mambo mengine yote muhimu yanayohusu Sanaa. Ikiwemo ujumbe wa bodi kwenye Tamasha la majahazi,
Kutokana na haya, kwa miaka mingi himaya (“empire”) hii imetumia nafasi yake dhalimu kukandamiza watu wengine hasa Wasanii. Kwa mfano kama Msanii hayupo kwenye hiyo “himaya”
Walifikia hatua ya kuhodhi mpaka biashara ya usambazaji kwa “Wadosi” ambapo bila ya wao kuruhusu basi Msanii yeyote kazi yake haipewi nafasi ya kusambazwa wala kusikika. Hata kama nyimbo au album yake ni nzuri kwa kiasi gani.Kibaya zaidi wamehodhi mpaka nia njema ya Rais Kikwete katika kusaidia Sanaa na Wasanii. Mfano ni Studio ambayo Rais kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii wa
Yote niliyoyataja juu, japokuwa hayo ni kwa uchache tu! Yanalalamikiwa
Na sio tu wasanii na wadau wengine wanawapoteza katika hili. Kwa watu hawa kuhodhi na kuvuruga kabisa biashara ya muziki, hata Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kodi. Kwa mujibu wa utafiti
Napenda ieleweke wazi kwamba mimi binafsi ni “Mhanga” au “victim” wa uharamia wa “himaya” hii kwa miaka mingi, tukupitia migogoro kadhaa ya kibiashara lakini kilichonisikuma kuchukua hatua hii; sio nafsi yangu pekee bali wajibu nilionao hivi sasa kama mwakilishi umma.Izingatiwe kuwa baada ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge na wananchi wa Mbeya tena kwa kishindo, Serikali kupitia Wizara inayohusika na utamaduni na pia Baraza la Sanaa (BASATA), walinipongeza kwa barua huku wakinitaka niendelee na harakati za kupigania sanaa na wasanii kwa kutumia nafsi au jukwaa langu jipya Bungeni na nje ya Bunge. Jukumu ambalo nililikubali kwa mikono miwili kwani harakati za muziki huu si kitu kipya kwangu, ulianza kabla ya Ubunge na ndio ninachokifanya na hasa ukizingatia mimi pia sasa ni Waziri Kivuli (Shadow Minister) wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Kwa lugha nyingine ujumbe nilioutoa wa kukataa Fiesta ni ishara ya mgomo wenye nia ya kutuma ujumbe wa madai ya msingi. Na historia inaonyesha kuwa, Wasanii wa Nigeria walianza kulipwa vizuri kama wanavyolipwa sasa baada ya kuanzisha migomo dhidi ya mapromota wanyonyaji wa nchini kwao.Na kama ni suala la kukuza uchumi na ajira, Ni nini mchango wa Fiesta na matamasha mengine kwa halmashauri za mji na majiji wanayopita na kuvuna mamilioni ya fedha kila siku?
Wenu katika kutaka haki,
Joseph Mbilinyi (Mb)
9/7/2011-Mbeya Mjini



MICHUZI unaweka habari za SUGU mtandaoni.halafu tukiweka comment zetu, hauzitoi Dahhh inasikitisha sana!
ReplyDeleteDa afadhali umenifungua macho. Komaa nao tuu. Hii ndio faida ya watu kujua wanachokitaka
ReplyDeleteHongera sana Sugu,wengi watakuelewa hata kama sii leo basi huko mbele watakuelewa,Wazamini nao wanakuwa ni tatizo kubwa sana kwa sasa,nao ni watu wanaofanya uharibifu mkubwa sana kwa jamii ya sanaa na wasanii.
ReplyDeleteWewe na Kitime ninawakubali na tupo nyuma yenu.
Phew! That's all I can say for now. Nitarudi tena humu baadae. But clearly and in essence, Joseph Mbilinyi amejenga hoja nzito na nzuri sana (IMHO).
ReplyDeleteWell done... Kaza buti mzee, Tanzania yetu ndivyo ilivyo hivyo - only the fittest of the fittest shall survive!
Dennis B.
Buckinghamshire
hoja alizotoa sugu ni nzuri na nzito. tatizo ni moja:- sugu amekua ktk uadui wa muda mrefu na clouds. amekosea kuanda tamasha tarehe moja na mji mmoja ktk muda unaolingana. kama mwanasiasa angeelewa kuwa lazima polisi watasema wanahofia uvunjifu wa amani kwa kuwa tamasha la sugu limeandaliwa ktk misingi ya bifu.
ReplyDeleteUSHAURI KWA SUGU NA WADAU WENGINE
bila shaka clouds (prime time) wanashikilia ufalme wa muziki hapa nchini. wanaweza kumbeba msanii au kumuangamiza msanii akatoweka ktk tasnia ya muziki. lazima msanii awanyenyekee ili wambebe.
sugu lazima ahamasishe baadhi ya wasanii kusimama hima ktk kutetea haki zao zinazonyonywa na clouds. ASILIFANYE KISIASA. yeye ni msanii. ana ukaribu na wasanii wengi. ahamasishe kisanii. nimependa alivyoonesha heshima kwa rais ktk makala yake! amekosea kutaja vile viwanja kwa jina la dr slaa. hapo anaingiza siasa. ili afanikiwe katika HII VITA ya ukiritimba wa clouds (ambao mimi naulani), ashughulikie hili suala kijamii zaidi kuliko kisiasa.
MUNGU AKUBARIKI BW SUGU KTK JITIHADA ZAKO ZA KUWATETEA WANYONGE
Maisha ni mapambano. Ni vita kati ya MUNGU na shetani. MWANGA na giza. UKWELI na uongo. Hii ipo sana tu..hata huko mbele. Hebu sikilizeni wimbo wa Michael Jackson "tabloid junkie" na "they dont real care about us" cha msingi SUNGU unapaswa kuwa upande wa MUNGU kwani Hashindwi kamwe. Pia ujue ni nini asili ya muziki.
ReplyDeleteSugu, pole sana kwa yaliyokusibu, yanayokusibu, na yatakayoendelea kukusibu katika harakati zako za kutetea haki na ukweli. Ni bahati kwa Tanzania kuwa na mtu mwenye ustahimilivu na makusudi ya dhati kama wewe, na umechagua sekta ambayo haijapata mtetezi wa kweli kwa muda mrefu. Mungu akutangulie katika yote uyafanyayo kuwatetea Watanzania, maana wamefinywa kila kona ya uhai wao. Kumbe hao jamaa ndivyo walivyo??! Mimi sikujua, ila nimefurahi kujua sasa. Kwa nini usianzishe umoja wa wasanii (maana naamini wapo wa ukweli na sio wakuyumbishwa yumbishwa) na kwa pamoja, chini ya uongozi wako, muwe na sauti kubwa zaidi? Naamini unaweza kabisa kubadilisha mambo kwa kuwashirikisha maana kama mambo menyewe ndio hayo basi hata wengi wao itakuwa wamejeruhiwa sana kiuchumi na kihisia.
ReplyDeletehoja yako nimeikubali sana kaka ipo siku mambo yatakuwa sawa ktk sanaa. lazima tupinge ufisadi ktk sanaa.
ReplyDeleteWe ni kichwa mzee, hata hao Askari ipo siku watakuelewa tu. Pamoja sana mzee
ReplyDeleteMheshimiwa Mbunge,
ReplyDeleteKwanza nawasikitikia wasanii wa Tanzania kwa kunyonywa,
Lakini nawasikitikia sana kwa kutokujitambua.
Ndugu Wasanii, Wanaowapenda siyo hao wanaoitwa ''Himaya'' katika Statement ya Mh. Sugu, wanaowapenda ni WATANZANIA na mnashindwa kuitumia nafasi hiyo kudai haki.
Nawaambia kuwa, siku zenu na siku za vipaji vyenu zinahesabika na siku moja mtatamani ushabiki wa muziki wanu wa Bongo Fleva uliopo sasa urudi bila mafanikio, wakati huo WATANZANIA tutakuwa tunaimba nyimbo za ukombozi ambazo hata Kwaya za Kanisani na vikundi vya Kaswida katika Misikiti wanaweza kuziimba bila nyinyi.
Hao walioitwa Himaya na wasanii wanaoikumbatia himaya hiyo na wote wanaosambaza kazi zenu ni vibaraka wanaoutumikia utawala wa kifedhuli wakiogopa wasivyofanya hivyo watakula wapi, naomba niwaambie kuwa Demokrasia sio huduma ya Bure, DEMOKRASIA INALIPIWA.
Kwa wenye akili Mh. Sugu anachotafuta ni Demokrasia kwa ajili ya kuboresha kwanza hali yenu kimaisha kama wasanii na kisha Pato la Taifa.
Acheni kutumikishwa, wanaowatumikisha ni vibaraka wa watu waliotufikisha hapa tulipo, watu wasiotaka kufikiria kutafuta ufumbuzi wa maonyesho yenu kutumi Generator.
Nyinyi mnajidanganya kuwa mna vipaji, vipaji mnavyovifungia kiunoni na kwenye statrehe zisizowaruhusu kubakia na chenchi...siku moja tutawakimbia, tutaacha kununua, kusikiliza na kuangalia vyombo vyao na kuacha kwenda kwenye biashara zao.
Mh. Sugu,
Umetoa hoja, umeiandika vizuri sana, wasanii nyinyi ni vijana mna awajibu wa kuutekeleza. Hali ni mbaya.
Ahsante.
Well said Sugu.
ReplyDeleteNa wewe ungekubali kuendelea kuwa kibaraka wa Clouds Radio na Primetime Promotion, mpaka leo ungekuwa kwenye chati na vijisenti vya kufuta machozi a.k.a Jina kubwa mfukoni hakuna kitu!
Mimi naamini ukilitimba wa Clouds radio na Prime time Promotion ndio unaosababisha wasanii wengi kukubali kuendeshwa kama pia. Hii inapelekea wasanii hao kutengeneza sanaa imbayo si tu itaburudisha jamii bali pia kuenya, kuelimisha, kurekebisha, kuifariji.
Kwa mtazamo wangu, naamini ukilitimba wa clouds na Primetime promotion, ndio unaosaidia kupiga vita wasanii wenye hisia kali na kuitakia nchi umoja usawa na maendeleo ya kweli kwa kufichua maovu, kukandamizwa na kufichwa kabisa. Pia naamini kuwa Clouds wanaisaidia serikali kudidimiza wasanii wa kweli ili aibu ya serikali na maovu yake isianikwe hadharani.
Chakunishangaza mimi ni kwamba vyombo vingine vya habari kama Radio 1 na ITV mbona havijishughulishi kupambana na hali hii wakati wana mikili media kama clouds!?
Ili sanaa iweze kukuwa, itabidi kuwe na upinzani kwa clouds. Vyombo vingine vya habari inabidi navyo vijitose ktk kunyanyua wasanii ktk mfumo wa kushindana na clouds.
Alipoanzia Sugu ni pazuri sana. Sugu umeweka baraka sasa wadau wengine jitokezeni kunogesha mpambano.
Ni hayo tu,
Msanii wa kweli Asiyevuma.
very sad to have mbunge anayepigania burudani, jamani watanzania are we mad? kwanini walimpigia huyo mtu kura? halafu utakuta mtu analalamikia maendeleo.. tutaendelea vp kwa kuwa na mtu kama huyo bungeni? sidhani hata kama huwa anaoga kila siku.. phewwwwww
ReplyDeletenkamu muheshimiwa mbunge sugu ujobile kanunu nkamu jope bandu wa bikuti fijo ba clauds? ba kali kanunu jope tupo pamoja nu kyala akutule nkamu baleke hao, kuti fiki nkamu bali balosi hao. nimeongea kikwetu kuweka msisitizo kwani hao clouds ni nani? ndomaana watanzania hatuendelei mara clouds clouds ushuzi mtupi haya sasa kaka mchuzi usibanie hii we tuma tu mkuu kwani tatizo nini? hasara roho bwana..
ReplyDeleteDr. US Blogger)
ReplyDeletePole sana mzee sugu, huo ndio uwanaume. hao polisi wamekuonea, anayestahili kuka kukamatwa ni wale watu wa mjengoni, na mafisadi yanayopeta mitaani pamoja na NABII feki Nabii Yohana Mashaka. Mashaka amefanikiwa sana, na amejenga ufuasi wa kutisha kwa kuwa mstari wa mbele kuwafanya wachina waonekane kama wanyama ambao wanataka tu kupora nchi yetu.Siku mashaka anaingia tanzania namfungulia mshtaka akamatwe kwa uchochezi dhidi ya WACHINA. Wachina ni watu wazuri sana, wanatusaidia katika kila nyanja. Bila wachina siku hizi tuisngekuwa na chakula cha kutosha. Ni wachina watatuwezesha kuvaa vizuri kwa bei rahisi sana
Mimi kama msomi aliyebobea kutoka chuo kikuu cha OXford cha Lodon, nimemuomba huyu nabii aje kwenye mjadala lakini wapi ananikimbia kama mtoto mdogo, kazi ni kutuma makombora makubwa ktuka uhamishoni.Anatetea mada zake kwamba hawa wageni watamaliza kila kitu, madini na mali asili.
Hivi huyu Mashaka kasomea uchumi wapi? Wao ndio walioaribu uchumi wa dunia, mbona hata siku moja sijamsiki amshaka akiwalaumu wamarekani? kazi ni kuponda wachina tu? Bila wachina tusingeweza kungalaia TV, wala tusingekuwa na mafriji za bei Raisi. Mashaka leta oja nyingine la wachina umeshinda
Bado nakusubiri tukutane kwenye televisheni ya taifa TBC ili nionyeshe kwamba wewe ni fraud tena ni mtu ambaye hayupo. Wewe ni ni jini tu Michuzi ametengeneza ili blogu yake izidi kupata umaarufu. Kwa maana ni wewe tu ukiandika watu wanatiririka kama utitiri kuchangia. Wewe kama mwanamke, njoo basi kwenye mjadala. Nitakulipa na wafanya kazi wako wote.... naongeza dau hadi $3million ili ushirki kwenye mjadala.
Mimi ndio mchumi bora zaidi hapa Tanzania, nimeshauri nchi nyingi sana, angalia uchumi wa Zimbabwe unarudi kwa sababu yangu. Mshaara wangu kwa mwaka ni $5million kwa hiyo hela siyo shida kwangu. Usiogope nirtakulipa pamoja na tiketi yako. Najua hauwezi kujinunulia tiketi kwenda Tanzania
Dr. US Blogger
Alumni Oxford University
Economics Department
ww Anonymous wa sun jul 10 12:58.. unajuwa nchi za wenzetu entertaiment inachaingia pato kubwa kwa taifa. acha unafiki.. kwanza sana itapunguza wizi na vitendo viovu mtaani kwa kutoa ajira kwa vijana.. ucwe mshabiki wa kijinga watch out! Sugu ww ndio mpiganaji mbuge ambaye upo bungeni unaye weza kuwapigania vijana ktk nyanja ya sanaa.. acha hao wengine wapiganie kilimo kwanza ww komaa na sana! bigup sugu!
ReplyDeleteUnathubutu kusema ukweli halisi na unawatetea bila kujali itikadi zao,unatoa mwanga wa ukweli kwa matatizo yao...historia ya sanaa imepata mtu mweli na mpambanaji,vita uliyoianza kuna siku itaisha huku upande wako ukiwa ni mshindi..hongera sana.Nimeona onyesho lenu la bure jinsi lilivyojaa ,na kama kunasehemu ambayo fiesta wamepata idadi ndogo nadhani ni Mbeya,Hongera sana Sugu.
ReplyDeletehahhaha jamani bifu ya ZUNDUKA bado inamnyima usingizi SUGU wetu maana aligharimia kweli matokeo yake haikuifanya kisheria toka mapema wenzie wakamzidi nguvu. Usijali Sugu ndo maana Mungu akakupa ubunge kilaini ili urudishe vile visenti ulivyopoteza (ila kero hao waliokataa posho nadhani wanakuudhu sana maana wamewaonea sana NJUKA nyie msifaidi kama wao) lakini sugu rafiki yangu toka MBY hadi DAR nakushauri acha bifu upo juu sasa anzisha tamasha lako tupo pamoja nawe acha kufanya vitu kwa papara na kuandika kwenye FB nk. Kaa chini kumbuka papara bila ushauri ndio zilikufanya kete yako ya ZINDUKA ikapokonywa. tulia mzee.
ReplyDeleteNdani ya Tanzania kuna vibaraka wengi sana, tena wanaotumikia watu au kundi la watu katika upumbavu wa hali ya juu, yaani Mh, Mbunge anazungumzia tatizo la Sanaa ambalo ni sugu kwa miaka mingi wewe unasema haogi!!!
ReplyDeleteMara nyingi mtu anayejua kuhusu watu kuoga kila siku au kutokuoga huwa ana historia ya jambo hilo yeye mwenyewe na uzoefu wa kulitekeleza, unapoandika kitu kinachoweza kusomwa na watu wengi uwe muangalifu kwa sababu wanao read between the lines wanaweza kukutambua ulivyo na kukuona mpumbavu.
Nchi hii inahitaji fikra mpya sio fikra za mfano wako ambazo kama ungeziwakilisha vizuri Serekali ingeweza kufikiria mfumo mzuri wa upatikanaji maji safi na salama na hata sio vijijini tu!!!! hata katika Jimbo la Ubungo lililopo katika Makao Makuu ya Tanzania.
Hizo husda tu kwa watanzania wenzie, we sugu nani asiyekujua kua ni mtu wa visa,ni mwaka jana ktk uzinduzi wa malari ambassador umeleteana visa na wasanii wenzio kisa we umeachwa na hukwenda kuonana na raisi.
ReplyDeleteAcha roho mbaya, kwani THT wakipata si ni watanzania? kwa akili yako kqweli unaona kastudio kamoja kanaweza tosheleza watz wote???????
tumia akili we kijana,huu si wakati wa visa na malalmiko ni kutenda,we ni mbunge unao uwezo hata wewe wa kutoka nje ya nchi ukatafuta fursa mbalimbali kwa ajili ya wasanii na watanzania kwa ujumla sio kung'ang'ania haka ka keki kadogo tu kutwaaaaaaaaa
pole sana bwanaaaaa.lakini naona kama hujielewi elewi vile nini jukumu lako kama kiongozi,nakushauri utulie na ujue wewe ni kiongozi.
Joseph Mbilinyi huo ni ubinafsi tena mbaya sana tafuta mbinu za kuhamasisha shughuli yako sio kupanga siku moja na wenzio acha hizo wewe
ReplyDelete"Kwa akili yako kweli unaona kastudio kamoja kanaweza tosheleza watz wote?" Hilo swali muulize aliyetoa studio na sio Sugu.
ReplyDeleteUkiritimba wa Clouds umefanya hata baadhi ya wasanii kuishia kutunga nyimbo za ajabu ajabu coz wanajua Clouds watazirusha. Wimbo kama bongo fleva naipenda! What a shit???
mmh sugu usha prove failure ...nikisoma mada yako naona imejaa chuki na hasira ..utaandaaje tamasha lako siku moja na sehemu moja kama wenzako?? na kuandika facebok pumba tupu ......njia uliyotumia si sahihi ndio mana umewekwa ndani...jipange...tatizo la wabunge wa upinzani wanakurupuka !!fanyeni mambo ya msingi ...hospital,barabara ,maji na huduma mbovu kila sehemu jimboni kwako unatuletea habari za prime time hapa??!! acha wivu wa kizamani wewe
ReplyDeleteMSAADA TUTANI..KUNA HUYU MTANZANIA NI MWIZI KWA KUTUMIA INTERNET
ReplyDeleteKAKA MICHUZI NIWEKEE HII JUU TAFADHALI.
Ndugu zanguni hasa wale wanaoishi nje ya nchi, kuna kijana mmoja MTANZANIA ni tapeli wa kimataifa anamajina zaidi ya 5 kwenye facebook,namba za simu zaidi ya 3 na moja inaishia 8888 ambayo ikiipiga haipatikani.
Anambinu nyingi sana anayotumia moja wapo anasema anasafirisha komputer kwenda Tanzania tena anakupa bei ndogo ili ukubali, atakupa jina la mtu umtumie kumbe ni yeye mwenyewe, ukifika wakati unahitaji hizo komputer sasa utakoma uwongo wake mara secretary katoka, atakuweka kwenye simu kujifanya anaongea kumbe wapi yaani anaupuuzi mwingi sana.
Alafu anajifanya ni padri, au atakuambia ndugu yake padri, mara yeye ni mtoto wa balozi, mara mama anafanya banki kuu, yaani vyeo vingi mradi umwamini kumbe wapi.
Sasa nawaomba watanzania wenzangu huyu mtu tumuweke wazi kwa picha, namba zake za simu, na majina ili watu wasiendelee kulizwa?
Kama ulishakumbana na kishanga kama hiki tuwasiliane, tayari tupo watu zaidi wa 5 tuliotapeliwa na huyu mtu bwana mkubwa.