Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akisikiliza jambo kwa makini toka kwa Diwani wa kata ya Mzimuni, Mohammed Chambuso (kushoto) wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima na waishio kwenye Mazingira hatarishi cha Umra jana. Kulia ni Katibu wa Kituo hicho,Yusuf ahmed.
Mtoto Hasab Yusuf Mwenda (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya shule na chakula kwa mtoto yatima Abdillah Amri anayelelewa kwenye kituo cha kulea watoto yatima na waishio kwenye mazingira hatarishi cha Umra kilichopo Mzimuni, wakati Meya huyo alipotembelea kituo hicho Dar es Salaam jana. Meya huyo (kushoto) aliambatana na familia yake kwa ajili ya kujumuika na kula pamoja na watoto hao. Wa pili kulia ni Katibu wa kituo hicho, Yusuf Ahmed.
Mtoto Hasab Yusuf Mwenda akigawa keki kwa watoto yatima waishio kwenye kituo cha kulea watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu cha Umra, Mzimuni, Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...