Kwa wale waiokuwa wakibisha kuwa Mrisho Ngassa hakucheza kwenye mechi ya leo dhidi ya Man Utd,basi hivi ndivyo ilivyokuwa wakati kijana wetu huyo akichuana vikali na mchezaji Fabio wa Man Utd.Bado mnabisha??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2011

    Lakini wamepigwa saba nunge!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2011

    Acheni bwana hizi si picha zenu za kutengeneza!

    ReplyDelete
  3. Ankal ongezea na hii summary ya match inayoonesha Mrisho Ngasa aliingia uwanjani dakika ya 76 kama bado kuna wanaobisha;

    Scoring
    Sounders FC - None.
    Manchester United - Michael Owen (Patrice Evra, Ashley Young) 15; Mame Biram Diouf 49; Wayne Rooney (Nani 51); Wayne Rooney 69; Ji-Sung Park (Wayne Rooney) 71; Wayne Rooney (Gabriel Obertan) 72; Gabriel Obertan 88.

    Discipline
    Sounders FC - None.
    Manchester United - None.

    Lineups
    Sounders FC - Kasey Keller (Terry Boss 46), James Riley (David Estrada 73), Patrick Ianni (Taylor Graham 64), Jeff Parke (Michael Tetteh 64), Leo Gonzalez (Zach Scott 46), Mauro Rosales (Pat Noonan 46, Mrisho Ngassa 76), Osvaldo Alonso (Servando Carrasco 46), Erik Friberg (Brad Evans 46, Mike Seamon 64), Alvaro Fernandez (Lamar Neagle 46), Fredy Montero (Mike Fucito 46), Roger Levesque (Nate Jaqua 46, Miguel Montano 76).
    Manchester United - Anders Lindegaard (Ben Amos 46), Patrice Evra (Fabio Da Silva 56), Rio Ferdinand, Nemanja Vidic (Jonny Evans 56), Rafael Da Silva, Nani (Gabriel Obertan 56), Anderson, Ryan Giggs (Ji-Sung Park 46), Michael Owen (Mame Biram Diouf 46), Ashley Young (Michael Carrick 66), Federico Machida (Wayne Rooney 46).

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2011

    Mimi niliangalia mechi Live!. Aliingia kipindi cha pili dk ya 76, alivaa jezi #35, ingawa haikuwa na jina mgongoni, Mtangazaji alimtaja jina na kusema kuwa ni mchezaji wa majaribio kutoka Tanzania, alianza kucheza wingi ya kulia,lakini baadae akacheza mbele kushoto, alijitahidi kujituma na nusura afunge goli dk ya 90. Hata hivyo jamaa walikung'utwa goli saba bila majibu!!. Na kama angefunga goli lile basi pengine ndo lingekuwa goli la pekee kwa timu ya Seattle Sounders. Mdau USA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2011

    adobe photo 7 imetumika kuunganisha hawa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2011

    Tatizo letu ndio hilo, uchawi mwingi mtu kacheza ila watu wanakuwa wabishi. Ngasa jana kaingia kwa majaribio dakika 15 za mwisho na jezi namba 35 haikuwa na jina sababu hayupo kwenye kikosi kamili. Rio mwenyewe anajua ile mikiki miwili iliyotaka kusababisha goli na Kijana. Nashukuru watangazaji na wao walimsifia kwa kuonyesha alichonacho na nina UHAKIKA NGASA ANABAKI USA au atapata timu kubwa zaidi ya Hii. Mpira ulichezwa Saa kumi na moja Alfajiri kwa masaa ya Tanzania, wale wenzangu wa Comcast tuliicheki 555

    ReplyDelete
  7. Ngassa alicheza, aliingia dakika ya 76, na alionesha uhai mkubwa sana na aliweza kuwasumbua mabeki hasa Fredinand. Mnamo dakika ya 89 Ngassa aliwakosakosa goli moja matata, ilipelekea Fredinand kuumia mguu

    Niliiona mechi, na nimeirekodi kwa tathmini zaidi

    MAKULILO

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2011

    Hivi wewe Mrisho Ngasa mwanangu, kwani hawa jamaa umewatafunia wanawake zao? kwanini wanakuchukua sana?

    Nakumbuka ulipokwenda kwenye majaribio Uingereza watu hawahawa walikuwa wanaongea mambo haya haya. Kama namna gani vipi basi mwambie ankal michuzi asiwe anaweka habari zinazohusu mipango ya maendeleo yako.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2011

    Ngassa hakucheza alikuwa benchi tu. Hizo ni picha za kutengeneza msitudanganye!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2011

    Acheze asicheze si yupo huko USA.........!!!kashaandika jina!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2011

    Mtu anayebisha anitafute nimpatie DVD...Nimerecord mechi yote ..Pia separately nimerecord zile dk 15 za mwisho alizoingia Mrisho Ngasa....Ngasa aligusa mpira mara 5, katika hizo 5 alizogusa , alitoa passes 2 correct,1 miss pass, 1 short golini ambayo alim challenge Rio Ferdinad lakini bahati mpira ulipaa kidogo juu ya goli....Pia alifanya chasing mbili ambapo moja Fabio alimchezea Faul Ngasa na kusababisha Free kick in favour of Seattle na nyingine hakunasa mpira ,Rafael aka guard mprira ukatoka nje for free kick.


    Rodrick mwambene...
    Mdau

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2011

    Jamani eh hiyo picha imetoka kwenye yahoo....which means wamemkubali kwamba alicheza dkk 15 lakini alifanya vitu vinavyokubalika hapa http://news.yahoo.com/photos/seattle-sounders-fcs-mrisho-alfani-ngassa-left-tangles-photo-051524733.html

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2011

    Amna kazi watu wazima ooovyo kama amkuweza kuangalia wa sababu ya tanesko si muanze kumchawia kijana wa watu mbona sisi wabongo tunapenda majungu ya kijinga sana. mtasema yote amta change ukweli na kija huyu atafanikiwa one day.
    mdau paris

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 21, 2011

    Hili ndio tatizo la waswahili kujifanya wanajua kumbe hawajui jamma amecheza namimi nilikuwa kiwanjani naon hili boli tuache ujinga na fitina ukijumulisha moja na moja unapata mbili kwanini iwe tano ukweli jamma kacheza na man u hongera ngasa

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 22, 2011

    Game niliingalia live na ngasa alicheza jezi # 35, lakini hakufanya chochote huo ni ukweli tuache kudanganyana hapa. Alikosa bao dk za mwisho baada ya goal keeper wa MAN U kutoa pande kwa FERDINAND kwenye 18

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 22, 2011

    Mmmh wabongo! Silika yao haipotei kabisaaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 22, 2011

    Tatizo la watanzania tuna roho mbaya sana halafu hatupendani, huyo anayeng'ang'ania Ngasa hakucheka hata hela ya kula mfukoni hana, sababu ya roho mbaya yetu ndiyo maana mungu anatulani majanga kila siku hasa hili la umeme, hii ngozi bwana ndo maana hatuchoki kurogana! tuache ROHO MBAYA WATANZANIA, ROHO ZETU NYEUSI KAMA SHETANI. Sisi tuna roho mbaya sana, bora umfadhili mbuzi utamla mchuzi

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 22, 2011

    hata kama 7 nunge lakini si alicheza?

    ReplyDelete
  19. Ngasa alicheza dakika k15 za mwisho. Michuzi, kwa wale ambao bado wanabisha nimeweka video YouTube. Nime edit video na kuacha dakika 15 za mwisho Ngassa alivyoingia. Unaweza kuingalia hapa: http://www.youtube.com/watch?v=uZTQM8LO96o. Kama unataka kuona goli alilokosa, peleka video mbele mpaka dakika ya 11. Kama YouTube wataindoa, nitaiweka moja kwa moja bongoline.com/videos

    Thanks Subi for providing the video link.

    source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/07/video-mrisho-ngassa-vs-manchester-united.html#comments#ixzz1Ss5M5Idm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...