Hello kaka Michuzi,

Hebu wawekee wadau hizi picha za kijana wetu wa Tanzania,Mrisho Ngassa alipokua uwanjani na timu yake ya Seattle ilipokuwa ikikipiga na timu ya Man U, ingawaje zilikua zimebaki dk 15 za kumalizika kwa mchezo ila alileta uhai na makosa ya mabeki ya Man U karibia angeandika bao dk za mwisho,japo timu yake ilifungwa bao saba kwa bila...

Quality ya picha sio nzuri ila zinaonekana!

Mdau
Oceania
Ngassa akiwa uwanjani.
Ngassa akitoka mara baada ya mechi kumalizika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2011

    Full match report link hii ila sijaona jina la Ngassa, labla alikuwa substitute of substitutes. Yaani list ya tatu ukiacha wale wa uwanja, then substitutes then ndiyo Ngassa anakuwa kwenye list ingine.

    http://www.goal.com/en-us/match/63323/seattle-vs-man-utd/report

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2011

    Hao Goal wamekariri vikosi,
    kula list kamili hapa
    http://www.manchesterunitedmagazine.co.uk/seattle-sounders-0-manchester-united-7-wayne-rooney-scores-hat-trick/

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2011

    Wewe Ananoymous unaesema kwenye report hujaona jina la Ngasaa, jiulize ni wachezaji wote wanatajwa kwenye match report? Hizo picha hapo juu ni ushahidi alikuwepo na tuliongalia mechi hiyo live tulimuona..na kwa taarifa yako wale watangazaji walisema kabisa yupo kwenye trial. Sasa wewe ambaye hukuona unatoa kashfa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2011

    Ngassa hakuwa kwenye list ya substitutes yeye alipangiwa acheze mechi ile kama mchezaji mwalikwa kutokana kwamba yupo ktk majaribio na hata Man utd walifahamishwa hilo.dk 15 alizopewa alijitahidi kuonyesha ni mchezaji mzuri.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2011

    hamna lolote mnampa sifa za bure tu..alikuwa kama hayupo uwanjani bure ngali...........

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2011

    mbona hamjaweka picha za Nudir Khalfan vs Manchester City juzi? Nudir alicheza kwa kipindi kirefu zaidi ya Ngassa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...