Na Madaraka Nyerere, Butiama
Miezi michache iliyopita nilipokea barua pepe kutoka Bulgaria ikiniarifu kuwa kuna Mtanzania anaitwa Mohamed Sakara aliyedhaniwa amekufa lakini ilibainika kuwa yu hai na habari zake zikaandikwa kwenye gazeti moja la huko Bulgaria.
![]() |
Mohamed Sakara alivyo leo |
![]() |
Picha za hivi karibuni za Mohamed Sakara, akiwa jijini Sophia, nchini Bulgaria. |
Raia wa Bulgaria aliyesoma hizo habari aliniandikia barua pepe kuniomba nijaribu kuwatafuta ndugu zake Sakara huku Tanzania. Nilituma hizo taarifa kwa mwanablogu Muhidini Michuzi lakini sina hakika kama zilitoka kwenye blogu yake.
Kwa kifupi Sakara alienda nchini Bulgaria kwenye miaka ya 1980 kusomea uhandisi, lakini hali ilimuendea vibaya mpaka kujikuta hana uwezo kabisa wa fedha na akiishi kwa shida mitaani. Angependa kurudi Tanzania lakini hana uwezo wa kujilipia nauli. Inasemekana baada ya kutangazwa amekufa, ndugu zake hawakuendelea kumtafuta, lakini ukweli ni kuwa yuko hai. Taarifa zake nyingine ni:
- Amezaliwa mwaka 1961
- Inakisiwa alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1982 - 1984 halafu akaenda Bulgaria ambako alikuwepo mpaka kipindi napata taarifa hizi
- Anatoka kwenye familia ya watoto 8
- Taarifa za kaka yake Abeid Hassan Sakara ni: amezaliwa mwaka 1954; ameandika kitabu "Jizoeze Kiswahili", na "Rashid Mfaume Kawawa"; alikuwa mkuu wa kitengo cha uchapishaji cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Dar es Salaam); alikuwa akiishi Upanga Mashariki, Mtaa wa Maweni, Na.244, lakini hajulikani alipo kwa sasa.
habari, nafahamu baadhi ya ndugu zake, nawajulisha hapa,so watawasiliana nawe kwa njia ipi?
ReplyDeletepole sana bwana sakara, ila ni kweli kabisa wabongo kibao ni mahomeless nchi za watu, jamani majuu sio alimradi tuu lazima upambane haswa vinginevyo unakuwa homeless live haijalishi umesoma au hujasoma.
ReplyDeletewengine kutwa kupiga wenzao mizinga kila kukicha bora liende, ni hatari.
Mohammed Sakara mambo yameenda kombo, lakini hiyo hata bongo ingemkuta maana inaonyesha kuwa ni mtu "homeless". Cha kufanya sasa ndugu Mohammed ni utafute "immigration lawyer" akutetee ili upate uraia wa Bulgaria maana umeishi huko zaidi ya robo karne. 2012 Bulgaria inakuwa mwanachama kamili wa EU hivyo ukiwa na uraia wa Bulgaria mambo yako yatakuwa mazuri na utaweza kuja UK na kubeba boksi ili upate fedha kidogo za kuanza maisha hapo Bulgaria au hata UK. Kurudi bongo hafla sio vizuri.
ReplyDeleteJe ana undugu na Marehemu Fatuma Sakara aliyekuwa Diwani wa Upanga Mashariki?
ReplyDeletehilo ni jukumu la serikali au balozi zake kuregesha raiaa wake nyumbani.mdau hapo juu unaesema eti bulgaria aombe uraiaa huezi kumsaidia kitu maana huko njaa kali bulgaria.hungary,poland,latvia hizo nchi za eastern europa balaaa.wazawa wahuko wanakukimbia pia nakuzamia western europa
ReplyDeleteSio hatufutiwe nauli miaka yote aliyoishi Bulgalia sio mchezo jamani.Muhimu ni mawasiliano sio kumrudisha kwao HAKI YA BINADAMU Ulaya kuna watu wanaishi hivyo,sio kucheka au kulaumu ndio maana nchi zilizoendelea zinawasaidia raia wake.Hapo kwenye picha anakula fish and chips na bia je?akirudi TZ hataweza kula hivo?Hatujui alihamua vipi mpaka akaishi hivyo,chukulia barafu je?anaishije huyo?
ReplyDeleteKumrudisha huyo TZ ni sawa na matonya kumridisha Dodoma mwacheni aendelee na maisha ya watu wasiofikili cha kesho wao wanawaza kula na kunywa nampa hongera huyo jamaa kwa kuishi nchi hiyo kwa muda mrefu haaa
yeah,marehemu Fatuma Sakara ndo aliyekuwa mke wa huyo kaka yake Abeid Sakara
ReplyDeleteInasikitisha sana
ReplyDeleteIlikuwaje mwananchi huyu kufika katika hali hiyo ikiwa yasemekana kuwa ana elimu ya chuo kikuu DSM, sasa yeye ni kama mheshimiwa Matonya.
Mtu amshike mkono amuongoze kwenye ubalozi wa nchi, and they are duty bound to repatriate him back to Bongo
Inasikitisha kwa kweli ukizingatia alikuwa msomi wakati anaenda huko Bulgaria. Kisomo chake kingeweza kumsaidia. Lakini hii inaonyesha pia uhalisi wa maisha kwa nchi za wenzetu kama hizi ambako utaifa unapewa priority kwenye kazi. Utasoma na ma-degree yako lakini ikifika kwenye kuomba kazi hakuna anaekuangalia kwa vile wewe ni immigrant. Bila shaka state aliyo nayo imetokana na msongo wa mawazo na neglect ya muda mrefu. So sad, angebaki Tanzania, bila shaka ingekuwa quite a different and a promising story.
ReplyDeleteJamani msimkedhehi mwenzenu.We bwana nyerere ni mbulgaria gani amekuandikia? Mbona mnatafuta sifa kwa kutumia maafa ya wenzenu? Njia ya kupata habari kamili haswa kuhusu sakara ni kupitia blog au facebook group BULGARO.
ReplyDeletemdau KILI
kjmalisa@abv.bg
bulgaria
MIMI SISHANGAHI HATA INDIA WAPO WENGI WATAZANIA WANAFANYA KAZI YA UMATONYA. NA SEREKALI YETU INAJUA KUWA KUNA WATU KAMA HAO NA AWASAIDII.
ReplyDeleteWATANZANIA KWELI HATUJALI MTU ZAIDI NA YULE UNAYEMJUA
MDAU CHINA
Bulgaria kuna wanageria wengi tu na wanamaisha mazuri kwani wanasomesha kiingereza na kutafsiri magazeti kwa kiingereza. Ndugu yangu Mohammed inaonyesha anamatatizo ya kukata tamaa hivyo cha msingi ni kuwa apate kwanza matibabu ya maradhi yanaitwa "Depression". Maana yamemkumba kwa muda mrefu sasa.
ReplyDeleteWahusika msaidieni yaliyomtokea yametokea siku zote binadamu tunaanguka na kusimama tena kila la kheri mzee wetu Utapata msaada tu
ReplyDeleteI think as someone said above, this mwananchi has mental health problems and needs to be brought back home.
ReplyDeleteKazi mojawapo ya balozi wa Tz huko ni kumsaidia Mtz, hawezi ajiuzulu, maana wanajisahau inakuweje Mtz awe matonya kwenye nchi za watu na mabalozi wao wapo? Kila mtu huwa anakosea na Watzwengi wakifika nje hawana umoja na kama ni miaka hiyo ndo kabisa na tena wengi wanajifanya wanajua kila kitu. Wakati binadamu huwezi kujua kila kitu.
ReplyDeleteAnyway inaelekea yuko resedential home. But labda akipelekwa home atakuwa fine. But ni vyema kujua kwanza atafikia wapi na afya yake ikoje before maana nchi za wenzetu haki za binadamu zinazingatiwa kuliko Tz iliyopata uhuru MIAKA 50 ILIYOPITA. Mhhh inatisha. Pole kaka
MASIKI BAB WA WATU SIJUI NINI KILIMKUMBA MMUNGU AMPE FAHAMU AJITAMBUE AWE MTU KATI YA WATU NA KISOMO CHAKE ALAFU NI MTU MZIMA NASIKIA UCHUNGU SANA HADI MACHOZI YAMENITOKA
ReplyDeleteSIE KAMA WATANZANIA TUNA MSAIDIAJE HUYU MTU JAMANI? HASA WALE WANAO KAA BULGARIA MTU HUYU ANAONEKANA AMESHAATHIRKA KIAKILI KUTOKANA NA MAISHA
SIMLAUMU WALA KUMDHIHAKI KAMWE SITOFANYA KWANI BINAADAMU HATUWEZI KUJIJUA TUNAKO KWENDA WISH NINGEKUWA BULGARIA NINGEJARIBU VILE NAWEZA
TAFADHALINI SANA WATU MNAOKAA HUKO MUMSAIDIE KWANZA MZEE WETU KWA KILA MALI M MUNGU ATAWALIPA HAMUWEZI KUJUA NINI KILISABABISHA AKAWA HIVYO NCHI ZA WATU KUNA MENGI
MICHUZI TAFADHALI SANA FANYA CHANGAMOTO ZOZOTE TUMSAIDIE MZEE HUYU M MUNGU ATAKULIPA JAZA YAKO HUWEZI JUA MANGAPI AMEYAPITIA MZEE HUYU TAFADHALI SANA
YABINTY NALIA KWA SIMANZI
hapa nilipo ninona uchungu sana mpaka machozi yananitoka na simfaham huyu bwana. angekua ni mamerika yuko abroad na akajikuta kwenye hali aliyonayo serikali yake ingemrudisha nyimbani haraka sana. watanzania na ubalozi wa tanzania wamsaidie arudi nyumbani. hata kama ubalozo hauna pesa watanzania tulioko nje na popote kule tumchangie.
ReplyDeletePole sana kaka Sakara. Hata hapa Reading yupo mtanzania mwenzetu aitwaye Zinga, kwa wale wanaomfahamu hali yake ni mbaya zaidi kiasi kwamba hawezi kuomba kutafutiwa ndugu zake. Naamini Zinga akifanikiwa kurudi nyumbani Tanga atapatiwa ufumbuzi wa matatizo yake ya kiafya pia.
ReplyDeleteNamfahamu sakara .tulisoma nae bularia maisha yake yalikuwa ya anasa na alikuwa hakai hosteli alikuwa anakaa apartimenti ya kukodi na mama wa Kibulgaria. Huwa alikuwa akisafiri Sweeden na uingereza wakati wa likizo.mambo yake yalikuwa safi, lakini masomo yalikuwa yanamwendea kombo. watanzania wengi walirudishwa kwa msaada wa UN, yeye alikuwa wapi? mbona akina Sindeu Mchau, chesko , Dr. Omari wapo SOFIA je wanaishije hao? inaelekea huenda sakara ana Ugonjwa wa akili. Nakuomba ndugu michuzi Uwasiliane na wizara ya Elimu elimu ya juu( muone mama Kibaya) atasaidia Bwana sakarsa arudishwe Bongo kwa kushirikiana Na wizara ya elimu Bulgaria. pia Balozi wa tanzania Moscow ajulishwe( wasiliana na wizara ya mambo ya Nje).Kama Sakara amesalimu amri na kuamua kurudi Bongo msaidie hivyo. ni jukumu la serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa anarudi tanzania haraka sana.naomba Tangazo hili ziwekwe katika daily news na ikiwezekana uundwe mfuko au akaunti tumchangie ndugu yetu sakara. Bulgaria ni wanyanyasaji sana angalia jino moja wameshamng'oa inasikitisha sana. Pole sana sakara
ReplyDeleteNashukuru kwa aliyeweka taarifa hizi kwenye blog. Nilichelewa kuiona ila huyu Bwana nimesoma nae Azania. Alikuwa na akili sana kiasi cha kuwa mwanafunzi bora alipomaliza form IV akiwa na A nane. Pia alisoma A level Azania na licha ya kutokuwa na walimu kwa vipindi tofauti alifaulu sana akiwa daraja la kwanza la point 6. Baada ya JKT aliingia Chuo Kikuu kuchukua uhandisi ila akiwa mwaka wa pili kuingia wa tatu aliamua kwenda Bulgaria. Ukweli tulimshauri lakini hakushaurika. Yaliyotokea huko Bulgaria ni pamoja na kutokuhudhuria vipindi akiendekeza Starehe na Biashara. Yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo. Je kuna utaratibu wowote wa kumchangia ili arudi hapa nchini. Pia kwa tabia yake ninavyomfahamu inabidi akubali kwanza kwa vile ni mbishi sana kwa jambo analoliamini kuwa ni sahihi kwake.
ReplyDeleteNashukuru sana kwa habari hizi, huyu ni mjomba wangu.
ReplyDeleteWe have been trying to reach him for years. Please Please if you do have any updates with regards to where we might be able to find him, please let me know.
I have just come across this blog today, when I was doing my little research, and I am hoping it is not too late(2016).
I can be reached through iqbasetn@gmail.com or 9132020285 USA.