Mzinga huu umetokea usiku wa kuamkia leo kwenye barabara ya mandela road maeneo ya tabata AMI,ambapo chanzo cha ajali hiyo ni hilo lori hapo mbele ambalo lilikuwa likiingia kwenye barabara hiyo ya Mandela tayati kwa safari yake ya mikoani,lakini lori hilo halikuweza kuendelea na safari yake baada ya kuharibika katikati ya barabara na matokeo yake hali ikawa hivi kutokana na uzembe wa dereva na kondakta wake wa kutoweka ishara yeyote barabarani ya kuashiria kuharibika kwa gari hilo.
Hii ndio gari iliyoharibika sana kutokana na kuigonga hii pikup kwa kutokana na kwamba zilikuwa karibu karabu sana kwa kufuatana na ilikuwa katika mwendo wa kasi kidogo.
Pikup ikiwa imegonga lori hilo lililokuwa limesimama katikati ya barabara kutokana na kuharibika kwake.
hivi ndivyo hali ilivyokuwa.






Ghosssh! Huyo mwenye roli kwa nini hakuweka alama mapema hadi yakatokea haya? na huyu mwenye pick up kwanini hakuwasha hazard mapema hadi akasababisha mwenzie agonge?Huyo mtu wa tatu aliyegonga pick up naye ama alikua spidi au alikua amelewa,hapo itabidi alipie pickup na gari yake kwa mfuko wake au insurance yake kwa kutokua muangalifu,pia naye kama betri ni nzima kwanini hajaweka alama au hata kuwasha hazard?. But i hope hakukua na vifo maana ni hasara watu wakifa hawakujiandaa kiroho.
ReplyDelete