Meneja wa mawakala wa kampuni ya simu ya vodacom Maico Kasubi  (kulia) akifuatiwa na mratibu wa tamasha hili la waandishi Jamila Omari. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha (Taswa Arusha) Mussa Juma akifuatiwa na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini TBL  Wilderson Kitio wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Richi hotel jijini Arusha kuhusu kukamilika kwa  tamasha hilo waandishi wa habari.
Mwanamziki Ndanda Kosovo akiwa na waimbaji wake wakati wa mkutano na  waandishi wa habari ambapo wanatarajiwa kupamba tamasha lao linalofanyika jumapili hii ya Julai  24 katika viwanja vya General Tyre mkoani Arusha. 
Picha na habari na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha

Na Woinde Shizza,Arusha

TAMASHA la sita la vyombo vya habari Kanda ya kaskazini linatarajiwa kufanyika julai 24 katika viwanja vya General Tyre Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari mjini hapa leo,Mratibu wa Tamasha hilo, Jamila Omary alisema kuwa tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na TASWA - Arusha na kampuni ya MS Unique promotion ya Arusha, litashirikisha timu za waandishi wa habari toka mikoa ya Arusha, Manyara na Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa Katika tamasha hili, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku,mpira wa pete na mbio za magunia.

Mgeni rasmi katika tamasha hili anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Isdore Shirima pia kutakuwa na bendi ya Watoto wa Tembo ikiongozwa na Ndanda Kosovo siku ya tamasha.

Timu zitakazo shiriki katika tamasha hili ni TASWA Arusha,Taswa Dar,Radio Triple A,Radio 5, Radio Sunrise FM,Chuo cha uandishi wa habari cha Arusha, Radio ORS ya Terati mkoani Manyara,NSSF Arusha,TBL,Wazee Klabu na PEPSI.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya bia nchini, TBL, kampuni ya simu ya Vodacom, TANAPA,mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,NCAA, ALPHATEL, NSSF

Baada ya tamasha kutakuwa na hafla ambayo itafanyika Ricks klabu Philips kuanzia saa moja usiku hadi asubuhi.

Kwa upande wa meneja mauzo wa kampuni ya bia ya TBL kanda ya kaskazini Wilderson Kitio alisema kuwa wao wameona umuhimu wa michezo ndio maana wameamua kuthamini tamasha hili.

Aliongeza kuwa, pia wameamua kuwapa ushirikiano waandishi wa habari kwakuwa na wao wamekuwa wakiwapa ushirikiano katika mambo mbalimbali.

Alitoa wito kwa wapenzi wa michezo na wapenzi wa wanahabari wajitokeze kusherekea kwa pamoja katika tamasha hilo ambalo wameliandaa kwa ajili ya kujumuika pamoja.

Kwa upande wake meneja wa mawakala wa kanda ya kaskazini wa kampuni ya vodacom Maico Kasubi alisema kuwa wamefurahia sana kwa waandishi wa habari kutambua umuimu wao na kuwaruhusu kushiriki kwa pamoja katika tamasha hili.

Alitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hilo ambalo alisema waandishi wa habari wameandaa mambo mengi ikiwemo msaanii ambaye makazi yake ni mkoa wa arusha ajulikanae kama ndanda kosovo ambaye atakuwa na bendi yake ya watoto wa tembo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...