Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Pembeni ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga aliyemkaribisha Mhe. Spika Ubalozini.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga mara baada ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Pembeni ni mjumbe wa kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Beatrice Shelukindo aliyekuwa ameambatana na Mhe. Spika.
Spika wa bunge Mhe Anne Makinda akiwa katika mazungumzo na maafisa wa ubalozi wa Tanzania Nchini Uingereza wakati alipotembelea ubalozi huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga pamoja na watumishi wote wa Ubalozi wetu nchini Uingereza mara baada ya kutembelea Ubalozi wetu Uingereza. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...