Familia ya marehemu SARAH LUTHER GELLEGE ya Ukonga Madafu D'salaam, inapenda kutoa shukran zao za DHATI kwa ndugu,jamaa,majirani na marafiki wote waliokuwa pamoja nasi katika kipindi chote kigumu cha msiba wa mama yetu mpendwa SARAH. Tunaamini kila jambo afanyalo MUNGU anamakusudi yake!!!!!
Shukrani zetu ziwaendee madaktari na manesi wa Tumaini Hospital, Wachungaji wa Ukonga Madafu Lutheran Church, Kwaya zote za hapo kanisani haswa Kwaya ya Vijana ambayo ilikuwa pamoja nasi usiku na mchana siku zote za msiba kutufariji, Wanajumuiya ya madafu na vikundi vyote ambavyo vilijitoa kwa hali na mali katika kutufariji bila kusahau ndugu,jamaa, majirani na marafiki.
Kwa kuwa ni vigumu kutoa SHUKRANI kwa mtu mmoja mmoja,Tunaomba sana sana mpokee SHUKRANI ZETU ZA DHATI kwani mlitufariji sana.MUNGU azidi kuwabariki sana muendelee na moyo huo na MUNGU awaongezee pale mlipopungukiwa. ASANTENI SANA.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!!
Jamani POLENI SANA wana familia!! Tulikuzoea katika kutupambia na shughuli zote za mapambo jamani. MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
ReplyDelete