assalam aleikum waungwana.

sasa inashangaza mtu kununua simu ya bei mbaya kisha kuanza kubeep watu ukimuuliza anasema hakuwa na salio. utashindwaje kununua vocha ya shilingi 5000 wakati una simu ya shilingi laki5? na mbaya zaidi unapompigia mtu anayebeep huwa aidha hana la maana la kusema au atajibu NILIKUWA NAKUSALIMIA MKUU!!!!. sasa hujiuliza kusalimia ndio huku au? mara kadhaa wanaobeep huharibu utulivu wa vikao maofisini, kusababisha ajali barabarani na hata vifo nk. baadhi ya ofisi hupiga marufuku simu kwenye vikao kwa sababu ya kero za wanaobeep.
kwa mtazamo wangu kubeep kutakuwa na maana iwapo kutakuwepo mazingira yafuatayo:
1. iwapo wahusika walikubaliana kuwa nikikubeep namaanisha kuwa nimemaliza kazi au nipo tayari kwa safari au utoke nje tuonane na mfano wa hayo.
2. iwapo wahusika wamekubaliana kuwa nikikubeep namaanisha kuwa unipigie kwa kuwa sina credit ya kutosha.
3. iwapo wahusika wamekubaliana kuwa nikikubeep namaanisha kuwa kuna ujumbe mfupi (sms) nimekutumia na umepita muda mrefu sijapata jibu hivyo nasisitiza kuwa unijibu hiyo sms.
ukiondoa sababu hizo hapo juu ambazo ni lazima wahusika wawe wamekubaliana kabla, kubeep kutaendelea kuwa kero na maudhi kwa wamiliki wa simu. inasikitisha kuwa watu wengi wanaendeleza tabia hii ambayo kwa hakika inakera sana. baadhi wakibeep usipowapigia hununa na kukasirika. sasa hujiuliza nini maana ya kubeep? ulitaka nikupigie kwa nini usipige wewe? au jee tuliweka makubaliano hayo kuwa ukibeep nikupigie? maswali ni mengi na majibu ni machache.
nadhani kuna haja ya makampuni ya simu kudhibiti hali hii aidha kwa kutoza fedha kidogo kwa wanaobeep au kuchukua hatua kali zaidi juu yao. kuwe na system kuwa ukibeep ovyo unaweza kufungiwa line yako nk. wakati mwengine mtu hubeep zaidi ya mara 10 na unapoamua kumpigia kwa kudhani kuwa labda kuna emergency au ana shida muhimu unaishia kupata majibu ya kijinga...aaah niliona nikusalimie tu mzee....au aah nipo hapa klebu karibu na kwako... na majibu mengine kama hayo. wakati mwengine ulikuwa umelala kabisa umechoka na mizunguko ya maisha au upo na kazi very sensitive na mtu anakuondoa stimu kwa beep za kijinga.
naomba wadau wanisaidie mawazo yao jee kubeep hasa kuna maana gani maana mimi nimechoka na hii kero.
Mdau wa Kudeep..
Kubeeb maana yake ni kwamba "ninamiliki simu ya mkononi ingawa kiuchumi sistahili kuwa nayo"
ReplyDeleteWanasema hata Bilgate wakati mwingine anakuwa hana salio...inatokea kiukweli upo sehemu mbaya, salio limekwisha, duka lipo mbali, unachofanya nikumtafuta rafiki unayemjua `unabeep' sio mbaya, ila kuna wale wenzetu na sisi kweli wamezoea, kila akitaka kuwasiliana na mtu anabeep,...na sio swala la maana sana... halafu akipigiwa, anapokea kwa madaha, anakunja kwanza nne, simu ipo hewani hapo...anapokea kwa mikogo, simu ipo hewani hapo, halafu akianza kuongea, hana haraka..mpaka simu ilie tiii, salio limeisha...halafu anakashifu, watu wengine bwana wanakuwa mabahili wanaweka hela kidogo....
ReplyDeletejamani mumesikia kuwa Watanzania pamoja na umasikini wao wanaongoza kwa gharama za simu..lol
Sasa tutachangia nini hapa? wewe muuliza swali kweli swali lako ni la kizushi. Unataka tuchangie vitu visivyo na kichwa wala miguu? Uwe na mtazamo wa kimaendeleo zaidi....ujue wanadamu "tunatofautiana" wote hatuna tabia kama yako...kwa hiyo uvumilie ukibipiwa au uzime simu unapokuwa kwenye masuala muhimu. Achana na hasira za mkizi wewe, mind your business!
ReplyDelete1. KIJANA NA WEWE PIA UKIWA MIKUTANONI LAZIMA UJUWE MAANA YA KUZIMA SIMU.
ReplyDelete2. WATANZANIA SIE PIA TUJIFUNZE KUWA NA NETWORK MOJA TU IMEZIDI NI 2 MTU UTAMKUTA ANATAKA SIMU KARIBIA 5, UKIMUULIZA SABABU ANAKWAMBIA NA NETWORK 5, UKIMWAMBIA NUNUWA SIMU YENYE SIMCARD 2 ATAKWAMBIA YEYE HATAKI SIMU YA MCHINA ANABAKI KUOMBA NITUMIE SIMU BASI MKUU YA IPHONE NI TABIA MBAYA TU NA NETWORK ZA SIMU TANZANIA NDIO ZINASABABISHA HILI KUFANYIA WANANCHI WIZI NDIO MATOKEO YAKE WANA BEEP TU. MZ.
Simu za mkononi ni ghali sana kuziendesha kwa mTZ wa kawaida. Sasa hii kubeep ni kuwa yeye hana pesa au hataki kutumia pesa zake kumpigia mtu simu. Wanawake ndio wenye tabia hii sana.
ReplyDeletemie huwa inaniboa sana mbaya zaidi siku hizi sh.moja kwa sekunde, ninachokifanya atakenisumbua tu huwa namblock hanipati tena! hilo ndo suluhisho!
ReplyDeleteWewe mdau namba 2 wacha fixi zako huyo Bill Gates amebeep lini?
ReplyDeleteUnadhani watu kama wale wanatumia simu za vocha za prepaid za kukwangua? Grow up huo ni mtindo wa kwetu wa kimaskini unanunua kivocha cha shilingi mia tano halafu kikiisha ndiyo unabeep.
Kuna rafiki yangu aliniomba mchango wa harusi( kwa ku-beep sana mpaka nilipompigia) na nikamtumia dola 200 za kimarekani.
ReplyDeleteAlipozipata akaendelea kuni-beep sana nikadhani hakuzipata au amesahau namba ya Western Union niliyompa.
Nilipompigia kwa mara ya pili aliniambia kuwa alikuwa anani-beep ili nimpigie anishukuru kwa mchango niliomtumia (yaani hizo pesa hazikumtosha hata kuweka vocha ya kumuwezesha kunitumia msg, pum<<>?>?><BU zake, simpigii tena hata akipata msiba, Khabith yule.
We anonymous no 3..inaelekea ndo walewale wa kubeep..maana imekutouch hadi kumoyo..lol umekuwa mkali...hahah ha ha ha ha haaa...
ReplyDelete