Taarifa kwa Vyombo Vya Hahabri
Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (YUNA TZ) kwa kushirikiana na United Nations Alliance of Civilizaation (ambao pia ni wadhamini wakuu wa mradi huu), wanatekeleza mradi wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana katika Kuendeleza Amana, Usalama na Haki za Binadamu nchini Tanzania.
Mradi huu, Unatekelezwa katika mikoa kumi (10) ya Tanzania ambayo ni Mwanza, Dodoma, Mtwara, Kigoma, Mbeya, Ruvuma, Zanzibar, Tanga, Arusha and Dar es Salaam. Mradi huu ambao umeanza kutelezwa tangu mwishoni mwa 2010, una ngazi kuu mbili za utekelezaji ambapo, ngazi ya kwanza ilihusisha kubaini vijana ishirini (20) kuwa Vijana wawezeshaji wa kitaifa.
Vijana wawezeshaji hao walijengewa uwezo katika maeneo husika ya mradi ili waweze kuwafundisha vijana wengine pia. Katika ngazi ya pili, Vijana wawezeshaji wataenda katika mikoa yote 10 ya Tanzania na kuwafundisha vijana wenzao.
Malengo makuu ya mradi huu wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana katika kuendeleza Amani, Usalama na Haki za Binadamu ni kama ifuatavyo;-
Kuwajengea uwezo vijana ili waweze kushiriki ipasavyo katika kuimarisha na kuendeleza Amani, Usalama na kulinda na kutetea Haki za Binadamu.
Kujenga na kuendeleza utamaduni wa kuheshimiana na kuvumiliana katika mitizamo na Nyanja mbalimbali za kisiasa, kiutamaduni na kidini pamoja na kukuza uwajibikaji kwa kila mtu.
Kusadia na kuendeleza jukwaa la majadilino baina ya kundi rika la vijana na makundi rika mengine ili kukuza ushirikiano na kuendeleza majadiliano ya masuala muhimu ya ustawi wa Taifa letu bila kusababisha madhara hasi na pasipo kugombana.
Asasi ya Vijana ya Umoja wa Umoja wa mataifa inapenda kuutangazia umma wa wa-Tanzania na wadau wote wapenda Amani na Maendeleo kuhusu mradi huu muhimu ili kwa pamoja tuweze kuilinda Tanzania yetu iendelee kustawi zaidi na kuwa mahala salama na pazuri pa kuishi kwa ajili ya kizazi cha leo na cha baadae.
Mungu Ibariki Tanzania
Lawrence E. Chuma
Mratibu


Tatizo kubwa tulilonalo kuzidi hata janga la ukimwi na umaskini ni adui ufisadi mi nadhani ili jambo lolote la kuleta maendeleo liweze kutufanikisha nchini lazima lihusishe hili janga la kitaifa inalobakia kutafuna jamii ya kitanzania.
ReplyDeletemkoa wa Zanzibar ndio upi?
ReplyDelete