Patrick Mafisango akiwa amembeba Juma Kaseja baada ya mchezo kumakalizika.
Amir Maftah (shoto) na Kaseja wakishangilia ushindi wa Penati 5-4.
Golikipa wa Simba, Juma Kaseja akiwapungia mashabiki wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya timu ya El-Mereikh ya Sudan uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Kulia ni Kocha wa Makipa, Idd Pazi.
Mpira umeisha na Simba imeingia fainali ya CECAFA KAGAME CASTLE CUP kwa kuitoa El Mereikh ya Sudan kwa mabao 5-4 kwa njia ya penati. Hadi dakika 120 zinaisha ngoma ilikuwa droo 1-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2011

    SUBIRI JUMAPILI NDIYO UTAJUWA KAMA THERE IS ONLY ONE YANGA...NYODO ZAKO ZITAKWISHA ......

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2011

    Jamani tutajieni wafungaji wa magoli

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2011

    anony wa kwanza,umeumia yanga shughuli imeshaisha,kaseja kipa itabaki hivyo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2011

    we anony wa kwanza nadhani unaota ndoto, kwani yanga wameshafuzu? au ndio yaleyale ya juzi mmehakikishiwa na cecafa? ili mapato yazidi kwa kubebwa hata kwenye penalt.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2011

    Simba:Hizo hela mtakazozipata kwenye michuano hii kiasi fulani mfungue mtandao wa Timu..Watani wenu wameifungua www.yangasc.com.Mpira wa sasa hivi bila mtandao hamtafanikiwa.

    TFF:Mtandao wenu una habari za zamani sana:

    CECAFA:Mamilioni yote hayo hamna Mtandao?,nimejaribu kuwatafuta kwenye google siwapati.Msonye Tafadhali


    David V

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2011

    Hakuna wafungaji, simba butu hadi sasa wamefunga magoli mawili tu. Au tuhesabie na hizo penalty za baada ya mchezo?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2011

    anonymous 11:10:00

    cheki na hapa pia..jamaa wanajitahidi kiasi chake.
    www.kandanda.co.tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...