Ndugu Malumbo S Malumbo ni mwenzetu anaeishi hapa ujerumani, Anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Mama mmoja na Baba mmoja Bw Hamza S Malumbo (pichani) kilichotokea Ghafla huko Dar es salaam. Mipango ya mazishi inafanywa.
Kama ilivyo ada kwa watanzania kufa na kuzikana kwetu ni moja ya utamaduni wetu. Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) Unapenda kuwatangazia Watanzania wote wanaoishi hapa ujerumani. Tumfariji ndugu yetu Malumbo na Familia ya wafiwa. Kwa kumchangia senti kidogo kama Rambirambi kutoka kwa wanachama/watanzania tunaoishi ujerumani.
Ndugu watanzania mwenye 5 10. 15 euro na kuendelea tunaomba mchango wenu wa hali, ili tumfariji mwenzetu asijione yupo peke yake katika majonzi haya makubwa yaliyomfika. Pesa zitakazopatikana zitakabidhiwa kwa Familia ya Malumbo kama mchango wa Mazishi kutoka kwa Umoja wetu.
Tafadhali unaweza kutuma mchango wako moja kwa moja kwa Bw. Malumbo S Malumbo katika account Namba ifuatayo
Malumbo Salim Malumbo
Acc Nr. 7926977820
Blz. 310 108 33
Santander Consumer Bank
Nitamuomba Bw. Malumbo Kuratibu zoezi hilo kwa kukabidhi majina ya waliochanga kwa kamati ya umoja wa watanzania Ujerumani (UTU) kupitia e mail yetu ya kamati mara baada ya zoezi hili kukamilika, ili kuweka kumbukumbu. Kamati pia itamtumia kila mtanzania orodha ya waliochangia.
Huu ndio Utanzania Halisi wakati wa shida tusaidiane na wakati wa Raha pia tufurahi pamoja.
Umoja wa watanzania Ujerumani umesikitishwa sana na habari hizi za majonzi na unajumuika na Familia ya Malumbo katika kipindi chote cha maombolezi.
Tunamuomba Mwenyezi mungu aiweke roho ya Ndugu yetu Hamza S Malumbo Mahala Pema Peponi
AMIN
Kny
Kamati
Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti
Poleni sana wajomba Malumbo na Hamisi pamoja na wafiwa woote. Hiyo ni kazi ya Mungu na haina makosa, tumuombee marehemu makazi mema huko aendako.
ReplyDeleteHamim, U S A
Mwenyekiti, hongereni sana Watanzania wa Ujerumani kwa ushirikiano wenu.
ReplyDeleteTafadhali tuwekeeni na mawasiliano ya simu za wafiwa ili nasi tulioko mbali ( sio ujrumani) tuweze kuwafariji na kutuma michango yetu.
Inna Lillah Wainna Ilayhu Rajeeuun.
Massoud, USA
poleni sana wafiwa mungu awape wepec, MI SIJAELEWA HII HABAR YA KUWA MAJINA YATUNZWE KWA WALIOCHANGA ILI IWEJE KUWA WASIOJALIWA WAONEKANE WABAYA AU?ACHEN USWAHILI MPAKA KWENYE MISIBA MTU KAMA ANACHO ATOE KAMA HANA BAC MAMBO YA KUTUMIANA MAJINA NDO IONEKANE VP BADILIKEN JAMAN MKO UGHAIBUN BADILIKEN AAAAAAH INABOA MDAU SWEDEN
ReplyDeleteHallo Mdau Massoud. Mawasiliano ya wafiwa
ReplyDeleteMalumbo Ujerumani anapatikana ktk namba hii +4917636737351