Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Peopleshome Association kutoka nchini Ujerumani , Kretzschmar akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Bunge mjini Dodoma leo kuhusu mradi huo.
Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa African Business Information Bank,Tumenta Kennedy kutoka nchini Ujerumani akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi za Bunge kuhusu mradi wa umeme wa jua mjini Dodoma na {kushoto) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Peopleshome Association,toka Ujerumani pia Ulrich Kretzschmar. Mradi huo unatarajia kugharimu Euro milioni 150, utatekelezwa mkoa wa Katavi ,Kigoma na Kahama utaanza Januari mwakani.

NA MAGRETH KINABO - DODOMA

JUMLA ya Euro milioni 150 zinatarajiwa kutumika katika mradi wa umeme wa jua katika mikoa ya Katavi, Kigoma na Shinyanga ili kuweza kukabiliana na tatizo la uhaba wa umeme .

Hayo yamesemwa na Ofisa Mkuu wa kampuni ya umeme wa jua ijulikanayo kwa jina la Peopleshome Association kutoka nchini Ujerumani , Ulrich Kretzschmar wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Bunge mjini Dodoma(leo).

“Tumeshazungumza na Waziri Mkuu ,Mizengo Pinda kuhusu mradi huu, ambapo tayari ameshaukubali , hivyo tunataka kutekeleza mradi huu kwa umakini,” alisema Kretzschmar huku akisisitiza kuwa mradi utakelezwa ambapo faida itabakia kwa nchi ya Tanzania hivyo wao hawahitaji faida.

Aliongeza mradi huo unaratajiwa kuanza kutekelezwa Januari mwakani kuwa fedha za kutumika kwenye mradi huo, zitatoka katika serikali hya Ujerumani, benki na wadau mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa African Business Information Bank, aambayo inashirikiana na kampuni hiyoTumenta Kennedy, alisema mradi utakuwa ni MW 50, ambapo MW 20 za Katavi, 20 Kigoma na Kahama MW 10. Alisema asilimia 99 ya umeme huo utakuwa akwa ajili ya viwanda na iliyobakia ni ya makazi.

Aliongeza kuwa pia mradi huo utahusisha ujengaji wa nyumba 1000 ambazo zitawekewa umeme huo, 400 zitakuwa Katavi, 400 Kigoma na 200 Kahama, huku akisema nyumba hizo zitauzwa kwa Watanzania kwa gharama nafuu.

Kennedy alisema mradi huo upawapatia ajira Watanzania 1000 na kufanywa na wakandarasi Watanzania. Hivyo mradi huo utasaidian kubadilishana teknolojia na ujuzi.

Alisema hivi sasa waklo nchini kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa seriakli wabunge na wadau mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...