Mdau Dixon Busagaga wa globu ya jamii akiangalia gari jinsi ilivyoumia mara baada ya kupata ajali wakati akiwa njiani kuelekea Dar .

WAANDISHI wa habari Abdalah Hussein maarufu kama "Master voice"aliyewahi kufanyakazi radio one na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi jana wamenusurika katika ajali ya gari ndogo aina ya Toyota Carina yenye namba za usajili T 790 BRD iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 7 mchana eneo la Kwa Makunganya kilometa chache kutoka kambi ya Sokoine baada ya gurudumu la nyuma kupasuka na gari kupoteza muelekeo kiugonga mti kisha kuingia kwenye mtaro.

Hata hivyo mungu ni mwema watu wote 6 waliokuwemo katika ajali hiyo wakiwemo watoto wawili,familia ya Abdalah Hussein hakuna alieyeumia mbali ya kuibiwa vifaa mbalimbali likiwemo begi dogo lililokuwa na
Camera aina ya Nikon na Laptop,Toshiba.

Abdalah Hussein akitazama gari ilivyoharibika.

Familia ya Abdalah Hussein wakitoka katika gari baada ya ajali.

Mafundi gari wa mkoani Morogoro walifika kuangalia uwezekano wa kutengeneza.

Gari inavyoonekana baada ya ajali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2011

    Gurudumu la nyuma haliwezi kunitoa barabarani inaelekea dereva si mzoefu wa kuendesha au hakuwa amekoncentreti. Nimesha wahi kupasukiwa na gurudume la mbele mara nyingi nikiwa ktk speed 130 wakati wa zile tairi za Dunlop na sijawahi kutoa gari nje ya barabara. Inadidi kutafutwe utaratibu watu wajifunze nini chakufanya katika dharura kama hizi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2011

    Ilikuwaje gari akaacha njia? Unapofanya safari ndefu unashauria kupumzika kila baada ya masafa maalum ili akili yako ipowe. Hapa mdau aliyekuwa dereva akili yake ilikuwa haipo kwenye kazi ya kuendesha gari. Tumshukuru Allah kwani hakuna majeruhi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2011

    Kwanza poleni na kukutwa na hiyo ajali. lakini waandishi wa habari ndio mnatakiwa kuwa mfano na kuielimisha jamii kuhusu tahadhari na usalama barabarani - wewe utabebaje watoto wadogo katika gari (tena safari ndefu kama hiyo) bila kuwafunga mikanda au kuwa na viti vyao maalum vinavyoweza kuwakinga pindi itokeapo ajali kama hiyo. Tunapoingia kwenye utamaduni wa kuendesha magari, basi ni vyema pia tuzingatie utamaduni wa usalama na tahadhari stahiki za utumiaji wa vyonbo hivi vya moto. Ufungaji mikanda umeokoa maisha ya watu wengi pindi itokeapo ajali. Iige tabia hiyo nzuri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2011

    walikuwa wamefunga mkanda ndio maana wote wko salama,poleni sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2011

    gari iliacha njia baada ya tairi kumenyeka kama nilivyoliona pale gereji ya moro,msilaumu mtu kabla hamjajua mazingira ya ajali,wote wako salama ina maana mikanda ilifungwa,poleni ndugu zangu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 11, 2011

    Inashauriwa kuwa kabla ya kufanya safari ndefu mtu anunue tairi nyingine ufunge kwenye gari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...