Ankal salaam,
Pole na majukumu ya kulijenga Taifa hili japo linaonekana halijengeki kwa sababu ya watu wachache.
Nadhani hata wiki mbili hazijaisha toka serikali yetu itangaze kuwa kuanzia mwezi huu wa saba (July) kulingana na kuanza kutumika kwa bajeti mpya ya 2011/2012 kwamba bidhaa mbali mbali zingeshuka bei.
Na katika hili tuliona hata wabunge wetu wakipiga kelele sana pale mjengoni kuhusu suala la nishati ya Mafuta kwani imeonekana ni kupanda kwake bei ni kikwazo kwa uchumi na maisha yetu kwa ujumla.
Huku watanzania wengi tukiwa na hamu ya kusubiri kuona bidhaa hii muhimu ikishuka bei pengine kutoka shilingi 2200/liter (bei za mkoani Shinyanga) hadi shilingi 1200/liter, mkoani Shinyanga hali ni tofauti. Taswira hii hapa chini inaonyesha bei za pump kwenye filling station nyingi kama inavyoonekana leo tarehe 4/7/2011.
Pichani ni bei za mafuta leo tarehe 4/7/2011 mjini Shinyanga.
Pichani ni bei za mafuta leo tarehe 4/7/2011 mjini Shinyanga.
Kutokana na hili nimejiuliza maswali mengi sana ambayo majibu yake sijayapata mpaka sasa labda wadau wanaweza nisaidia! Miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na:
1. Hivi serikali na wabunge wetu walipokuwa wakitangaza habari za kushuka kwa bei za mafuta kuanzia July mosi walikuwa serious au walikuwa wanatania?
2. Hawa EWURA wao kwa akili ya kufuatilia haya mambo kwa kina ama wana interest zingine tu?
3. Vipi hawa wafanya biashara, ni kwamba wanadharau serikali yao au wanajua kuwa serikali haina madhara so wanajipangia bei wanavyotaka?
4. Lakini pia nini nafasi ya Mtanzania ambae anaathirika na gharama hizi kubwa za mafuta? Je afanye nini ili mambo yanyooke?
5. Kuna sababu ya wananchi kuiamini serikali?
Nimepata wakati mgumu sana kupata majibu ya mswali haya, mwisho nikajisemea kuwa kwa hali hii wananchi wakiingia barabarani na mabango serikali itawaita wavuruga AMANI?
Mbaya zaidi walisema ongezeko la kodi kwenye bidhaa ya mafuta ya taa hakutaadhiri bei za bidhaa hiyo!! Lakini kwa mkoani Shinyanga kabla ya July mosi bei ya mafuta ya taa ilikuwa shilingi 1850/liter, leo hii bei iko tambarare na petrol na diesel!!! Sasa hapa manake nini???
Mdau wa Shinyanga.
Angalieni link hiyo kuhusu Machimbo ya Uranium Tanzania ambayo Tanzania katika USD 200 Million itapata USD 5Million.
ReplyDeletehttp://www.bbc.co.uk/news/world-africa-13989264
hapo ndio bei imeshuka!!! marcio maximo alisema wachezaji wa tanzania, wengi hawana nidhamu, alikuwa ana maana watanzania wengi hawana nidhamu. wangekuwa na nidhamu wangelifanyia kazi na kulifuatilia. ndio maana wanaona posho za vikao ni haki yao iliyosafi bila mawaa!
ReplyDeletemimi kama mdau aliewasilisha sijaelewa mantiki ya serikali kupunguza kodi za EWURA,TRA,TBS na TPA wakati mfauta yameendelea kupanda badala ya kushuka.Tarehe 1/7/2011 chapisho la EWURA lilionyesha bei elekezi DSM ingekuwa petrol 2,052 hadi 2,206 wakati diesel ingeuzwa 1,939 hadi 2,084, kitu ambacho sijaona punguzo lolote hada hapo.Leo hii BP petrol ni 2,226= sasa ndugu wa shinyanga nafuu yako wewe.HEBU TUELIMISHENI SISI AMBAO HATUKUELEWA ILE BAJETI KUHUSU BEI YA NISHATI, ILIPANDISHWA AU KUSHUSHWA? huu naona ni usanii mungine wa serikali yetu katika njia ileile kuwahadaa wananchi wake.Kama sijakosea waziri Nkullo alisema kuna punguzo la sh.345 katika kodi ya mafuta imepunguzwa, sasa kwa nini yaendelee kupanda? au huu uchumi hatuuelewi vizuri
ReplyDeleteSource ya mafuta kupanda bei kila uchwao sio kodi kama serikali inavyotaka tuamini. Hata kama wataondoa kodi zote za mafuta lakini wakashindwa kui-control shilingi (Inflation) basi haya mafuta yataendelea kupanda bei day in day out. Time will tell.
ReplyDeleteMIMI NINAVYOONA KWAMBA TANZANIA TUMESHINDWA KUJITAWALA NA PIA HATUNA UZALENDO BORA,MUHIMU TUWARUDISHE WAKOLONI WETU WALIOTUTAWALA KIKAMILIFU SIO KAMA HIVI SASA TUNAWARUDISHA KIMITINDO TU NI HASARA KUBWA KWA TAIFA MAANA HATUJULIKANI WAPI TUPO NA WAPI TUNAELEKEZWA NA VIONGOZI WA TAIFA LA TANZANIA TUFANYENI TUAMKE MAPEMA KABLA HAWA VIONGOZI HAWAJAZIMALIZA RASLIMALI ZA TAIFA.Mdau bwegenaz
ReplyDeleteHivi hizo Mamlaka mbona zinakaidi amri, na kuvunja sheria na taratibu...yaani mnazidi kuwabana wananchi tu...hakyanani...ningekuwa Rais...kweli ningekuwa Dictator kwa wale wanaowaonea wananchi...kudadadeki zenu!
ReplyDeleteNchi yetu ni nzuri sana hakuna nchi kama TANZANIA maana tunapata vihela vihela vya kiujanjajanja hakuna kulalamika ila Watanzania (TUPO KWENYE CHUPA)
ReplyDeleteKisa cha kupandisha bei mafuta ya taa ni wafanyabiashara wanaochanganya mafuta ya taa na diesel hivi nchi haina usalama (polisi)
Wabunge wanatetea posho kwa sababu wananchi wanawaomba pesa wabunge(NDIO MAANA NASEMA TANZANIA NI NCHI NZURI DUNIANI WATU WANAISHI KWA KUMTEGEMEA MTU)Nenda ulaya mtu bila kazi huli chakula
siku nyerere anakufa. Nilijua 10 yrs after kifo mabaya yataonekana. These people walianza take advantage soon nyerere alipokufa. walianza kuiba na kutumia madaraka vibaya soon after his death. walikaa kikao na kujigawia raslimali bila kutushirikisha. mnayoyaona sasa ni matokeo ya kugawana ufujaji mara baada ya baba wa taifa. Sasa tufanyeje? watanzania ni wapuuziaji wa mambo. Leo twalalamika 2014 hawa watu wataanza kujaribu utekelezaji tena ili kuwasahaulisha 4yrs ya msoto. na tulivo wajinga, tutawapa kura zetu na hata kuwasaidia kuziiba kwenye vituo ambavyo hawajapata. baya zaidi, walio na tu-hela twa kubadilisha mboga ni ki-mkoko cha second hand watalala usingizi siku ya upigaji kura na wala wasikumbuke machungu ya miaka 5. sielewi sisi ni watu wa aina gani. katiba imetushinda.
ReplyDelete