HABARI BWANA MICHUZI,

KWANZA NAKUPONGEZA KWA KUTUHABARISHA MAMBO MBALIMBALI YA NYUMBANI TZ. MIMI NAOMBA UNIWEKEE KERO YANGU KUHUSU CHUO CHA UHASIBU TANZANIA, AL-MAARUFU KAMA TIA.

HAWA JAMAA BADO WANAFANYA KAZI KIZAMANI SANA. MIMI NIMEOMBA KOZI HAPO YA MASTERS MWAKA WA MASOMO 2011/2012. NIMELAZIMIKA KUSAFIRI KUFIKA DAR NA KUKAMILISHA TARATIBU ZA KUJAZA FOMU NA KULIPIA.

 SASA TANGU NILIPOMALIZA PROCESS HIYO HADI LEO NI KIMYA HAKUNA TAARIFA YOYOTE. MIMI SIISHI DAR BALI MKOANI. KABLA YA KURUDI KUTOKA DAR NILIWAULIZA JEE NITAJUAJE KAMA NIMEPATA ADMISSION. WAKAJIBU WATATUMIA NJIA ZA SIMU, BARUA PEPE NA ANUWANI ZA POSTA NILIZOTUMIA KATIKA FOMU YA MAOMBI.

HATAHIVYO HADI LEO NI KIMYA WAKATI KOZI INAANZA MWEZI SEPTEMBA 2011 NA KAMA TUNAVYOJUA TOFAUTI NA KOZI ZA BACHELOR, WATU WA MASTERS WENGI NI WATUMISHI WA UMMA AMBAPO UNALAZIMIKA BAADA YA KUPATA ADMISSION KUFUATA TARATIBU ZA KIOFISI KUOMBA RUHUSA. HAWA JAMAA NI KIMYA KABISA.

BAADA YA MUDA NIKAAMUA KUTUMA E-MAIL KUULIZIA. HADI LEO SIJAJIBIWA!!! HATA KUAMBIWA TUNASHUGHULIKIA PIA IMEWASHINDA. NIKAAMUA KUPIGA SIMU ZAO AMBAZO ZIPO KATIKA MTANDAO WAO AMBAZO NI +255 22 2851035 NA +255 22 2851036. NI WIKI YA PILI SASA NAPIGA NAMBA HIZO NYAKATI TOFAUTI SIMU ZINAITA LKN HAKUNA ANAYEPOKEA. MWANZO NILIDHANI LABDA ITAKUWA MHUSIKA AMETOKA KIDOGO. LKN HATA UKIBADILI MUDA AU SIKU BADO SIMU HAZIPOKEWI IJAPOKUWA ZINAITA.

SASA NAOMBA HAWA JAMAA WAKISOMA POST HII, WAJUWE KUWA WANABOA. HII NI KARNE YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA SIO MIAKA 5000 KABLA YA KUZALIWA KRISTU. WAWE WANAJIBU MAWASILIANO NA KUTOA UFAFANUZI. WAKUMBUKE KUWA TUNALIPIA HAPO NA ADA NI PESA NYINGI TU SASA KWANINI WANAOPERATE KIENYEJI HIVYO? HIVI WANAPOKUWA KIMYA WANATAKA KUSEMA TUWAELEWEJE?

MWANAFUNZI MTARAJIWA TIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2011

    pole sana hiyo ndio nchi yetu ya wadanganyika maendeleo zero.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2011

    Achana nao vyuo vipo vingi Tanzania omba kwingine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2011

    Hiyo ni kila nchi ambako kuna huduma ambayo ya kukupa maendeleo wewe binafsi. Hakuna anayejali wewe masomo unaanza lini, uhamiaji ndio hao, wanakutambua wewe pale tu wanapotaka pesa kwako.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2011

    Pole sana ndg yangu. Sayansi na Teknolojia tunaisikia kwa wenzetu tu, lakini nchi kama Tanzania, namna wanavyoendesha ofisi utachanganyikiwa. Njoo ughaibuni uone mambo yanavyoenda faster. Kila kitu kipo set hadi kuna wakati unahisi home huwezi rudi tena. Lakini kwetu ni kwetu, na sisi ndio tunaopaswa kurekebisha hii hali. Mambo mengi bado yanaendeshwa kienyeji sana Tz. Nadhani wakati umefika sasa kuanza kuwasomesha kwa wingi na kuajiri watu wa IT wengi ili waweze kusaidia masuala ya Mitandao na Computer. duh Mungu inusuru Tz.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2011

    Usishangae hiyo ndiyo TIA ndugu yangu, unapanda Mabasi kuja DAR eS SALAAM kuchukua application form ya masters? Chuo cha karne hii? KAZI IPO, ANYWAY UNAJUA KILE CHUO CHA SERIKALI na kinaendeshwa na CEO sio Principal SO ule ukiritimba wa serikalini typical upo na HAMNA MWENYE KUJISHUGHULISHA SAANA NA ISSUES kama hizo. Poleeee

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2011

    Nenda UDSM

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2011

    hiyo ndio TIA.mwenzako nipo hapo mwaka wa tatu,yaani ni balaa tupu.mpaka leo hata huyo CEO bado ni acting,coz amestaafu tokea mwaka jana.
    Hatuna uongozi wa serikali ya wanafunzi,kisa rais mstaafu alikula hela za TIASO.hata hatujui nani atatuwakilisha kwenye board kwa ajili ya course work zetu.
    yaani kiufupi,uhasibu ni balaa.wacha tumalize tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2011

    CEO ni acting kwani TIA nayo imekuwa mkoa wa Dar es Salaam? Manake kumbe kuna baadhi ya vitu vinaweza kwenda bila uongozi kama ilivyo jiji la Dar es salaam....
    Mwaka mzima mkoa hauna RC, sijui JK na serikali kwa ujumla haina mtu wa kumpa mkoa.
    Very hopeless country, but still our loving country.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...