Baadhi ya wakaazi wa manispaa wakiwa wamepiga foleni kwa kununua sukari kwa bei nafuu ya shilingi 1,700 inayouzwa na wakala wa kiwanda cha sukari cha Kagera Bw.  Amir Hamza. Bei ya sukari mkoani Kagera imekuwa ikipandishwa kiholela na wafanyabiashara wa sukari kwenye maduka kwa bei ya kilo moja kati ya shilingi 2,100 hadi 2,500. 
Mmoja wawakazi wa mannispaa akiwa amebeba mfuko wa sukari baada ya kuununua toka wakala wa kiwanda cha sukari cha Kagera. Kwa sasa mkoani Kagera kuna uhaba mkubwa wa sukari unaosababishwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaosafirisha sukari inayozalishwa na kiwanda cha sukari hicho kwenda nchini Uganda kwa njia ya magendo. Inadaiwa bei ya sukari nchini Uganda ni shilingi za kiganda 7,000. 
Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbona mnaturejesha kule kule kwa enzi ya mwanzilishi!!!

    ReplyDelete
  2. Siku zote huwa sielewi kwanini bei ya sukari ktk mkoa wa Kagera ni kubwa kuliko mikoa mingine wakati wana kiwanda cha sukari? Nadhani kuna tatizo kubwa la mfumo wa usambazaji sio tu kupeleka Uganda.

    ReplyDelete
  3. kagera si kuna kiwanda cha sukari, hii kali, haya mambo hayaigii akilini au kuna issue underground ya kiutawala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...