Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Fedha hizo zitatumia kwa ajili ya miradi ya uwezeshaji wa wanawake.
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimuelezea Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo . Benki ya NMB imeichangia taasisi hiyo shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumia kwa ajili ya miradi ya uwezeshaji wa wanawake.
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimuonyesha kabrasha lenye kazi mbalimbali za WAMA Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10. Fedha hizo zitatumia kwa ajili ya miradi ya uwezeshaji wa wanawake.
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB (kushoto) na ShyRose Banji ambaye ni Afisa Mahusiano (kulia) katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...