KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jana, katika Offisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM mjini Dar es Salaam, kutangaza mgombea wa jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM. Kushoto ni mlezi wa mkoa wa Tabora, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba. Picha na mdau Bashir Nkoromo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwa nini mhangaike kufika kote wakati ninyi ni chama tawala tokea uhuru, si wananchi wanatakiwa tu kuwapigia kura bila ya nyinyi kusumbuka namna hiyo kutokana na ukomavu wenu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo? Mambo si yanaonekana wazi wazi jamani, au? Mnatakiwa mtulie tu muwaache wapinzani wahangaike kujitambulisha maana wao ni wageni na wachanga, ila nyinyi CCM mnajulikana tayari, tena tokea kitambo kweli kweli. Vuneni mlichopanda, tulizeni boli.

    ReplyDelete
  2. We mdau wa kwanza umeniacha hoi, sijui nikufikirie vipi. Kwa mpangilio wa sentensi zako za mwanzo utafikiri unawasanifu CCM (i thought you were being sarcastic, and frankly, it would have been really funny and also quite clever), lakini duh kumbe mwenzangu upo serious. Kweli kazi tunayo. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. HATUDANGANYIKI.
    MMESHINDWA KUONGOZA NCHI.

    ReplyDelete
  4. Yaani mimi nikiona rangi za kijani basi nakosa raha kabisa na presha inapanda kwa hasira.. hivi sasa nina mpango hata wa kutokula mboga za majani zenye asili ya ukijani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...