mdau akiwa na vazi rasmi
Msafara ukizunguka Notting hill.
Salam,
URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na Miss Jestina Blog wanakuletea matukio katika picha ya Notting hill Carnival iliyofanyika Jumapili tarehe 28 agosti 2011. Hii ilikuwa siku ya kwanza Carnival ya watoto ambayo hufanyika kila mwaka tangu mwaka 1964 ikifuatiwa kesho yake siku ya jumatatu ikiwa siku ya watu wazima.
Maelfu ya watu zaidi walijitokeza katika mitaa ya Notting hill wakati wa Carnival ya jana ambayo ni tofauti na miaka yote pia nyongezo ya polisi 1000 wa ziada na kufanya Jumla ya polisi 6500 kwa ajili ya usalama na kufanikisha shuguli nzima ya wanachi walio hudhuria. Hii inatoka na maasi yaliyo tokea hivi karibuni katika kitongoji cha Tottenham na sehemu nyingine nchini Uingereza.
Jumla ya watu 53 wanashikiliwa na polisi kutokana kutaka kufanya fujo jana katika carnival.
Msanii Kutoka Urban Pulse alifanya makamuzi katika Carnival hii iliyohudhuriwa na watu wengi, mmojawapo wa wadau waliojitokeza kumuunga mkono ni msanii Page kutoka Xfactor.
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE NA MISS JESTINA BLOG
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...