
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya mjini,John Mwambigija akiwa na nakala ya hotuba ya Waziri wa mambo ya ndani kivuli,Godbless lema,akisoma sehemu ya Hotuba hiyo mbadala ya kambi ya upinzani wakati wakilaani kauli ya aliyekuwa Ofisa wa Polisi Abdallah Zombe, huku Katibu Mwenezi wa wilaya,Manyerere akimsaidia kushika kipaza sauti. Bw. Zombe alikaririwa majuzi kumweleza Mh. Lema kuwa hajui katiba baada ya Mbunge huyo wa Arusha mjini kuhoji hukumu ya kuachiwa huru Bw. Zombe katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara jijini Dar es salaam. Bw. Zombe aliapa kwamba atajinyonga endapo kama CHADEMA watachaguliwa kuongoza nchi.

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya,wakiwasalimia wananchi wa Kata ya Ruanda juzi, katika mkutano wa 'Operesheni twanga kote kote', unaoendelea kufanywa na chama hicho, mkoani Mbeya, Picha Zote na Mdau Thompson Mpanji
Hao sio mgambo kweli?
ReplyDelete