Salamu,
 Nia yangu ya kushirikisha wadau na kuusambaza ujumbe huu si tu kuonesha hasira na masikitiko yangu kwa yanayojiri na kuendelea nchini bali pia kuvunja ukimya na kuwapa sauti wanaoonewa na kukandamizwa na uonevu unaotokana na kuvunjwa sheria kiholela na bila sheria kufuata mkondo wake kila inapovunjwa.

Nakusudia kupaaza sauti ili ujumbe huu ufike mbali iwezekanavyo kwa vyombo husika ili hatimaye suti hiyo isikike na hatua ziweze kuchukuliwa. Tukio hili moja linazua mijajadala kadhaa ikiwa ni pamoja na dhidi ya ulazima wa kutolewa fomu ya PF£ kabla ya huduma hasa wakati wa dharura ya ajali, dhidi ya dereva anayefanya kosa la barabarani na dhidi ya raia wanavyochukua hatua dhidi ya matendo ya uhalifu. Ninachokataa hapa ni ile dhan potofu kwamba mambo kama haya ni nje ya uwezo wetu.

Jana mdogo wangu kauwawa katika ajali ya  Hit and run- katika barabara ya Kinondoni sehemu za Open University jijini Dar es salaam, ile inayokata kwenda Mwananyamala Hospital majira ya saa 3 usiku. 

Kwa vile driver hakusimama na hakuna mtu aliyejali kumsikiliza na kumhudumia  mdogo wangu  alipoanguka na kutokwa damu hadi kufa  baada ya kugongwa. 

Aliyemuua katoroka na labda imekuwa kheri mara mbili: kwanza kamuacha karibu na nyumbani ambapo hatimaye mlinzi aliweza kumtambua na kutoa taarifa; pili angeweza kumtokomeza mbali kama ilivyokuwa kwa yule mtoto wa shule aliyechukuliwa alipogongwa Temeke na aliyemgonga kusimama kumchukuwa watu wakadhani anapelekwa hospitali kumbe kenda kutoswa Coco Beach kupoteza ushahidi. 

Kinachosikitisha ni kuwa mdogo wangu kafa kama  mita  500 toka Mwanyanyamala hospital. Alipopelekwa kwa ajili ya huduma kwanza walitaka aletwe na PF3 badala ya kumpa huduma ya kwanza. Hivyo, kati ya ile kukaa bila kuhudumiw baada ya kugongwa na baada ya kuchukuliwa na kupelekwa hospitali roho ya binadamu imekwenda. 

Kadhia ya ajali za barabarani si tu kwa mabasi yanokwenda mikoani au kwa waenda kwa miguu. Wala si tu kwa madaladala kwani aliyemgonga marehemu si tingo mhuni bali ni mtu huenda anaitwa mheshimia au kaka… Binafsi hivi karibuni tu nimetishiwa kuuwawa baada ya kijana tajiri jeuri kurudisha gari ya reverse hafla katika main road kutoka alipokuwa ameegesha. Nilipomhoji anafanya nini na ana kusudio gani jibu lake kwangu lilikuwa “ntakutwanga risasi”.

Je, hali hii itaendelea hadi lini?
Nawasilisha Mdau Mwenye Majonzi na hasira
Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Pole sana kwa msiba uliokupata mwenyezi mungu akupe roho ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Hilo tatizo lipo katika jamii yetu ya kitanzania na wauguzi na madaktari wanajaribu kutumia hiyo fomu ya polisi namba tatu(PF3)kama njia yakupata rushwa.

    Sheria za dharura zipo kwamba alipaswa ahudumiwe kwanza halafu maelezo mengine yatafuata baadaye. Kwa kweli kuna haja yakuanzisha movement hili tuibadilishe nchi yetu maana kila sehemu kumeoza sijui twende wapi?

    Nchi yetu mpaka kutokee msukumo ndipo watu wanafanyekazi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  2. Na ungepeleka PF3 wangesema umeme hakuna na mishumaa imeisha, kweli watanzania ubinadamu umetutoka kabisa kuna waumini wengi wa dini zote lakini sijui kwanini watu wanakuwa na roho mbaya ya kupenda mslahi kwanza bila kutoa msaada na kuendekeza ubinafsi. Ina hitajika msukumo wa nguvu na wenye moyo haswa kubadilisha tabia hii iliyoota mizizi minene na migumu kutoka kama ya mikoko
    Mkerwa mnoo!!!

    ReplyDelete
  3. Dah, Pole sana mdau kwa msiba, yaani imenisikitisha sana! Pole kwa mara nyingine.
    Iliwahi kunitokea hata mimi mdogo wangu alipata matatizo alipigwa na wanajeshi, bahati mbaya au nzuri kuna mtu anamfahamu na ananifahamu mimi pia maana wanafanya kazi wote. Akanipigia simu na bahati nzuri nina kausafiri nikatoka mbio kwenda eneo la tukio. Dah nilimkuta dogo yuko kwenye hali mbaya sana, nilimchukua mbio nikielekea Temeke hospital yule jamaa akanishauri tupitie PF3 maana hawatampokea hospital. Nikapitia kituo kidogo(Mwembeyanga), duh askari oooh kwani umepita vituo vidogo vingapi mpaka uje hapa? nikawaomba mpaka nikatoa tip 5,000/- akaandika haraka sana!
    Kufika hospital ni kama saa tano kasoro usiku, huwezi amaini kundi la kinamama wengi na watoto wote wanenda kumuona daktari mmoja tu aliyekuwepo (Bonge la foleni) "nilienda Temake hospital baada ya kukataliwa hospital binafsi maana walisema anahitaji matibabu ya hali ya juu zaidi so ni vema nimpeleke Temeke. Ilibidi nimtumie Nurse wa zamu kwa kumtipu pia ili kumuona daktari, na kuwatip watu wote waliohusika mpaka dogo akatibiwa. Roho iliniuma sikujiona shujaa kuwapita wale kina mama na watoto ambao walikuwa wanataka kumuona daktari ambaye nilimkuta anaongea na simu mguu mezani.
    Nachotaka kusema mfumo mzima umeharibika kuanzia barabarani, polisi, mahospitalini watu hawajali utu tena bali fedha. na hii inatokana na uongozi waote wa kitaifa kuwa umeoza. In short viongozi na watendaji wazuri serikalini ni endangered species (yaani wako hatarini kutoweka)!

    ReplyDelete
  4. UNAJUA WATANZANIA WATU WA AJABU SANA... CHADEMA waliposema nchi hii haina haki, kwamba haina utawala bora wa sheria, wakazimiwa vipaza sauti bungeni kunyamazishwa. Wakitoa hotuba iliyojaa malalamiko kwa niaba yao na kwa niaba ya wananchi, waziri Lukuvi anasimama kuipinga(tena bila utaratibu kwasababu anaomba muongozo alafu anatoa hotuba kinyume ha utaratibu), Chadema wakipaza sauti kukataa upendeleo huu wanatolewa nje: nyie watanzania badala ya kuwaelewa na kuwaunga mkono mnakubaliana na kina Lukuvi kwamba wanafanya fuju bungeni kwa kuvunja taratibu!!

    Kwa hiyo mnanyimwa haki hospital, mnatishiwa barabarani, wanajeshi wanawapiga ndugu zenu, polisi wanauwa ndugu zenu hamna kesi, Chadema wakilalamika bungeni wananyamazishwa...alafu hamuawaungi mkono, hiyo haki mnayolilia mtapata wapi?

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli sheria ni msumeno na watu wengi wanakufa kwa sababu sheria inasubiriwa ichukue mkondo wake. Kwa kweli inasikitisha sana kuona mambo kama haya. Sheria inatakiwa ibadilike maana ya sasa inasababisha vifo. Kuna daktari mmoja ughaibuni alibidi avunje sheria ili aweze kufanya utafiti wa tiba ya moyo ambayo sasa inatumika na kuwaponya watu wengi.

    ReplyDelete
  6. POLE SANA MDAU na MUNGU aiweke Roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEN.

    Mimi naona hizi ajali ni janga la Kitaifa watu wengi wanapata ulemavu wa muda mrefu na wengine kufa kila siku. Kama haijakukuta uwezi jua bali hali ni mbaya. Hata angesimama provided ana hela yeye ndo angekuwa sahihi.

    Hali mbaya kila sehemu mungu atuepushe.

    Observer

    ReplyDelete
  7. HAWA VIONGOZI NA SHERIA NYINGINE ZISIZO NA MAANA KABISA,MIMI NILISHAWAHI KULIFIKIRIA HILI SWALA ILA SIKUPATA JIBU KABISA.

    ReplyDelete
  8. Masuala haya yapo mda mrefu, na kwa kweli yanasikitisha sana. Kwa sasa tumepata platform kama hii, ambayo tunaweza kuwasilisha maisha halisi ya Mtanzania mtaani. Bila shaka wahusika pia wnapitia humu, na huenda wakaona aibu na kuchukua hatua!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...