Jana katika hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es salaam palifanyika sherehe ya aina yake ambapo iliadhimishwa kufanyika upasuaji wa 200 wa Fistula katika mwaka huu wa 2011, ikiwa imesalia mazoezi 100 ya upasuaji ili kutimia azma ya kuwakufanyika upasuaji 300 kama lilivyo lengo la hospitali hiyo kwa mwaka huu. Mwaka 2009 kulikuwa na upasuaji 162 tu, hivyo ndio kusema lengo ni kuongeza asilimia takriban 50 kwa mwaka huu, na kwa jinsi mambo yanavyokwenda hilo linawezekana kabisa kutokana na kampeni kabambe inayoendela, ikiwa ni pamoja na kutumika mpango maalumu wa Vodacom M-Pesa unaohamasisha wagonjwa kuletwa CCBRT hata kama hawana uwezo.
Kwenye sherehe hizo Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Erwin Telemans (pichani juu) alitoa hotuba fupi ya kusifia na kupongeza wafanyakazi na wafadhili, kabla ya Naibu Mkurugenzi wa CCBRT Bw. Tom Vanneste kuonesha mafanikio hayo makubwa kwa njia ya video na kushuhudiwa na wawakilishi kutoka Vodacom, AMREF, na taasisi ya Women's Dignity ambaop wote ni wafadhili wa mradi wa kutokomeza Fistula.
Baadaye sherehe zikahamia kwenye wadi ya Fistula ambako wakinamama wanaohudimwa hapo CCBRT waliimba kwa furaha kuhusu ugonjwa wa Fistula ambao unatibika bure hapo hospitali na kushukuru kwa huduma inayotolewa kwao.
Naibu Mkurugenzi wa CCBRT Bw. Tom Vanneste (shoto) na wafanyakazi wa CCBRT wakisikiliza hotuba
Wageni wakitembezwa katika wadi ya Fistula
Kinamama waliolazwa katika wadi ya Fistula wakiimba kwa furaha kusherehekea upasuaji wa 200
Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Bw. Erwin Telemans akiongea na wafanyakazi na wageni toka Vodacom na AMREF
Pamoja na kuwepo sherehe lakini huduma ziliendelea kutolewa kama kawaida.
Kwa habari zaidi na mawasiliano na CCBRT
Tel: +255 (0) 22 260 1543
Fax: +255 (0) 22 260 1544
Email: pennie.cabot@ccbrt. or.tz
Web: www.ccbrt.or.tz
www. baobabhospital.or.tz
Kwa habari zaidi na mawasiliano na CCBRT
Tel: +255 (0) 22 260 1543
Fax: +255 (0) 22 260 1544
Email: pennie.cabot@ccbrt.
Web: www.ccbrt.or.tz
www.


Wadau Fistula ni ugonjwa gani?
ReplyDeleteHuu ni ukombozi mkubwa kwa akina mama. Nawapa hongera kwa wote wanaofanikisha zoezi hili kwa bidii kubwa.
ReplyDeleteMungu atawasaidia na kuwapa mafanikio zaidi.
Wewe anony namnba mbili tunauliza fistula ni ugonjwa gani? Usituyeyushe.
ReplyDelete