Habari toka Bungeni sasa hivi zinasema Rais Jakaya Kikwete ameamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Bw David Jairo asiendelee na kazi hadi hapo baada ya uchunguzi dhidi yake wa kuchangisha pesa ili Bajeti ya wizara yake ipite ukamilike.

Hayo yamesemwa sasa hivi na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda wakati akijibu swali la papo kwa hapo toka kwa Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe, ambaye alitaka kujua kama Bw. Jairo ataendelea kuwa likizo ili kupisha mchakato wa uchunguzi huo utaofanywa na kamati teule ya Bunge.

"Jambo hilo limekwisha fanya Mheshimiwa Rais", alijibu Mh Pinda kwa utulivu na kwa kifupi baada ya swali hilo, huku wabunge wakishangilia kwa kugonga meza.

Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Bw. Jairo kuripoti ofisini kwa shangwe, ambapo wafanyakazi wa wizara walimpokea kwa vifijo, na wengine hata kusukuma gari lake hadi ofisini, aliporipoti mapema asubuhi.

Uamuzi wa kumrejesha kazini Bw Jairo ulipokewa kwa husia tofauti na kila kada nchini, wengi wakihoji sababu ya mhimili mmoja kati ya mitatu iliyopo (Serikali, Bunge na Mahakama) kuingilia mwingine, ikizingatiwa kamba sakata hilo liilianzia bungeni na wengi walihisi ingekuwa vyema Bunge lingelishughulikia hadi mwisho.

Bunge lililidhia kuundwa kwa kamati maalumu kuchunguza tuhuma hizo na inategemewa wajumbe wake watatangazwa kesho wakati wa kufunga kikao cha Bunge kinachoendelea sasa. Ripoti yake inategemewa kutolewa Bunge lijalo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Atleast now we know that someone is not sleeping!

    ReplyDelete
  2. GöttingenAugust 25, 2011

    Angalau nimepumua kidogo. Sikuweza yavumilia matusi ya Luhanjo kwa kuruhusu kodi yangu kuchezewa na kufanya mbwembwezao za jana. Nafikiri ameshachoka madaraka maana imefikia anaendesha serikali kama familia yake. Pia CAG atueleze hilo fungu la kufanya lobbing ili bajeti ipite lilipitishwa na bunge gani. Huwezi kusema mtu hana hatia eti kwasababu kiwango cha ubadhilifu kimeonekana ni tofauti na kilichowasilishwa mwanzo.

    ReplyDelete
  3. Nina maoni ya aina mbili:
    1. Inawezekana Jairo asiwe na kosa kwani atakuwa amefuata kanuni, taratibu na sheria za Wizara yake katika kuchangisha fedha. Kama ni hivyo, makosa yapo kwenye hizo sheria. Zinahitaji kupitiwa upya na kubadilishwa.

    2. Ni vizuri wananchi tukaelimishwa ni shughuli gani zinafanyika kwenye kupitisha bajeti tu hadi kugharimu shilingi milioni mia tano (mil 500) na ni akina nani wanhusika kufanya hizo shughuli? (Mil 500 ni kwa vile baadhi ya idara hazikuchanga. ina maana kama idara zote zilizotakiwa kuchanga zingechanga basi zingetumika sh bilioni 1.2). Kama shughuli hizo ni "genuine" ni kwa nini zisiingizwe kwenye vitabu vya bajeti ili zijadiliwe bungeni na badala yake zinachangishiwa pesa pembeni?

    3. Idara zinapochangishwa fedha zinatumia bajeti ipi au vyanzo gani vya mapato wakati nazo zinaomba fedha serikalini? In maana wanaomba fedha ambazo hazina matumizi ndio maana wanapata za kuchngia kupitisha bajeti.

    KUMEKUWEPO NA UFISADI WA KUTUMIA SHERIA AMBAPO WATU WACAHACHE HUTUMIA SHERIA HIZO KUJITAJIRISHA KWA KODI ZA WANANACHI NDIO MAANA INAKUWA VIGUMU SANA KUWAPATA NA HATIA WAHUSIKA PINDI WANAPOBAINIKA. JAMBO HILI LINATAKIWA LIKOMESHWE MARA MOJA KAMA SERIKALI INATAKA KUJISAFISHA MACHONO MWA WANANCHI WAKE.

    ReplyDelete
  4. HATUNA IMANI NA CAG!!! YAANI ANASEMA HAKUNA MAKOSA? HAINGII AKILINI KUSIKIA MILIONI 500 ZIMETUMIKA KUPITISHA BAJETI TU.

    JAIRO ANAWEZA ASIWE NA MAKOSA KAMA KUNA SHERIA INAYOMPA MAMLAKA YA KUCHANGISHA FEDHA. LAKINI HATA KAMA FEDHA ZIMECHANGISHWA HAINA MAANA ZITUMIKE TU KIHOLELA. HAZIKUCHANGWA KUTOKA MIFUKONI MWA WATU BINAFSI. NI ZILEZILE ZILIZOTOKA HAZINA. UHALALI WA HIZO SHUGHULI ZILIZOGHARIMU MAMILIONI YA PESA KATIKA KUPITISHA BAJETI TU UKO WAPI? HAYA NDIO MAMBO CAG ALITAKIWA KUBAINISHA.

    HATA LUHANJO HATUNA IMANI NAYE. ANASEMA WAFANYAKAZI WASITOE SIRI ZA SERIKALI? KWANI SERIKALI NI MALAIKA? KAMA MMEANZISHA POLISI-JAMII HUKU MITAANI KWA NINI KUSIWEPO NA POLISI-JAMII HUKO KAZINI? KAMA WANANCHI WAMEPEWA MAMLAKA YA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU POLISI VILEVILE WAFANYAKAZI WARUHUSIWE KUTOA TAARIFA KWENYE VYOMBO HUSIKA PALE WANAPOONA MAMBO HUKO OFISINI YANAPINDISHWA. WAFANYAKAZI WANA HAKI YA KULINDA RASILIMALI ZETU ILI ZINUFAISHE WATANZANIA WOTE.

    ReplyDelete
  5. Serikali inatuchanganya sana jamani.
    Walishusha bei ya mafuta alafu ghafla wakapandisha.
    Wamemrudisha kazini Jairo, sasa ghafla wanamsimamisha tena.
    Nadhani watawala wamechoka, wanahitaji mapumziko 2015.

    ReplyDelete
  6. Naomba kama Edward M.Sokoine angelikuwepo hadi leo,haya mambo ya usanii yasingelikuwepo, nadhani kila mmoja angenyooka na kuwa mwadilifu.
    Naomba pia turudishe Uhujumu Uchumi kwa mara nyingine na tuanze na viongozi wetu.
    Hili suala limekuwa kama mchezo vile ,waziri mkuu kakemea na mwingine anoana eti hakuna hatia,tabia chafu zimezidi kwenye wizara ndio maana hakuna maendeleo ,hata tukibebwa vipi hatubebeki.
    nashindwa kutofautisha walioenda shule na wasioenda ,maana vitu vingine havihitaji Rocket Science kuamua.
    Eti wafanya kazi walisherehekea kurudishwa mtu aliyekuwa tayari na kashfa,inaonyesha ni jinsi gani kuna uozo kwenye wizara,kuanzia wafagizi hadi wenye vyeo vya juu.

    ReplyDelete
  7. Watumishi serikalini oyeeeeee .Utouh atakuwa akitusafisha tukipga panga serikalini.....hahahahahahahah wazee leo mmechemka

    ReplyDelete
  8. katika yoooooooooooooooooooooooooooooooooote, nimewadharau sana wafanyakazi wa hiyo wizara. Hasa wale waliokuwa wakisukuma gari. Mngageuka tuone sura zetu. Pambafffffffffffffffffffffffffffff. Nawe Jairo si ujiuzuru tuuu. Aibu ishakupata. Najua serikali inaogopa dam changa mana wanajua tutaiendesha nchi kisasa.

    ReplyDelete
  9. MUNGU inusuru nchi yangu ya tanzania mikononi mwa watu wasiokuwa na huruma kwa maskini wanaoishi kwa dola moja....TUNA KAZI YA KUJIBU MBELE YA MUNGU DAHH INAUMA SANA ....iko wapi future ya kizazi kinachokuja jamani
    MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  10. Siyo siri nammiss Lowassa!!

    ReplyDelete
  11. Mussa AllyAugust 25, 2011

    Serikali hii ni butu na haijali wananchi wake. Kuna udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa nchi, hasa kiongozi mkuu. Amekuwa si thabiti katika kufanya maamuzi ya kuinusuru nchi yetu isiyumbishwe na wabaka uchumi badala yake amekuwa ni mtu wa 'kuwabeba viongozi dhaifu na wasio na tija'.

    Eeh Mwenyezi Mungu tusogeze haraka 2015, wananchi tufanye maamuzi mazito.

    ReplyDelete
  12. CAG achunguzwe. Inawqezekana ni swahiba mkubwa wa Jairo.

    ReplyDelete
  13. Nimefurahishwa na maoni ya mdau mmoja hapo juu. "Bajeti inapitishwa kwa mamilioni ya pesa, kuna nini kikubwa kinachofanyika kwenye kupitisha hiyo bajeti"? Mtu mwenye akili hawezi kukubaliana na matusi kama haya, ila wadanganyika ndio wanaokubali.

    ReplyDelete
  14. Hii tabia ya wananchi kumpokea Jairo kama shujaa ni ya kukemewa kabisa. Ina maana bunge ni wajinga waliofanya akasimamishwa? Ina maana ilikuwa ni vita kati ya Jairo na bunge kasi kwamba sasa ameshinda hivyo watu wanampongeza kwa ujasiri? Ni unafiki uliokithiri. Na kama sio unafiki, basi hiyo wizara wote waliomshangilia jairo ni mafisadi.

    ReplyDelete
  15. Mimi sina tatizo na Jairo. Hasira yangu ipo kwenye sheria zilizomruhusu kuchangisha fedha. Nasema ni sheria kwa sababu ingelikuwa ni Jairo kajitungia, Ngeleja asingekubali. Na kama si sheria zilizotumika kuchangisha fedha, basi hata Ngeleja anahusika. Achukuliwe hatua.

    ReplyDelete
  16. Hiyo waizara walijifanya smart sana wakifikiri kwamba pesa za kuchangisha hazikaguliwi. Zingekuwa zimechangishwa toka mifukoni mwao pengine wasingeulizwa. Za mwivi ni arobaini. Wamefanya ujanja huu miaka nenda rudi sasa wamebainika. Shujaa wetu ni huyo mtumishi aliyetoa siri. Big up sana. Una uzalendo na nchi. Endelea kuwa na ujasiri huo huo hadi viongozi wa nchi hii watakaponyooka.

    ReplyDelete
  17. Kwa kweli hiki ni kipimo cha kutokuweza kazi kwa Luhanjo ni vyema Rais umuliona hili maana tulianza kukosa imani na serikali yako bora kwa hili angalau wananchi wamepumua kidogo.Naomba umwonye huyu Luhanjo asifanye kazi kama yeye ndiye Rais wa nchi.

    ReplyDelete
  18. THIS IS VERY ENCOURAGING KWAMBA AT LEAST TUNA RAIS, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WANYONGE WAKE, AMEN

    ReplyDelete
  19. Kumbe ina maana hawa wenzetu hela za bajeti hazikuwako ila za kupongezana zilikuwako kwa kweli hawa mawaziri wanampa Waziri mkuu wakati mgumu sana. Wanapanga hela kama arusi vile sipati picha kama mhazina wa wizara anaweza kukaa na hela kiasi kikubwa kiasi hiki wakitumbua zinazobaki ndipo wanazirudisha na hapa hatuna uhakika kama kweli walizirudisha. Wafanyakazi hawa wana haki ya kumsukuma katibu maana wanayotendewa ni mazuri sana maana wanadiriki kugawana fedha za Wizara wana haki hata kumnunulia mataji ya maua na kumbeba.

    ReplyDelete
  20. Kimsingi Viongozi wakuu wa nchi hawana uzalendo na wanalindana kupita kiasi yani hata mambo ya wazi bado wanalindana sijaona sababu ya waziri wa nishati na madini kukimbia bungeni kuja kumpokea katibu wake inaonyesha anajua kinachondelea.Chamsingi Mh.Raisi apige chini wote kuazia waziri,naibu waziri na katibu mkuu aanze upya uwezo wa waziri wa nishati ni question mark.Tuamke watanzania tusishabikie vyama anayeweza kazi apewe uongozi na si kuangaliana usoni yanayotokea nchi za wenzetu yalianza kama vihi viongozi waogope nguvu ya umma itawaumiza one day.

    ReplyDelete
  21. WOTE WALIO MPOKEA JAIRO KWA SHANGWE NA KUSUKUMA GARI LAKE WAFANYE VIVYO HIVYO WAKATI ANATOKA KU OFISI,,,,NYAMA NYIE!!!

    ReplyDelete
  22. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa, Aliye juu mngojee chini,Subira yavuta heri. TUTAKUTANA IGUNGA

    ReplyDelete
  23. Kwakweli serikali imechoka na inahitaji kupumzishwa mwaka 2015. Haiingii akilini eti zimetumika mil. 500 kwa ajili ya kupitisha bajeti mihela yote hiyo wakati kuna wagonjwa wanalala chini? uzalendo wanaouhubiri viongozi wetu uko wapi? ufujaji wa kodi zetu ndio uzalendo? jamani viongozi waliopo madarakani tumewachoka mbona wao sio wazalendo, tunaomba waachie ngazi mapema kabla hawajaadhirika!

    ReplyDelete
  24. Mbona hatujawahi kusikia bungeni wabunge wakipitsha bajeti kwa ajili ya kupitisha bajeti za wizara? huu utaratibu umeanza lini?

    ReplyDelete
  25. CAG tuambie:
    1. Je ma-katibu wakuu wa kila wizara walichangisha fedha kupitishia bajeti zao? Kama jibu ni ndio tueleze na viwango(vya pesa) vilivyopatikana kwa kila wizara.
    2.Kanuni au sheria inayoruhusu shughuli ya uchangishaji pesa kama wafanyavyo ma-katibi wakuu.
    3. Je, marejesho na ukaguzi hufanyika baada ya matumizi, yaani kupitisha bajeti? Mbona tangu umekuwa CAG, hujawasilisha taarifa ya ukaguzi wako?

    Tafadhali msitufanye tuichukie serikali yetu kwa madudu yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...