Michuzi naomba uniwekee malalamiko yangu kwenye Blog yako ili wahusika waone na waweze kujirekebisha.

Naamini kwamba system ya kulipia Parking iliwekwa ili kuongeza mapato ya jiji na pia kufanya mpangilio mzuri wa kuegesha magari kusiwe na kero barabarani!

Hapa Mwanza hawa jamaa wanaotoza ushuru kwa kweli ni kero kubwa sana kwa sababu,wanafanya kazi kama MAROBOTI...kwanza sehemu nyingi hazina alama za kuonyesha kwamba unaruhusiwa kupaki au lah! hivyo watu wanatumia uzoefu, kwa hiyo sisi wageni tunapata shida sana kujua na kwa bahati mbaya sana, wanakuvizia, wakiona unahangaika wanajificha na ukitoa mguu tu wanakufungia mnyororo-kutoka tena ni lazima ulipe faini ya tsh 50,000/-

Sehemu zingine mfano pale maeneo ya CBE, kuna parking lakini hakuna alama inayoonyesha kwamba unatakiwa upaki kimshazari au kiurefu, ukipaki kiurefu badala ya kimshazari, mambo ni yale yale tena! Na mbaya zaidi wakishakufungia gari yako, hakuna sehemu yoyote unayoweza kulalamika na kupatiwa haki...wanasema ni lazima ulipe kwanza halafu uandike barua kwa mkurugenzi wa jiji kulalamika...hii ni KOMEDI!
Nadhani hawa jamaa wanalipwa kutokana na magari ambayo wanayafunga kwa siku hivyo wanafanya juu chini wapate vichwa!

USHAURI;-Uongozi wwa jiji uboreshe alama za kuelekeza ni wapi kwenye parking na wapi hakuna, na gari lipakiwe vipi.
-Kama hilo haliwezekani basi kila mahali akae mtu anayemwelekeza dereva apaki vipi, sio kujificha mkiona dereva anakosea.
-Mfanye kazi kama binadamu wenye akili, sio kufunga tu minyororo hata kama mmekosea hamkai mkasikiliza maoni ya watu
wengine

Ahsanteni!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Napenda kumuunga mkono huyo mdau alitoa lalamiko la parking ni kweli mi pia napata sana usumbufu nikitaka kupaki gari langu tena ndo mzaliwa wa mwanza je kwa huyo mgeni?tunaomba hili swala lichukuliwe umakoni wa hali ya juu wako mdau.GRACE-MWANZA.

    ReplyDelete
  2. Huo ugonjwa umeingia Dodoma pia tena recently tu. Juzi jinga moja la parking (no offense, ila jamaa jinga kweli) linabishana na dereva aliyekua anamsubiri mwenzake achukue vocha ya airtime pembeni ya kiduka, bila aibu na kwa sauti kubwa likapayuka "Ukishazima gari tu umepaki, kwa hiyo lete hera!"

    ReplyDelete
  3. Watu wa parking na mgambo hakuna tofauti. wote ni njaa tu tuwasamehe bure. Wale ni cheap labour tusitegemee wawe na akili vichwani, ndio maana hata shule iliwagonga. Ila walijaaliwa nguvu...raia kazeni misuri ili tuwe sambamba

    ReplyDelete
  4. Hii ipo na Dar e Salaam pia hasa mjini kati. Wanakwambia ukalipe faini au uwape nusu ya faini! Hivi nchi hii ndiyo ishakua lawless? Umeme shida, Maji Shida, Foleni ndiyo usiseme, pale katikati ya jiji wameweka oneway njia ambazo ni pana, na zile finyu ni two way (ujinga mtupu!). DART inaanza baada ya miaka 50 na ni mradi wa miaka 10 kwa pesa ya zaidi ya mara 3 ya deni la taifa. Maeneo ya wazi wanachukua za waaarabu na wahindi, mbona jengo nyuma ya umoja wa vijana wameiacha? Wanataka kujenga nyumba za ghorofa huko upanga, huku uswahilini kwananini hawataki? Halafu wanasema wanataka wananchi wa hali ya chini wakae humo walipe dola 1000 kwa mwezi kwa mtu ambaye ana kipato cha dola 60 kwa mwezi, ufisadi mtupu! Wanataka watoto wao wakae mjini karibu na kazini kwao!

    ReplyDelete
  5. Mbaya zaidi ni pale wanapotoza parking fees hata siku za sikukuu, sijui hiyo ni ofisi gani. Ukiuliza eti ni pesa ya kuanzia siku ambayo siyo sikukuu. Hiyo ni Mwanza. Nadhani wanatuchakachua!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa hapo juu eh hiyo kali, eti pasa ya kuanzia siku ambayo siyo sikukuu! Ama kweli utapeli umepamba moto tz, kwani siku hiyo isiyokuwa sikukuu si itafika tu?

    ReplyDelete
  7. Mimi wjinga hao walifunga gari pale Salma Cone kisa eti wanasema gari haina risiti za parking za siku zilizopita. Nikawauliza ni sheria gani inamtaka dereva kutunza risiti za parking, wakasema hilo swla niulize mahakama, nikawauliza tena je kama tmu ana shughuli ake nje ya mji, anatoka kwake na kwenda huko ambako hakuna parking fee wakasjindwa kujibu. Basi nikakodi taxi nikawaachia gari. uzuri sikuwa katika wrong parking. Nikawaambia waendelee kulilinda gari mpaka hapo wakiridhika na ulinzi wao. Wakataka shs. 30,000 nikawajibu wakaiombe mahakama. Saa 2 usiku wakainipigia simu nikachukue gari na kuomba msamaha juu. Kiukweli niliwatukana sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...