Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Immam Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Masoud Mohamed Jongo, akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El-Fitr leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. raisi wetu jamani ingewezekana kurudi tena angerudia huyu ndio aliyekuwa raisi wetu wa nguvu na kikwete

    mungu awabariki.

    RIP JKN

    ReplyDelete
  2. Duh! eh bwana eeh... huyu Mzee Ruksa alikuwa mcheza karate au vipi? Anawezaje kukaa mkao huo wakati ana umri wa miaka zaidi ya 85?

    Mnyonge mnyongeni, lakini hiki kibabu kiko fiti kama chuma

    ReplyDelete
  3. edd mubarak kwa wote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...