Maafisa kutoka Wizara ya Sheria na Katiba na Mahakama wakifuatilia hotuba ya Bajeti ikisomwa na Waziri wa Sheria na Katiba Mh Celina Kombani Bungeni Dodoma Jumatano jioni
 Maafisa wa Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na wa Idara ya Mahakama wakifuatilia hotuba
 Waziri wa Sheria na Katiba Mh Celine Kombani akisoma hotuba ya wizara yake bungeni
Maafisa zaidi wa Wizara ya Sheria na Katiba na wa Idara ya Mahakama wakifuatilia hotuba kwa umakini mkubwa
 Ankal na mdau mkubwa wa Globu ya Jamii Bw Jacob Mwambegele wakiwa bungeni
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mh Angela Kagaruki akiongea na mmoja wa maofisa wa Wizara ya sheria na  Katiba baada ya kutoa hoja yake, akitetea maslahi ya wafanyakazi wa Idara ya Mahakama na wizara ya sheria, ambapo kasisitiza kuna haja ya kuongeza bajeti ili taasisi hizo zifanye kazi kwa ufanisi na wafanyakazi wake wafanye kazi kwa ari
 Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto Mh. Sofia Simba akiongea na Naibu waziri wa Kazi na Ajira Mh Milton Makongoro huku Mbunge wa Kigoma Mjini Mh Peter Serukamba (shoto)  na Mbunge wa viti maalumu Mh Al- Shaymar Kwegyir wakisikiliza
 Mbunge wa Pangani Mh. Saleh Pamba akiongea na Mbunge wa Viti Maalum Mh Zakhia Meghji
 Mwenyekiti wa CHADEMA, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na pia Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akibadilishana mawazo na Waziri wa Sheria na Katiba Mh Celine Kombani na Msajili wa Mahakama ya Rufani Mh Francis Mutungi baada ya waziri kusoma bajeti yake Jumatano jioni
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Ummy Ali Mwalimu (shoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalum Mh.  Al- Shaymar Kwegyir 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mh.Ummi mwalimu ametulia sio mchezo,nahisi pia na ifisini yupo hivyo.

    ReplyDelete
  2. Hivi zile kesi za bongo zinazochukua miaka mingi zitaisha lini?
    Maana najua kuna kesi ya jamaa yangu inahusisha ofisi ya kigogo mmoja mstaafu, wafanya kazi wa huyo kigogo wamekubali kosa la upotevu wa mali mikononi mwao na ushahidi upo, lakini mpaka leo hii jamaa hajalipwa, kesi inaahirishwa kila siku na jamaa wa huyo kigogo hawatokei mahakamani.
    Viongozi wengi wanaijua hii kesi lakini wanaifumbia macho kwa ajili mnamhusu rafiki yao.
    Hakuna haki za kisheria kabisa bongo sio mahakama wala polisi, na unaweza kuwa maskini siku moja tu wakaiamua kukufanyia na hakuna pa kukimbilia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...