Uncle nipo US kwaajili ya International visitor leadership program,promoting social change through the Art. washiriki tupo 21 toka nchi mbalimbali mpaka tumetingisha nchi,tumefika tu Washington bonge la "EATH QUAKE" likatokea ambalo halijawahi kutokea kwamiaka 40,hahaaa!

Siku chache tumekuja New york, toka jana jumamosi na leo jumapili tunaambiwa tusitoke nje sababu ya" HURRICANE IRENE"nayo haijatokea kwa miaka mingi pia.(kama ningeandika msahafu ingekua..Amin amin nawaambia, wasanii walipoingia, nchi ya babeli ilitetemeka vimbunga na mvua za mafuriko zika ifunika nchi...nk.)

Jumatano nitaelekea North carolina ambako watu watano wamefariki Dunia kwa kimbunga, Mwishoni tutakuwa Hawai Honolulu .Tuombeeni salama kwani ni SANAA tu ndio itaweza kumkomboa mwanadamu, inaunganisha watu pasi kujali tofauti zetu.

Sanam ya Martin Luther king ambayo ilifunguliwa kwa public wiki iliyopita, Baadhi ya magazeti yamealiandika sanamu imeleta mitazamo tofauti kwa baadhi ya watu. moja, kwanini imechongwa kwenye jiwe jeupe na yeye ni mweusi?

Pili kubwa, kwanini hakupewa hiyo kazi ya kuumba sanamu mtu mwesi, badala yake akapewa mchina.Sanamu hii imegharimu milioni moja na arobaini na ushee PESA ZA KIMAREKANI.

Kwa jicho langu la usanii kweli ukiangalia kuna UCHINA UCHINAfulani hivi, msanii sikuzote akifanya kazi ya kuumba au kuchora inasemekana kuna asilimia ya muendelezo wa kujinukuu mwenyewe,(multiplying your own image)kwani umezoea kuona ndugu zako wa karibu unao fanana nao na kujiona mwenyewe tokea utotoni,ndio lililomtokea ndugu yetu msanii wa kichina.

Lakini haizuii umati mkubwa kwenda kuona sanamu hii.
Huu ndio mfano mzuri wa kuleta mabadiliko katika jamii kupitia sanaa.Najiuliza kungekuwa na badiliko gani kama ingetengenezwa na mtu mweusi na jiwe jeusi! LABDA WADAU TUSAIDIANE.!
Wadau wakiangalia na kuiga picha sanamu ya Martin Luther King Jr.
Mdau Paul Ndunguru akitalii mitaani.
Picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mabeberu ndivyo walivyo. Hakuna walifanyalo kwa watu wengine bila hila.

    ReplyDelete
  2. Haswa. Hila, kejeli, dharau na ubinafsi ndiyo zao. Sisi tukitangeneza ya Mwalimu tutaleta mtaalamu toka Mtwara, poa. Uwe na ziara ya amani.

    ReplyDelete
  3. Unapendekeza kazi hiyo angepewa Pacha wake? Maana tofauti zingeendelea kuwaepo! weusi, urefu, unene, jimbo analotoka, historia yake akama naye alitoka katika familia ya wapigania haki nk. Wenzetu wamechagua nani ana uwezo wa kufanya kazi hiyo, sio nani mweusi zaidi afanye kazi hiyo! Na mafanikio unayaone katika Nyomi la watu wanaofika hapo kuliangalia.

    Hebu angalia lile Sanamu la Mwalimu pale Mwanza, Linafanana na nani?

    ReplyDelete
  4. WEEEE WANIRUBUNII, WAKIWANUNA, WAMNUNIANANI KATATEEEEEEE, HAHAHAHAHA. Naona Kiumbe, unatembeza jicho lililo enda shule kwenye makazi ya wababe. lol. Hasante sana kwa kutuhabarisha mambo muhumu na matamu kama haya.Six

    ReplyDelete
  5. Naomba kuwa tofauti kidogo,na maoni ya wadau wenzangu. sidhani kama nimfumo wa kibepari,bwana Paulo Ndunguru,kasema/kaeleza vizuri kabisa kuhusu athari za ufinyazi/uchongaji vinavyo athiriwa na msanii yeye mwenyewe. Tumezowea,na nimazoea yetu kutoruhusu mitazamo,na ubunifu vitawale katika kazi zetu.ingekuwa mweusi kapewa tusinge jifunza kitu zaidi ya kuiangalia sanamu hiyo katika ukawaida wake usio leta udadisi,na hii ndiyo sanaa. hongera ,Paulo(zamani mzee wa manyaninani) Kaka S.

    ReplyDelete
  6. naona umenunua pc yako ya macntosh hapo ....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...