Mshambuliaji wa timu ya shule ya sekondari ya Katenge iliyopo mkoani Njombe, Majura Mlola akijaribu kuupiga mpira katikati ya mchezaji wa timu ya shule ya Wanging'ombe katika mchezo wa kirafiki uliochezwa shuleni hapo. Katenge ilishinda bao 2-0
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Katenge iliyopo mkoani njombe wakishangilia ushindi wa timu yao mara baada ya kuinyuka mabao 2-0 timu ya shule ya sekondari ya Wanging'ombe,mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya wanging'ombe mkoani Njombe
Wadau kutoka mkoani Arusha, Danford Mpumilwa(shoto) na Evance Mkonyi wakishuhudia mechi baina ya timu za shule za sekondari za Wanging'ombe na Katenge katika uwanja wa shule ya wanging"ombe. Wadau wako vekesheni Njombe. Picha na Mosses Mashalla


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...