Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Heko wazee, simamieni haki na kamwe msifanye kazi kwa hisia. Tunajua kuna kinyonga anabadilika badilika lakini ninyi simamieni haki.

    ReplyDelete
  2. ingawaje michuzi umekuwa ukiyaminya maoni yangu karibu yote lakini naomba niseme tu yote yanayofanyika hapa ni show tu lakini sterling wa hii move yote ni JK akijaribu kumuokoa rafiki yake kipenzi kwani huwezi kuchangisha mamilioni yote haya kihalali bila waziri mkuu ambaye wizara zote ziko chini yake kutokujua, it does not make sense.

    ReplyDelete
  3. Inawezekana sisi wananchi hatujui mengi yanayotendeka na kuendelea bungeni kuhusu mambo ya pesa zetu zinavyotumika.
    Ni miaka mingi sana palikuwa na siri kubwa ndani ya bunge ktk kupitisha bajeti za wizara,leo mungu anatuonyesha na bado tutaonyeshwa zaidi, na wote wanaofanya mambo kinyume cha sheria au kuitumia sheria kwa wanavyojua wao basi malipo yapo hapa duniani.
    Inatia hasira sana jinsi mwananchi anavyoteseka ktk nchi yake na huku viongozi hawana hata uchungu na pesa kidogo ya serikali iliyopo.

    ReplyDelete
  4. Mbona waziri mkuu alisema kama angekuwa na uwezo angalimfukuza kazi siku ileile.
    Hii ina maana kuwa 95% ya tuhuma ni ya ukweli,ila sasa kuna hii kitu ya kupindisha sheria , hata kama kuna makosa kuna jinsi ya kuliweka kosa na kuwa hali ya kawaida.
    Hatutaendelea kamwe,tutaishia kuomba misaada kwa wazungu kila siku.Hali pesa kama hii ingefaa kupunguza matatizo ya wananchi.

    ReplyDelete
  5. Taarifa ni nzuri na inashawishi kuwa Jairo hana kosa. Lakini, kwa nini taarifa ya mkaguzi ilipofika kwa Luhanjo, haikupelekwa kwa raisi ikajadiliwa na maamuzi yakafikiwa kwa pamoja ili kuepuka mkanganyiko. Luhanjo anaamuru Jairo arejee kazini wakati huohuo raisi anasema aendelee na Likizo. Jambo hili lisingetokea kama mngejadiliana hiyo taarifa na mkafikia maamuzi ya pamoja.

    Jambolingine ambalo linatutaiza sisi wananchi ni uhalali wa matumizi ya pesa nyingi hivyo katika kupitisha bajeti!! Hili hasa ndilo linaloleta mashaka kwamba huenda kuna ufisadi kwenye hicho kinachoitwa "kupitisha bajeti". Na zaidi ya hayo kama huo upitishaji wa bajeti ni shughuli inayokubalika kisheria, kwa nini isiombewe pesa kupitia kwenye mfumo wa kawaida wa bajeti ambayo inajadiliwa bungeni na kupitishwa? Kwa nini pesa nyingi hivyo zifanye kuchangishwa? Je hizo idara zinazochangishwa fedha nyingi kama hizo zinatoa wapi pesa za ziada ili kuweza kuchangia? Hapa kuna uwezekano idara zikawa zinaomba pesa kwa kutumia bajeti hewa ili zibaki zielekezwe kwenye mambo mnayoyajua ninyi kwa njia hiyo ya michango.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...