Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Msingi Mchuchuma wilaya ya Ludewa mkoani Iringa Bw.Joseph Thomas Lugome (58) akionyesha darasa la saba ambalo limekuwa likisomewa pia na wanafunzi wa darasa la sita kwa kupokezana na darasa la saba kutokana na shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 200 kuwa na walimu wawili pekee
Na Francis Godwin(TGNP),Ludewa
SHULE ya msingi Mchuchuma katika wilaya ya Ludewa mkoani Iringa yenye wanafunzi 208 wakiwemo wanafunzi wasichana 90 na wavulana 118 imekuwa ikifundishwa na mkuu wa shule na makamu mkuu wa shule pekee ambao wote ni wanaume .
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari za mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP ) mkoani Iringa umebaini kuwepo kwa hali hiyo ambayo pia imekuwa ikiwapa wakati mgumu walimu hao hasa pindi wanafunzi wa kike wanapougua na kuhitaji msaada wa kupelekwa katika matibabu .
Hata hivyo kutokana na upungufu mkubwa wa walimu katika shule hiyo ambayo inaelezwa kujengwa juu ya madini ya mchuchuma na linganga ,umekuwa ukikwamisha kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo na kupelekea baadhi ya watoto kuacha shule kwa kutokana na kukosa walimu wa kuwafundisha .
Mmoja kati ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo Augustino Haule alisema kuwa kwa upande wake alikuwa na watoto wawili waliokuwa wakisoma katika shule hiyo ila mmoja wa kike ambaye alikuwa darasa la saba amelazimika kumwachisha shule baada ya muda mwingi kushida mitaani baada ya walimu kutofundisha mara kwa mara.
Haule alisema kuwa mbali ya walimu kuwa wachache katika shule hiyo ila bado mazingira ya shule hiyo yamekuwa yakichangia watoto kuacha shule kutokana na muda mwingi kufanya kazi za kupika na kuchota maji ya walimu umbali wa zaidi ya kilomita 2 kutoka katika shule hiyo.
Pia alisema kuwa ni vema serikali kuifunga kabisa shule hiyo hadi pale itakapolipatia ufumbuzi tatizo la upungufu wa walimu kuliko serikali kuendelea kuwaacha wanafunzi zaidi ya 200 kufundishwa na walimu wawili pekee tena wote wakiwa ni wanaume.
Mwalimu mkuu mssaidizi wa shule hiyo Joseph Lugome alithibitisha uhaba huo wa walimu katika shule hiyo na kuwa hadi sasa kwa zaidi ya wiki mbili mwalimu amebaki peke yake baada ya mwenzake kupata matatizo ya kiafya.
Alisema kuwa katika shule hiyo wanafunzi 47 ni darasa la saba ambao wanangoja kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi na kati ya wanafunzi hao wasichana ni 24 na wavulana ni 25 huku wanafunzi wa darasa la nne katika shule hiyo ni 10 pekee wasichana wakiwa 11 na wavulana 8.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na shule hiyo kutokuwa na maji wanafunzi wamekuwa wakipagiwa zamu ya kuchota maji ya walimu umbali wa kilomita zaidi ya 2 kutoka katika shule hiyo ili kutoka nafasi ya walimu kufundisha wanafunzi wengine .
Kwani alisema kuwa iwapo walimu wataondoka na kwenda kutafuta maji basi upo uwezekano wa wanafunzi kuendelea kukosa vipindi .
Lugome alisema kuwa wakati mwingine shule hiyo imekuwa ikifungwa kwa muda iwapo wanafunzi zaidi ya mmoja wataugua na walimu hao kufanya kazi ya kuwabeba mgongoni wanafunzi hao wagonjwa na kuwapeleka zahanati iliyopo kijiji cha jirani kilichopo umbali wa zaidi ya kilometa zaidi ya 12 kijiji cha Nkomang'ombe.
Pamoja na mazingira hayo ya kufundisha yakiwa magumu bado mwaka jana shule hiyo darasa la saba ambalo lilikuwa na wanafunzi 36 wanafunzi 8 walifaulu kujiunga na elimu ya sekondari.
Aidha alisema kuwa mbinu za ufundishaji ambazo zimekuwa zikitumiwa katika shule hiyo yenye walimu wawili ni pamoja na kuunganisha madarasa kwa kufanya darasa la kwanza na la pili ndani ya chumba kimoja na darasa la tatu na la nne kuwa ndani ya darasa moja na darasa la sita wamekuwa wakisoma kwa kupokezana na wale wa darasa la saba.
Mwalimu Lugome alisema kuwa tatizo la utoro kwa wanafunzi limekuwa ni sugu kwa kipindi cha masika zaidi kutokana na wanafunzi kutoka mbali na shule hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 2 na kuwa kutokana na mvua na mito kujaa maji wa wanafunzi ambao wamekuwa wakifika shule ni 100 ama 90 pekee na sehemu kubwa hushindwa kufika shule.
Afisa elimu wa wilaya ya Ludewa Robart Hyella amethibitisha kuwepo kwa tatizo la uhaba wa walimu katika shule za msingi ndani ya wilaya hiyo na kuwa shule zinazoongoza kwa upungufu wa walimu ni zile za pembezoni mwa wilaya hiyo .
kwa kweli hawa waalimu wawili wanahitaji wapewe bonus ya nguvu, tena ya kujengewa nyumba ya kuishi manake umri wao tayari umekwenda na bado wanaona umuhimu wa watoto kupata elimu, hivi wizara ya elimu inajua kuwa ina waalimu wa ngapi? na ina upungufu wa waalimu wangapi? sidhani hata mbunge wa eneo hilo anajua hili,wahusika tunaomba mfanye mtakavyoweza kusaidia hii shule, please!!!!!!!!
ReplyDeleteHaya Jamani wana Ludewa muanze na baiskeli mbili za walimu baada ya hapo mchangia mshahara wa walimu wapya... Onyesheni Utanzania wenu
ReplyDeleteWe have a long way to go, wa Tanzania wenzangu. Hizi story nilikuwa nazisikia toka kwa wazazi wangu enzi zao za shule. 2 generations later bado tuna hili tatizo, tena baada ya miaka 50 ya "Uhuru". Uhuru gani huu? Unaweza kuhalalisha kweli mishahara ya viongozi wakati wananchi wanaishi hivi? Sasa hao watoto, do they even stand a chance in the 21st century bila basic primary education? Tunapokwenda si pazuri. More investment in the education sector please.The children of today are the leaders of tomorrow.
ReplyDeleteKuna Black mmoja USA alianzisha chuo kikuu na akawa lecturer pekee yake. Anaitwa Booker T Washington. Hiyo ya kuwa shule ya msingi ina walimu wawili sio ajabu. Chapa kazi, somesha wanaohudhuria, wasiohudhuria wapeni ueliwa wa umuhimu wa elimu kwa maisha yao na wanakijiji wenzao. Acheni kusikiliza wanamapinduzi maana lengo leo ni choyo tu hakuna zaidi. Hizo nchi mnazosikia zina maisha mazuri hawakulala usiku na kuamka asubuhi wakakuta mali. Historia mnaijua. Kuna wenzenu wanakudanganyeni ati watakuleteeni maendeleo. Huwezi kupata maendeleo kwa kusimama kwenye viriri. Ili nchi itajirike wengine lazima watu wafe kwa kufanya kazi na wengine wapate vilema vya maisha.
ReplyDeleteDUH, TICHA TU ANATIA HURUMA...maskini mwal. pole ndugu...ndo maana walimu wanaenda kufundisha mijini tu...ukiambiwa ni Tanzania hii hii huwezi amini!!
ReplyDeleteHmmm yaani nimesoma mpaka nacheke kwa kusikitika, jamaani hapo kuna Elimu au ndio michosho tu. mmmm mpaka wanafundi wenyewe wameshagundua yakua wanapoteza muda tu hapo. Hmna lolote
ReplyDeletesasa mheshimiwa DEO anayajia hayo????????????????????
ReplyDeleteHabari inasema darasa lina wanafunzi 10, wakiume 11 na wa kike 8. Pia inasema kuwa walimu ni wawili tu lakini wanafunzi wanaacha shule kwa sababu wamechoka kuwachotea walimu wao maji. Kuna ubaya gani kwa wanafunzi kuwachotea na kuwapikia walimu wawili tu, ili hao walimu watumie muda mwing kuafundisha? mwandishi kabla kutuma habari kama hizi ujue kuna watu watasoma kila unachoandika kwa hiyo kuwa makini.
ReplyDeletehii tanzania haina maana tufe wote tuu khaaaaa ndio nini mwalimu anateseka kiasi hiki jaman,walimu hawapewi mishahara ON TIME isitoshe wanaonewa unakuta mtu wa anachukua mshahara wa mwalimu aliekufa miaka mingi,hiyo ipo na tunaijua kabisa hao viongozi hawatoi taarifa hao ni kula mishahara ya walimu ambao wameshakufa kuna rafiki yangu mwalimu ndio alikuwa akilalamika hivi tutanyanyasika mpaka lini umeme ndio huo maisha magumu,watu wanakula nchi taratibu wengine twateseka subirini 2015
ReplyDeleteInashangaza kwa kiasi kikubwa hasa tunapoona mipango mingi na mikubwa ya kuboresha elimu ikipita bila kunufaisha walengwa kwa kiwango ridhishi. Tulikuwa na MMEM, MMES, MKUKUTA, MKURABITA n.k. mipango yote hii inagusa maendeleo ya kiuchumi. Je funds huwazinaishia kwenye tathmini na kuandika riport za mezani? Imefika wakati tusimame kwa miguu yetu na tupange na kufanya kazi kwa kusugua akili zetu wenyewe. Miaka 50 iliyopita, nchi yetu ilikuwa sawa kiuchumi na eastern tigers, tumejiloga wenyewe kwa kuendekeza misaada mpaka leo miaka 50 baadaye ni least developing country wakati wenzetu tayari ni medium developing.
ReplyDeleteNawapongeza hawa walimu wawili kwa juhudi zao katika kulikomboa taifa letu kielimu. Ni wakati muafaka kujifikiria upya namna ya kutathimini ubora wa watawala wetu katika maendeleo ya kiuchumi ambayo mguso wake unaonekana katika jamii na siyo propaganda za bank kuu na hazina.
Jamani Ludewa mbona mbali sana, njooni huku Mkuranga mtayakuta haya! Enhe, hii ndio "education for the future generations". Tuliosoma shule za upe tuu nchi bado inatusumbia, sembuse hawa? Kazi ipo!
ReplyDelete1. Nasema hivi, kwanini walimu kama hawa wasiwerecognized kama HEROES! Wanajitolea kwa juhudi zao zote na si ajabu hata mishahara haifiki wakati muafaka!
ReplyDelete2. Kama hii ni shule ya serikali, wizara yetu tukufu ya elimu ina habari hizi au na wao wanazisoma toka kwenye blog kama sisi?!
3. I am speechless!!