Mwili wa mmoja wa watu walaiokutwa chumba Na. 425 hoteli ya Southern sun jijini Dar
ukitolewa nje ya hoteli kupelekwa garini.

ULEVI wa kupita kiasi unaaminika kumuua raia mmoja wa Zambia na wengine watatu akiwamo Mtanzania, kubaki hoi na mmoja kuzindukia Muhimbili wakiwa katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

Watu hao wanne ambao wote ni wanaume walikutwa katika chumba namba 425 ghorofa ya nne, kinachodaiwa kukodishwa na raia wa Kiingereza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha tukio hilo na kusema wanaendelea na uchunguzi.

Aliyezinduka Muhimbili ni Eliud Sikwabi ambaye ni Muingereza na kuwataja wenzake kuwa ni Ikbar Bahabur wa Zambia na Mtanzania aliyetajwa kwa jina moja la Omari.
Kamanda Shilogile alisema inaonekana kuwa watu hao walikunywa kupita kiasi. Taarifa zaidi zinasema kwamba watu walianza kunywa katika sherehe ya harusi ya mtoto wa Jaji Mark Bomani, Clement.
Mwili ukipakiwa katika gari la wagonjwa tayari kupelekwa hospitali.
Wapelelezi wakiwa kazini kukusanya vielelezo kwa ajili ya uchunguzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. HangOva 3 Gonneeee Wroooong!!

    ReplyDelete
  2. Na huyo Risepshenist na e matatani huyo.

    Aliruhusuje watu wa 4 wa jinsia moja wote kulala kwenye chumba kimoja?

    Ulevi jamani Nomaa!

    ReplyDelete
  3. FUNDA MOJA LA ZIADA LIMEWAUMBUA

    ReplyDelete
  4. kweli wewe zero brain eti ''aliruhusuje wa4 wa jinsia moja kulala kwenye chumba kimoja?''............na wewe muingereza huna akili yaani baada ya kula box lako ukaamua kwenda kumaliza viji pound vyako bongo.

    ReplyDelete
  5. DUH RAIA WATATU TOFAUTI KULIKUA NA BONGE LA DILI HAPO LINATAKA KUCHEZWA

    ReplyDelete
  6. Dar kuna CSI bomngo tambarare si mmeona waungwana?

    ReplyDelete
  7. Nilikua kwnye hiyo harusi, nikaona wageniw engi toka nje ya nchi, nikajiuliza na kwney harusi hii usiku kitatokea nini, jibu nimelipata, maana last time harusi ya Heri, ilitoke bonge la mzinga wa ajali , sijui hawa jama wana tatizo gani.

    ReplyDelete
  8. Kichwabuta Mwendantwala - OSLO, NORWAYAugust 01, 2011

    ......funda moja la ziada limewaumbua !!! Ilitakiwa baada ya kutoka kwenye mnuso waende wakapumzike, sasa wao wakaona ndio muda muafaka wa kuendeleza libeneke na ndipo hilo FUNDA LA ZIADA LILIPOWAUMBUA ! Poleni kwa wale walioponea chupuchupu na hilo JANGA la kupoteza MAISHA !!!

    ReplyDelete
  9. Hiyo ni aibu tupu kwani ukialikwa kwenye sherehe lazima unywe mpaka uumbuke

    ReplyDelete
  10. Inasikitisha sana Pole sana Clement na Heba na familia yote kwa ujumla. Vijana wana upendo kwa rafiki yao na walichangamka sana siku ya sendoff tuliwaona. Mungu amlaze mahali pema peoni aliyetangulia maana sote safari yetu ni moja, na waliolazwa wapate ahueni mapema.

    ReplyDelete
  11. Jamani Clement poleni sana ila harusi ilikuwa bomba Pole kwa marafiki zako mungu akulinde. I can imagine how you feel now. Anyway thanks for the lovely wedding party I really enjoyed it. My love to your wife.

    ReplyDelete
  12. Pombe nouma bhana!

    ReplyDelete
  13. Salamu za rambi rambi ziwafikie wafiwa na mola amlaze peponi marehemu. Mola awajaalie wote waliolazwa wapate nafuu na warudie khali ya uzima.Amen.

    ReplyDelete
  14. Hao watakuwa homosexuals

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...