Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya ndege ya Precision Air Michael Shirima akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa safari ya kwanza ya Ndege ya kampuni hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 111, ambayo imeanza safari yake kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Alfonse Kioko na (Kushoto) Mkurugenzi wa TCAA John Njawa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya ndege ya Precision Air Michael Shirima akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa safari ya kwanza ya Ndege ya kampuni hiyo
Baadhi ya abiria wakisubiri kusafiri na Ndege nambari PW 700.Boeing 737-300 ya Shirika la ndege la Precision Air ambayo ilizindua safari yake jana kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini, kwa promosheni ya Dola 57 ili kuwawezesha watu wengi kusafri na shirika hilo
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakisubiri kusafiri na Ndege nambari PW 700 Boeing 737-300 ya Shirika la ndege la Precision Air ambayo ilizindua safari yake ya kwenda Johannesburg Afrika Kusini jana kwa promosheni ya Dola 57 ili kuwawezesha watu wengi kusafiri na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege la Precision Air Michael Shirima wa pili kushoto, Mkurugenzi wa TCAA John Njawa, Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi, Wizara ya Uchukuzi, William Nshama (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara Phill Mwakitawa wakijadilia jambo katika hafla ya uzinduzi wa safari ya ndege ya Precision Air kwenda Johannesburg Afrika Kusini kwa promosheni ya Dola 57.
Precision Air oyeeee! mko juu...
ReplyDeletei msafiri
habari njema!!!! ila rekebisheni website yenu inaboa pale unapotafuta kubook flight ipo very slow na muweke ratiba ya J'bourg trips tujue lini katika wiki kuna ndege.
ReplyDeleteme cjaelewa ni dola 57 au dola 570 nisaidieni kidogo
ReplyDelete